Wazazi kwanini mlitudanganya? Kama kweli mlikuwa mnatupenda, mngesema ukweli

jjs2017

JF-Expert Member
May 25, 2019
2,023
4,213
Habari zenu ndugu zangu

Katika hali isiyo ya kawaida kama kweli kusema uongo ni dhambi basi wazazi wetu wanapaswa kuanza kuchomwa moto na siyo vinginevyo.

Ndugu zangu , wazazi wetu wametudanganya sana kwa kigezo cha kujenga maadili ila kinyume chake wameyabomoa maadili kwa kasi sana

Ni heri mzazi ukawa muwazi na mkweli kwa mwanao maana zama zimebadilika sisi watoto wenu tunajaribu kila kitu ili kujua kama mlichotuambia ni ukweli au ni uongo

Kwanini mlitudanganya wazazi , kwanini mlitufunza kwa uongo na siyo kwa ukweli nia yenu ikikua ni nini hasa

Ndugu zangu wana Jf

a) Wazazi wetu walitudanganya mtoto ananunuliwa , wengine walituambia anapatikana kwenye ndege na wengine walisema wanaenda kumuokota kwenye nyumba za ibada hata wengine kudiriki kutuaminisha mtoto analetwa na mwanga wa jua asubuhi asubuhi

Sisi kama wanao tuliwakubalia ila kadiri umri ulivyo zidi kwenda tuligundua mmetudanganya, tulijaribu kucheza michezo ya "kimama mama na baba" ila tuliona wenzetu wakivimba matumbo na wakienda huko wanarudi na watoto,

Tuliendelea na mchezo wa kombolela ila mwisho wa siku tuligundua kuwa ukilala na mwezako anapata mimba kwanini mlitudanganya enyi wazazi wetu

b) Kwanini wazazi mlitudanganya tuwaambie moja ya mzazi kwamba tunataka mdogo wetu wa kucheza nae na mkiona hatuelewi mnatutengenezea midoli tena bila hata kujali jinsia kwanini lakini.

Kwanini mlitufundisha uongo ili hali mkijua kufanya hivyo ni dhambi , kwanini msingekuwa mnakaa kimnya na kunyanduana wenyewe kwa wenyewe huko.

Sisi vijana na mabinti zenu tumejaribu na tukajua kabisa ukitaka mdogo wako lazima unyandue tena hali iliyopelekea kuwa na unplanned family na unwanted pregnant

c) Kwanini wazazi mlitudanganya hizi nywele za huku ni malaika na hazinyolewi mlikua mnamaana gani kwanini hamkutuweka wazi , japo sisi tulipojaribu kunyoa tukajua ukizikata zinaota tena

d) Kwanini wazazi wetu mlipokuwa mnataka kucheza pamoja mlikua mnatudanganya tukacheze kwa jirani, tukasalimie ndugu au mnatutuma mbali zaidi, wengine mlidiriki kutuambia baba kapumzika nendeni nje mkakae mpaka mtuite huku mkituzubaisha na juice kola tena zile jole juice,

Kama kweli mlikua mnatupenda na mnataka tuwe na maadili kwanini mlitufundisha uongo sisi watoto wenu

e) Kwanini wazazi mlitudanganya ukimtukana, kumpiga au kuitwa na mtu mzima na usipoenda unakatika pua.

Kwanini mlifanya hivyo ilihali mlijua kabisa tutajaribu siku moja ili tuone kama pua zetu zitakatika na tulipo jaribu tuligundua ni uongo mtupu

f) Kwanini wazazi mlitudanganya kuna mtoto wa upande wa baba na mwingine wa upande wa mama, ilihali watoto wote ni wa kwenu na mmewazaa wenyewe .

Kwanini mlitugawa ndugu kama kweli mlikua mnatupenda na mnapenda tuwe na maadili na tuwe na umoja katika maisha yetu

Kwanini mliyajua hayo yote na mlikua mnajua zama zinabadilika na bado mkawa mnatudanganya na hamtuweki baadhi ya mambo wazi,

Kama kweli mlikuwa mnatupenda na mnataka tuwe na maadili mema kwanini mlitudanganya?

Ndugu wenye kujua kwanini wazazi walitudanganya aje hapa na nyie wazazi njoeni hapa kwa pamoja muweke wazi
 
Wazazi ni chanzo kikubwa cha kizazi hichi mnacho kiona
Vaeni viatu vya wazazi waliowatangulia
 
Back
Top Bottom