Usije uka google dalili za Ukimwi kama unajihisi unao "Utakufa kwa presha"

Atalanta

Member
May 25, 2022
59
175
Habari zenu wakuu Hope mko powa kabisa. Kwanza naomba ifahamike kabisa kwamba kuwa na UKIMWI sio mwisho wa maisha kwakua wapo watu wengi wanaoishi na ugonjwa huu lakini bado wanaendelea kuishi vizuri kwa kufuata ushauri wa madaktari.

Pia uzi huu haupo kwaajiri ya kuwanyanyapaa watu waishio na UKIMWI Bali upo kwaajili ya kuburudisha na kutoa funzo kwa vijana wenzangu kwa hiki kisa kiliochowahi nikuta . Okay let's cut the chase "moja kwa moja kwenye mada"

Kuna kipindi niliwahi kupita na Dem mmoja hivi wa mtaani ( Wakati huo nilikua Ni mgeni wa maeneo hayo ) alikua anaitwa Latifa. Aisee Ile ilikua Ni pisi Kali Tena Ni pisi kweli kweli kusema ukweli haikua rahisi kumtongoza Hadi akaja kunikubalia ilichukua mda kidogo. Sasa wakati namfukuzia yule Dem sikuwahi kumwambia mtu mwingine yoyote yule "Lilikua kosa hili" ikafika siku nikamuita magetoni mtoto akaja, aisee tulizagamuana Sana siku ile. Nakumbuka kabla hata hajaja me nilikua nshajipanga nilikua na condom ndani za kutosha Mimi kawaida yangu huwa siuzagi mechi kizembe. Sasa siku ilipofika ya kumuita Latifa magetoni nikasema siwezi uza mechi kwa huyu dem "kwenda kavu" Siku Ile ilikua Kama pepo aliniingia vile Lati alivokuja wakati tunasex alikua ni mtundu hatari nimesex na wanawake tofauti tofauti Ila nikiri Lati alikua hatari Kama ni maua Nampa maua yake. Wakuu nilipaka mkongo na ilikua Mara yangu ya kwanza siku hiyo Kutumia vumbi la kongo Ila alinipigia hiyo kitu inaitwa Tak* tatu aisee dakika tano nyingi Mara paaap nikaanza kuhisi wajomba wanataka kuja wazung hao hapo. Nikahisi labda nimeuziwa mkongo feki baada ya kile Cha kwanza nikaona utam unazidi kunoga nikatoa kondom tupia kwenye dustbin nikataka nicheze Kama Pele lakini Lati akanikatalia akasema vaa Kinga kidume nikawa sisikii kitu kwa wakati huo Yaani nilikua nshapagawa kabisa.

Nikamwambia tuendelee alinisisitiza Sana Kutumia Kinga lakini nikamgomea kabisa baadae akaridhia tukaendelea Hadi tulipokuja kumaliza tulikua hoi kitandani. Ukawa ndio mtindo wangu nikiwa na hamu tu namcheki mtoto anakuja tunasex t But at the end of the day tukaja kuachanaga hatukudum hata miezi mitatu. Kilichofanya tuachane nilikuja kujua kua Dem ana mtu wake mwingine. Sasa nakumbuka siku moja "sitokuja kuisahau hii siku aiseee". Nilikua nipo ndani nacheki Movie Avengers End game ndiyo ilikua yamoto kipindi hicho Nikasikia mtu ananiita Atalanta nikatoka nje kuangalia Nani anae niita alikua Ni rafiki yangu wa chumba Cha jirani akanaiambia oya njoo huku maramoja akaniitia kwenye chumba chake. Basi na Mimi bila kusita nikaenda ili nicheki ananiitia Nini tulipoingia mle ndani nikaona kulikua na marafiki zake wengine Kama watano hivi wao walikua wanacheza PS baadhi nilikua nawajua lakini wengine nilikua siwajui Jamaa mmoja Kati ya wale watano akaniuliza oya unamjua Latifa me nikajua tu hapa atakua anamzungumzia latifa niliye date nae tu wa hapahapa mtaani maan hakukua na latifa mwingine pale mtaani.

