Ushauri wenu unahitajika hapa

wamasai walinipima kama nina uwezo wa kumuoa binti yao wakaropoka mahari million 4 wala sikulalamika, kulia lia au kuomba wapinguze mahari.

Nikawauliza "mnaitaka mda gani hiyo hela?"

wamasai wakwe wakajibu "hata sasa mda huu kama unayo lipia"

nikapandisha suruali juu mguu wa kulia nikashusha socks nikatoa million 2

nikapandisha suruali juu mguu wa kushoto ikatoa million 2 nikawapa

wakataka kuhesabu nikawahibu haina haja wasiwe na wasiwasi imekamilika

nikatoa laki mbili nikaagiza vinywaji sikujua kumbe wamasai wanajua kucheza twaarabu. Zikapigwa nyimbo za mzee Yusuph "nitadumu nae kwa nguvu za manani, na waseme shauri yao....."

nimezaa na mmasai wangu watoto wazuri waarabu kama baba yao😀
View attachment 2660470

Mwaraaaabuuu
 
Habari ya uzima ndugu Wana JF,, poleni na majukumu ya kila siku.

Nimempenda binti wa kimasai naniko tiyari kwenda kwao kufanya taratibu za kuoana. Ugumu unakuja kwa kaka zake hawataki dada yao aolewe kwa mwanamme asiye masai. wakati huo mama wa binti amekubali na hajui kiswahili na namna ya kuongea naye vigumu.

Kaka ake mkubwa ndo mlezi mkubwa aliyemlea binti tangu mdogo pindi baba yao alipofariki. Binti wa wawatu amekufa ameoza kwangu kama ilivyo kwangu.

Naombeni ushauri wenu wenye experience na case hii. Natanguliza shukrani kwenu wakuu.
Hajakeketwa?
 
Tafuta mkalimani wa kimasai nenda kwa mama mkamalize taratibu zao.

Hao wakaka usihangaike nao
 
Tafuta mkalimani wa kimasai nenda kwa mama mkamalize taratibu zao.

Hao wakaka usihangaike nao
Mama mtu hana sauti mbele ya vijana wake. Vijana wake wameshikilia kipengele Cha waswahili( makabila tofauti na wamasai) hawezi kujenga boma( kudumu na familia).
 
Mapenzi yalinitia upofu kama wewe, ila niliishia kuachana na mwanamke akiwa na mimba ya miezi 9, akazaa after two weeks

nimejifunza kupita kiasi.

tani hata akigoma mtoto wa miaka mitano, sitaoa kamwe!!
 
Mtoroshe...huwa wamasai wanamila ya kuoa kwa mwanaume kumtorosha binti na wewe fanya hivyo....yaani anahamia kwako bila idhini ya wazazi. Watakupiga faini maisha yanaendelea.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom