Sitosahau mara yangu ya kwanza kuingia Barbershop

Atalanta

Member
May 25, 2022
59
175
Katika maisha kila mtu anakuwa na matukio ambayo siyo rahisi kuyasahau hata akumbwe na changamoto ya namna gani.

Leo na mimi nimeamua ku share na nyinyi Wana JF tukio hili ambalo sio la kutisha Bali Ni la kawaida tu Ila naimani linafunzo ndani yake, moja kwa moja tuanze Sasa..

Wakati huo nilikua nimepangiwa chuo Mbeya pia hii ilikua ni Mara yangu ya kwanza kwenda mbeya ijapokua sikupenda kabisa kwenda mbeya lakini Post zilivyotoka ikaonesha nimepangiwa MZUMBE mbeya.

Sasa si unajua life la First year ( Hapa ndipo story ilipo ) huwaga kunakuwaga na matukio mengi sana, Kuna kuuziwa dhahabu fake ingawa niliwakwepa Hawa jamaa, kupewa hela fake, kutolewa nywele mdomoni n.k Sasa vituko vinakuwaga vingi hasa kwa wale wenzangu na mimi wanaotokea bush Yaani vijijini Hawa ndio hukutwa na Mikasa ya hatari zaidi.

Zilipita sikuchache baada ya kuanza masomo Sasa nywele zangu zilikua zimekua hivyo nikaamua kutafuta saloon ili nikanyoe, katika kutafutatafuta nikaona saloon moja iliandikwa barbershop Basi na Mimi bila hiyana nikaingia mle ndani moja kwa moja. Nakumbuka wakati nimeingia mle ndani kidogo nianguke Ile saloon kwa nje ilikua nzuri Sana Ila kwa ndani ilikua nzuri zaidi Yaani malumalu zake zilikua ni nzuri kidogo niteleze (hahaaaa ushamba huu jameni).

Mle ndani kulikua na vinyozi wawili ambapo kwa wakati huo wote walikua wakiwahudumia wateja wengine. Sasa mmoja akaniona wakati huo me bado nimesimama nashangaa shangaa mle ndani yule kinyozi mmoja akanichangamkia "Dogo kaa hapo" aliniambia huku akinionyesha sehem ya kukaa.

Nikajiona mjinga kwa kushangaa shangaa mle ndani nikahisi huenda jamaa aliniona Kama wakuja sijui, Basi nikakaa kwenye sofa. Mle ndani kulikua na masofa ya kuwatosha watu watatu yalikua mawili. Sasa Ile kukaa daaaah Yaani lile sofa lilikua Ni laini hatari ukikaa linabonyea flani hivi afu ukiinuka linakua Kama Lina ku push hivi Yaani kama linakuja juu. Basi nikawa nazidi kushangaa shangaa tu

Wakati huo wote mfukoni nilikua na buku jero tu ambaapo nilipanga buku ya kunyolea na jero ya nauli kurudi Hadi chuo. Bhana bhana si nikajua eti wananyoa kwa buku. Na Mimi hata sikushtuka tu mazingira ya Ile saloon kua hapa sio level zangu aaah. Sasa baada ya muda kidogo Kama dakika Kumi hivi Kuna jamaa akaja na gari ilikua ni V8. niliweza kumuona kupitia vioo vilivyopo mlangoni pale saloon vile vioo vilikua ni tinted me namuona wa nje Ila wa nje hanioni Mimi. Sasa nikawa naishangaa lile gari ili nione atakaeshuka nikaona akashuka jamaa mmoja hivi alikua na madevu kama ya Rick Ross madevu yake jamaa yalikua yanang'aa weusi nafikiri ni kutokana na matunzo aliyokua anayapatia, yule jamaa akaingia Hadi mle ndani nikaona wale majamaa wanamchangamkia hapo ndio nikajua kua yule jamaa ni mwenyeji pale Basi me nikamsalimia akaitikia salamu yangu afu akakaa karibu yangu.

Sasa hapo ndio nikasikia vizuri harufu ya marashi yake yalikua yananukia vizuri sanaa. Sasa hapo ndio nikaanza kushtuka kua hapa nilipoingia sio level zangu, Machale ndio yakaanza kunicheza kua hapa hapawezi kua kunyoa buku. Nikawa na discuss na halmashauri ya kichwa changu naanzaje kuondoka hapa ili wasinishtukie.

Baada ya kufikiria kwa mda kidogo nikaona bhana eeh me ngoja niamke niende tuu Sasa Ile nimenyanyuka niondoke jamaa mmoja akawa amemaliza kunyoa tayari kwa kinyozi mmoja Tena ndio yule kinyozi aliyopo upande wangu kwaiyo wakati Mimi nimenyanyuka niondoke yule kinyozi akajua ndio najiandaa ili nipande kwenye kiti.

"Dogo inaonekana una haraka Sana eeh" aliongea yule kinyozi huku akisafisha kile kiti alichotoka yule mteja mwingine. Hapana brooh Ila nimeona niondoke tu ntakuja Tena baadae kunyoa. Niliamua kudanganya ili niondoke, hapa ilikua baada ya kushtuka kua hapa sio pa buku hapa. Sasa yule kinyozi baada ya kuona vile nataka kuondoka yeye hakujua kua Sina hela Ila nahisi alikua anajua kua nataka nimfanyie janja nisepe mazima.

Wakati huo tunaongea yule mteja aliyekua ananyolewa alikua tayari ameshatoka kwenye kiti. Sasa nikabaki Mimi na yule kinyozi tunaongea wakati huo Kwenye sofa pale kulikua na yule brooh mwenye madevu amekaa, Sasa wakati tunaongea yule jamaa mwenye madevu akasema "Dogo si ukae unyolewe watu tupo tunasubiri hapa ujue oy Emma em mnyoe huyo dogo Basi" aliongea bonge na ndio hapo nikajua kua yule jamaa kinyozi anaitwa emma.

Nikaona hapa nimekamatika nikaamua kujitoa muhanga ikabidi nimuulize yule kinyozi " samahani broo lakini hapa kunyoa kwani ni shilingi ngapi ??. "Haaa!! kumbe dogo ujanja wote huo alafu unaogopa bei ya kunyolea hapa ndio maana unataka kuondoka sio " aliongea yule kinyozi. Nikamwambia hapana brooh Ila nahitaji tu kutambua bei ya kunyoa Ni shilingi ngapi?

Wakati namuuliza hivyo nilikua bado sijakaa kwenye kiti Cha kunyolea nilikua nimesimama yunaangaliana na kinyozi yule "Emma". Nikamwambia broo Mimi Nina hela .... kabla hata sijamaliza yule Big akajibu dogo em kaa unyolewe bhana kwani unaogopa Nini mbona hapa kunyoa ni bei ya kawaida sana.

Nikatulia afu nikamwangilia yule bnrooh Emma nae akasema yeah dogo we kaa tu kwenye kiti hapa kunyoa ni bei ya kawaida sana. Kila nikitaka kukaa naona nafsi inagoma kabisa naona Kama "inaniambia wewe kima hapa kunyoa sio buku hapa ukinyoa kitakacho kukuta usimlilie Mungu", Nikamuuliza yule broo Emma Tena brooh me naomba nijue bei tu Ni shilingi ngapi ya kunyoa jamaa akanijibu tenah kua nisiwe na hofu bei yao ni rafiki tu me nisiwe na wasiwasi nikae tu ninyolewe. "Kwani wewe dogo Ni wawapi wewe au Ni mnyasa" Yule big aliongea hivo, aisee nikamwangilia yule jamaa afu nikajisemea Yaani Mimi Atalanta ambae home naonekana Mimi ndio mjanja Leo hii naambiwa eti me mnyasa..?? Daah nikaona isiwe kesi nikakaa kwenye kiti kidume ili ninyolewe pasipo hata kujiuliza tenah Mara mbilimbili.

Aisee yule jamaa alivyokua ananinyoa ndio alikua anazidi kunivuruga kabisa yaan, kwanza aliniuliza nikunyoe style gani..?. Nikafikiria kidogo kwa wakati huo me nilishazoea nikienda saloon ni kunyolewa tu Sasa hapa eti naulizwa ninyolewe style gani duuuh makubwa haya, afadhari ningekua najua hata jina la style hata moja bas ningemwambia lakini kwa wakati huo sikuijua yoyote Ile.

Nikabaki namkodolea mimacho tu jamaa akaniuliza tenah oy dogo unataka nikunyoe style gani..?. Nikawa najiuliza tenah moyoni nikasema hapa unaweza kuta kila style na bei yake Sasa nikianza kumwambia aninyoe mtindo wowote anaweza ninyoa style ya bei kubwa afu nikashindwa kulipa, nikamwambia kwa kujiamini kaabisa ninyoe style ya bei ndogo kuliko zote. Khaaaa!

Yule big akasema wewe dogo vipi mbona unatuletea vituko hapa Sasa ndio style gani hiyo, yule kinyozi akamwabia oy tulia mkubwa ngoja nimweleshe dogo inaonekana ni mgeni hapa mjini. Basi yule kinyozi akaniambia kua nitaje style yoyote Ile ataninyoa kwa gharama Ile Ile. me nikamwambia kua nilijua kila style inabei yake akaniambia hapana style zote Ni bei moja tu. Nikamwambia bas ninyoe unayoona wew Ni nzuri, Niseme ukweli tu Yaani kwa siku ile Kama yule Big mwenye madevu ndio angekua ni kinyozi nahisi angenitimua pale pale tenah na makofi juu maana jamaa alikua ana Ni mind hatar. Kinyozi Akaanza kuninyoa sasa huwezi amini naweza sema huenda Ile ndio saloon niliyotumia mda mrefu kunyolewa nilitumia Kama dakika 1
20- 30 kunyolewa tu.

Aisee jamaa alivyonimaliza Ile kujicheki kwenye kioo daah nilipendeza hatariii nikasema kweli majamaa wanajua kunyoa.

Sasa nilipotoka kwenye kiti Cha kunyolea nikawa najipukuta pukuta nywele kichwani na mikono yule kinyozi akaniambia oy dogo usijipukute utajichafua hapo bado hujamaliza.

Sikumuelewa anamaanisha nini alivyosema vile kua sijamaliza nikajua alikua nanitania sababu Hadi nanyolewa yule Big alikua akinitania Sana mule saloon. Me nikamjibu yule kinyozi "aah hapa mbona haina shida brooh nishamaliza hapa alaf...." Sikumaliza hata kuongea nikamsikia yule kinyozi mwingine anamuita mdada mmoja alikua nje "wee asha wewe afu mbona unajisahau Sana au haujaona wateja humu ndani afu we unakaa kaa nje tu " Sasa me nikajiuliza huyu asha anakuja kufanya nini tena nikajiongeza nikasema aah huenda atakua anakuja kufanya usafi labda. wakati huo nilikua najipukuta huku najiangalia kwenye kioo hapo.

Sasa Ile niangalie mlangoni ili nimuone asha mwenyew, khaa mama yangu nikabaki nimeganda Tena namuangalia tu alikua mdada mmoja mzuri mweupee pee sio mnene Sana Ila anashepu nzuri yakuvutia, wakati bado namshangaa yule Asha nikaona Kama upande wa pili Kuna mtu ananiangalia si unajua Kama mtu anakuangalia sana unaweza hisi tu kua Kuna mtu anakuangalia kwa muda mrefu, nilipogeuza shingo niangalie Nani anae niangalia huyo Basi nakakutanisha macho na yule big afu akasema "kua makini dogo mjini hapa".

Nikabaki najichekesha tu nikahisi mkono wangu umeshikwa na mkono laini aisee kidogo nipige ukelele Sasa Ile niangalie Nani aliyenishika mweee mwee mweee si nikaona Asha ndio kanishika mkono akasema ndio wewe ?? Kama kawaida yangu nikabaki nimeduwaa tena Sasa hapa najibu nini Mimi. Nikamuangalia Emma sikumwabia chochote Ila Ile angalia yangu tu alishajua kipi namaanisha. Yule kinyozi akaniambia dogo mfate huyo Dada nend nae humo "akionesha kichumba kingine kilichopo mlemle ndani" atakuosha hizo nywele.

Nikaona mmh hapa Leo nimeyakanyaga hapa naona kabisa nimeyakanyaga kiufupi Leo nitajibeba, Nikamwambia kinyozi brooh me kuhusu kujiosha ntaenda kujiosha hata hosteli we usijari. Akasema Dogo najua utakua unawazia kuhusu bei Ila kwa sisi hapa tunafanya bei moja Yaani mteja akinyoa tu nilazima aende huko kwenye hicho chumba ili asafishwe bei ya huko Ni hii hii ya kunyolea Hapa.

Hiyo huduma ya huko ni ya ziada tu hata Kama usipoenda huko Ila bei Ni Ile Ile moja tu kwaiyo Bora uende tu. Nikajisemea haya makubwa Sasa, Ikabidi nimfate yule dada anaeitwa Asha ambae alienda kwenye kile chumba kingine. Nilivyoingia mle ndani nikaona kulikua na kiti Ila sio Cha plastic na Wala sio Cha mbao sijui kipoje kipoje kile kiti pia kulikua na kitanda.

Basi nikaambiwa nikae pale kwenye kile kiti nikakaa kidume kutoka moro.Yule mdada Asha akakiminya kile....

Mwendelezo: Sitosahau mara yangu ya kwanza kuingia Barbershop
 
Mi niliwekewa dawa ya mmba bei yake 5000 na kunyoa 5000 jumla 10,000.

Niligoma, nikawambia mi sikuwambia mniwekee hiyo dawa pia nikawauliza ni dawa gani hiyo mpako mmoja 5000???😂😂😂😂
 
Back
Top Bottom