Me nikamjibu ndiyo si ni huyuhuyu Latifa wa mtaani hapa ?? Jamaa akasema ndio.. ulishawahi ku date nae ?? akaniuliza tenah. Nikaona hapa hapa ndio pa kujipatia point si nikaanza kujimwambafai kwa machizi pale. Nikasema ndio nilishapita nae Ila kwa saizi sio Dem wangu tenah maana tuliachana, Ila mtoto alikua mtam yule afu anajua ku sex oyaaa ana miguno Kama yote anajua kuifinyia kwa ndani sio pouwa.., yule jamaa akafanya Kam kurudia "anajua kuifinyia kwa ndani eeh". Me nikamjibu Yaani ana hatari afu kwenye miuno ndio hatari zaidi oyaa yule Dem atengwe wanangu. Nikaona machizi wameacha kucheza PS wananiangalia afu Kama wananionea huruma vilee, yule jamaa akaniuliza tenah uliwahitumia ndomu wakati una sex nae ?? Me nkajibu kwa kujiamini kabisa aah ndomu nilitumia mwanzo tu Ila baadae nikatoa nikacheza Kama mpoto afu hiyo ilikua Ni siku ya kwanza siku nyingine tulizo sex ni mwendo ya nyama kwa nyama Kama...

Kabla hata sijamaliza nikaona yule jamaa anatikisa kichwa akasema daah mwanetu tushakupoteza tayar. Nikakosa pozi, wakati huo na Mimi wasiwasi ukaanza kuniingia tayar nIkamwambia oya kivipi mwanangu mbona sikuelewi. Akasema Oya Ommy mchane ukweli Rafiki yako. Ommy ndio yule jamaa aliyekuja kuniita, Ommy Ni mwanangu Sana Yaani Ni marafiki kinoma. Ommy akanaiambia oya em kaachini kwanza usije ukatuangukia hapa Basi na me nkakaa chini akasema Oya kiufupi Latifa ana UKIMWI na watu wengi hapa mtaani wanajua Dem alizaliwa nao na wazazi wake wote wawili washafariki kitambo Sana kwa UKIMWI.

Aisee nilikosa nguvu hapo ndio nikaanza kukumbuka Kuna kipindi Ommy alishawahi kuniuliza Kama natoka na Latifa Ila nikamkatalia nikamwambia kua sitoki nae wakati huo ndio nilikua kwenye process za kumtongoza nikasema Bora ningemwambiaga ukweli tu Ommy nikakumbuka pia jinsi Lati alivyokua nanisisitiza tutumie Kinga. Yaani nilikaa pale ndani Ila mawazo yangu yalikua mbali Sana. Sikusikia hata machizi walikua wanaongea nini nikaamka nakwenda kulala ndani sikula kabisa siku hiyo.

Jioni ilipofika wakati nipo ndani Ommy alijua kabisa kua ntakua na stress akaja ndani akaniuliza oya uko sawa mwanangu, Me nikamjibu hivi unavyoona ntakua sawa kweli kwa hizi story nilizopata naona unauliza makalio ya paka wakati mkia unauona. Ilikua kawaida yangu kutaniana na Ommy. Akaniambia Yaani mwanangu na ulivyokua unajisifia pale Basi ukajikuta Kama John sin vile ukajua Wana tutakusifia eeh akawa ananicheka. Nikamwambia we acha tu mwanangu hapa najiona kabisa siko sawa Ommy akasema usijari lakini Ukianza Kutumia ARV utakua sawa tu na utaizoea hii hari. Nikaona huyu nae amekuja kunivuruga tu hapa Yaani anavyoongea Kama tayari kashanipima afu kanikuta nao. Afu umepika kweli wewe mseng* aliniuliza Ommy wakati huo anaangalia jikoni akaona Hamna kitu akasema nyoo Yaani dogo nakuona kabisa unaenda kufa kwa vitu vitatu Cha kwanza Unakufa kwa Ngoma Cha pili Unakufa kwa Njaa afu Cha tatu Stress. Me nikamjibu wakati huu nilikua mpole kinoumer "Sasa mwanangu napata wapi nguvu ya kula kwa Hali hii". Cheki unavyotia huruma kwaiyo unaniongelea kwa huruma unafikiri ntakwambia pole au afu tataizo lako umezidi Sana kujifanya secret keeper me nilikuuliza tangu siku ya kwanza kuhusu Lati we ukajua me namtaka sijui haya ona Sasa Yaani leoleo tu umeanza kukonda. Alivyosemanimeanza kukonda eti na Mimi nikaanza kujiangalia Mikono nikaoma mbonakama Kama kweli nimepungua hofu ikaanza zidi kuniongezeka. Ommy akatoka nkajua atakua ameenda kwenye chumba chake lakini baada ya Kama nusu saa hivi nikaona ameniletea kiepe yai na soda akasema Oya em acha ufala kula msosi huo. Nikamwambia poa ntakula akasema sio utakula inabidi ndio ule saiz afu dogo kwani Ni mda gani umepita tangu uachane na laifa ?? me nikamjibu Ni kama miezi mitatu iliyopita akasema Sasa ndio unakua na mawazo ya kifala hivyo Dem ushaachana nae mda mrefu hivyo. Nikaona afadhari mwanangu ameanza kunipa moyo saiz. akasema Oya wewe Kama ungekua nao dalili zake ungeshaanza ziona mapema ndani ya wiki tatu Hadi nne Sasa wewe mbona uko pw tu. Me nikamjibu hiyo siyo shida mwanangu Ila me nataka nikapime kabisa nipate uhakika, pengine nnao afu sijijui akasema yeah lakini hapo umeongea point mwanangu si unakumbuka wiki iliyopita ulivyoumwa Yaani wakati unaumwa ukawa unaonesha dalili kabisa Kama Una Ngoma vile. Nikaona hapa nikizidi kumsikiliza Ommy ntavurugika tu. Nikamwambia me nataka kulala niache nipumzike saiz. Akasema Ila kweli mgonjwa inabidi apumzike angalia usije pitiliza usingini ukaamka ukajikuta motoni. Yaani nakwa jinsi ulivyo na dhambi ukifa tu kwanza utaanza kuchomwa na jua afu hata Kama ukienda motoni wewe utachomwa na Moto wa gas. Kusema ukweli maneno ya Ommy yalikua yananichanganya Sana Japokua yeye alikua akiongea Kama utani Ila yalikua yananiingia akilini. Kuna wakati nikaanza kusali kabisa kuwa Mungu anisamehe dhambi na makosa yangu yote. Lakini sema tulishazoena kutaniana.

Baada ya Ommy kuondoka nikawa nimetulia tu ndani najiwazia hatma ya maisha yangu wakati nimetulia kitandani nikapata wazo la ku Google dalili za UKIMWI, sio kwamba nilikua sijui dalili za Ngoma Ila Lilikua Ni wazo tu lililonijia kwa wakati huo. Nikavuta PC na kuingia Google Basi ni kaandika DALILI za UKIMWI Ni zipi. Ndugu zangu nilijuta kwanini nime Google. Baada ya kuingia Google Basi ikaja linki iliyo nipeleka moja kwa moja Hadi YouTube ambayo ilikua inasomeka DALILI za UKIMWI zinazojitokeza wiki Moja baada ya mtu kuambukizwa. Nikatulia kwa makini nikiangalia Ile video nikaona wakaanza kusema mtu anaanza kukohoa na kweli na Mimi nikafikiria nikakumbuka kua mbona Kama Kuna kipindi nilikua nakohoa sana, baadae kidogo tenah wakasema mtu anaa kutokea na vidonda pembeni mwa mdomo nikaona hii dalili Mimi sijawahi kuwa nayo. Sasa nikaanza kujigusa pembeni mwa mdomo wakati naendelea kujigusa nikaona Kama Kuna ka kipele nikashtuka nkajisemea hiki kipele kimeanza lini tena Mara kikaanza ku washa nikaanza kujikuna nikitaka kuacha kinazidi kuwasha, nikaanza kuogopa Yaani kiufupi kila dalili nikawa naiona kwangu. Nikatoka kwenye Ile channel Nika Google Tena dalili za HIV. kwenye dalili kumi Basi Tano lazima niwe nazo aisee sikuacha kuona kila rangi siku ile. Tena unakuta wanaandika kabisa eti sio lazima mtu awe na dalili zote ukiwa una baadhi ya hizo dalili tu Basi uwahi hospital Yaani hapo ndio wakawa wananichanganya zaidi.

Nikazime PC nikasema saiz nalala huo usingizi ulikuja Basi Yaani kila nikitaka kulala naona ubongo wangu unaanzisha maada mpya ya kui discuss. Kuna muda nikaanza kukumbuka mafundisho ya dini pia jinsi nilichokua naambiwa kuhusu zinaa. Ikafika kipindi likanijia wazo lingine nikawa nadiscuss kichwani mwangu kwanini nisiingie play store Ni download app ya HIV test nijihakikishie Kama ninao au Sina ??. Nikachukua sim nikaingia Play store Nika download app moja ya HIV tester wakaanza kuniuliza maswali at the end wakasema niweke kidole gumba na Mimi nikaweka ika load... afu ikaniambia kua Niko safe Sina HIV hapo nikapata afazari oya niliruka ruka nikamuita Ommy kwa furaha oyaa ommyyyy oya wewe kmmmk* njooo njoo we matak* njoo uone.
 
FB_IMG_16950225274312547.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom