Naombeni ushauri wa haraka kwa niaba ya rafiki yangu kipenzi

Cryspina

JF-Expert Member
May 1, 2020
298
392
Habarini.

Waungwana nakuja mbele yenu na majanga ya rafiki yangu kipenzi na ninahitaji ushauri wenu wa busara. Naomba tusilifanyie hili swala nitakaloleta hapa mzaha bali ninaomba tushauriane kwa busara na hekima ili mimi nimshauri huyu rafiki yangu.

Ipo hivi, nina rafiki yangu best sana. Ambaye hapa katikati miaka kama minne nilikuwa mkoa mbali na yeye. Na kwa kipindi nimekuwa nae mbali ndipo yakamsibu yaliyomsibu

Ipo hivi. Huyu rafiki yangu kwa bahati mbaya ni yatima, wazazi wameshafariki, alianza baba, akaja mama mwaka 2006. Yeye kwa sasa umri wake ni maika 23. Kipindi wazazi wake wanafariki alikuwa ni binti mdogo sana na alikuwa bado yupo sekondari O Level.

Aliachwa katika care ya dada yake mkubwa wa kwanza kuzaliwa. Ila kwa bahati mbaya huyu dada hakuwa msimamizi mzuri na ndie amechangia majanga. Dada huyu alipokuwa akiishi na huyu rafiki yangu, alikuwa anatabia za kuwa na wanaume tofauti tofauti na ulevi, hivyo hakuwa na influence nzuri kwa binti huyu.

Kulikuwa na kijana m'moja alikuwa akimtaka huyu binti kipindi akiwa shule. Na dada yake alikuwa anampigia pande huyo kijana kwa kumtuma mdogo wake kwa huyo kijana mara kadhaa. Binti alishamchomolea sana huyu kijana na kwa vile alikuwa bado binti mdogo wa miaka 16 hakujua yanayokaribia kumsibu. Yule kijana, sikumoja, alimtegea kilevi kwenye kinywaji na kumuingilia jambo lililopelekea kupata ujauzito on the spot. Alipokuja kumwambia dada yake, dada yake hakuwa msaada kwa lolote ni kama alimuachia apambane na hali yake.

Binti alipomwambia jamaa alikataa na kumkana kuwa huo sio ujauzito wake alee mweneywe,so akafanya hivyo. Baada ya kujifungua mtoto wa kike(i can't go into details to keep the story short) akaendelea kupambana na maisha mwenyewe kwa kufanya shughuli ndogo ndogo. Shule alimaliza kipindi anapata ujauzito but kutokana na ile hali hakuweza kufaulu so aliamua kuachia form4. Baadae kwenye mwaka 2015 alikutana na jamaa baada ya dada mtu kumpa jamaa story za mdogo mtu kuwa analea mtoto mwenyewe, so jamaa alipomtafuta yule binti alimbembeleza jamaa akaishi nae, so akaenda na wakaanza kuishi.

Huyo kijana anafanya kazi kampuni ya tourism akawa anaishi na binti na huyo mtoto wao. Wakiishi, yule kijana alikuwa akifanya vimbwanga kama kutukana matusi, kujihusisha na wanawake, ulevi wa pombe na bangi. Binti alivumilia haya sababu hana pa kwenda. Wazazi hawapo, dada yake wa kwanza ndio huyo maisha yake si ya maadili, ndugu zake wa kiume watatu waliosalia hawana ramani baada ya wazazi kufariki wamekuwa ni watu wa majanga kwenye maisha yao hawana uelekeo wa maisha wanabangaiza kuishi.

Binti akavumilia manyanyaso na kukosa amani ya moyo kuishi kwa masimango na kudharauliwa. Mwaka 2017 mwezi wa tano, katika pitapita zake akakutana na kijana alikuwa mwanafunzi wa chuo mwaka wa 3. Katika kusalimiana na kubadilisha mawasiliano wakajikuta wameangukia katika penzi zito sana.

Huyu kijana alikuwa ametoka kuachana na mpenzi wake aliyekuwa nae tokea mwaka 2013. Kwa kipindi chote hiki hadi wakutane na huyu best yangu mimi akawa akinihadithia tu namna huyu kijana alimjali na kumpenda na kumpa attention ingawa alishamuelezea situation yake ila huyu kijana alizidi kumpenda. Mwanzo alidhania pengine kijana yupo nae sababu ya tamaa za mwili, ila alikuja kugundua ni zaidi ya hilo.

Penzi lao lilimea sana hadi huyu binti akaanza kusahau maumivu na kujikuta ana faraja tena. Huyu kijana ilipofikia mwaka 2017 mwezi wa kumi alikuwa ameshamaliza muda wake wa masomo na alikuwa anajiandaa kurejea Dar. Lakini kutokana na penzi lilivyomea na hali aliyokuwa nayo huyu dada, kijana akamwambia yeye atakuwa ready kufanya nae maisha sababu ameona yeye ni mwanamke wa kaliba yake na hata kama ameshakuwa na mtoto atampokea hivyo hivyo.

Binti alikuwa ameshakubali ila moyoni alikuwa hajiamini sijui no utoto. Wakakubaliana na kijana huyu mpya kuwa, atakwenda Dar kuandaa mazingira ya kuishi nae so ampatie miezi kama miwili yaani wa kumi na moja na kumi na mbili kisha atakuja mchukua. Waende kuanza maisha, na kwa wakati huo asionyeshe dalili yoyote kuwa anataka kuondoka kwa huyu mwanaume aliyezaa nae ambaye haishi na yeye vizuri.

Basi yule kijana masikini akaenda Dar, akajikusanya kwenye vidili vyake akaweza kusecure sehemu ya kuishi kwa kuanzia yaani chumba sebule. Katika kipindi cha October na December, huyu binti alikuwa hapatikani hewani na sababu mojawapo ni jamaa kumvunjia simu mara kwa mara na kumkataza asiwe anawasiliana na mtu yoyote hata nduguze. Kwa wakati wote huo akiishi nae hakukuwa na ndugu aliyekuwa ameshirikishwa, kwa kifupi jamaa alianza kuishi na huyo binti kiholela.

Basi yule kijana kwa shida sana alikuwa akimtafuta huyo binti na hampati hadi alipokuja mpata hapo mwezi wa kumi na moja mwisho kwa kutumia simu yangu nilipokwenda msalimia. Nilimpatia kisimu changu cha tochi at least asikose mawasiliano. Mara nyingi huyu jamaa wake alikuwa anasafiri na anarudi baada ya mawiki aidha mbili au moja. Hivyo muda mwingi huyu binti alikuwa anakuwa mwenyewe.

Huu mpango wa yeye kuanza maisha mapya na huyu kijana wa dar aliponishirikisha mimi niliunga mkono sababu niliona the type of hell anapitia. So nikamwambia ana baraka zote na haitakuwa shida akienda kwa huyu kijana mpya.

Wakati mambo mengine yakiendelea, mwezi wa 12 nikaja kushangaa bibie ameniita anipe taarifa kuwa anahisi ana ujauzito wa mwezi m'moja wa huyu jamaa wake anaeishi nae na hajui atamwambia nini yule kijana wa Dar kwa maana ameshamwambia yupo tayari kuja kumchukua na mtoto waende Dar kuanza maisha mapya.

Nikamuuliza imekuwaje sasa hadi na yeye amefanya hivyo kuzaa na mwanaume bedui asiye eleweka. Akanambia kuwa kuna wakati, yule mwanaume anaeshi nae alifumania simu na akaona mazungumzo yote akaingia baridi ya kumpoteza so akamsihi amsamehe mapungufu yake na anaomba waimarishe uhusiano ndipo akajikuta amerudisha moyo nyuma na pia influences ya baadhi ya marafiki zake wengine waliomwambia asiwaamini wanafunzi wa chuo wengi ni matapeli wanakuwa na haja ya ngono tu wakimaliza chuo wanaanza maisha mapya na wapenzi wapya so yeye ni bora abakie na huyu aliye nae kulikoni kuanza na stranger.

So anashindwa ni namna gani atamueleza huyu kijana wa Dar anaomba nimsadie kumwambia yeye hana huo ujasiri. Na hata akiwa mjamzito, walienda kujiandikisha ndoa zile wanaita za fasta za Roman, wakafunga ndoa bila upande wa binti kuhudhuria ndugu yoyote, na upande wa jamaa yeye alikuwepo mama yake wa kambo, baba yake mzazi, na rafiki na majirani binti hakuwa na muwakilishi yoyote sababu kaka zake na dada yake hata walipopata taarifa wakasema hawawezi kwenda maana hawajaridhia aina ya kuishi walivyoanza.

Basi mimi ikabidi nijitoe ufahamu nimtafute yule kijana wa Dar nimpe ile habari mbaya. Kiukweli ile habari ilimvuruga sana akili yule kijana kiasi kwamba alikosa amani na kuumia sana moyo wake. Akahoji sana kuwa amekosea wapi mbona walishakubaliana.
Basi yule kijana tokea hapo akawa wa baridi na akawa kimya kwa muda na hakumtafuta huyu binti kwa kipindi kidogo. Ilipofika mwezi wa tatu, huyu binti alimtafuta yule kijana wa Dar na kuzungumza nae na ikiwemo kumuomba radhi kwa yaliyotokea na kumwambia ilikuwa ni bahati mbaya.

Huyu kijana wa Dar kwa namna alivyompenda aliendelea kuwasiliana nae. Na mwezi wa nne mwaka 2018 alienda na wakakutana akimwa mjamzito hivyo hivyo na walifanya mapenzi mara nyingi sana ndani ya wiki 3 alizotembelea na kurudi Dar wakaendelea kuchat kama wapenzi.

Binti akajifungua salama mtoto wa kiume. Ila maisha hayakuwa tofauti ma mwanzoni, tena hali ya manyanyaso kutoka kwa huyu mwanaume wake ikazidi. Binti akajaribu kuvumilia ila uvumilivu ukamshinda kabisa.

Kama kawaida akaanza mtafuta tena yule kijana wa Dar. Ambaye kwa wakati huu alikuwa ameshaanza kazi na anaishi pekee yake bado. Kijana hakuwa na ule moto kama wa kwanza, wala mshawasha hata kidogo isipokuwa alikuwa anapokea simu na kuwasiliana na binti basi ila si kumtafuta. Mimi alikuwa ananipa michapo yote na nilimwambia sasa unataka mtu afanyaje jamani na umeshamfanyia ulichomfanyia unahisi yeye hana moyo?!

Siku zikaenda wakiwasiliana kimachale hadi mwaka huu 2020, binti alikuwa anaongeza kasi ya mawasiliano na kijana na kujaribu kumjengea ushawishi mpya kwa kuomba msamaha na kujitahidi kumpa attention yote. Kidogo kidogo akaanza kumshawishi kijana kurudisha hisia kwake. Kipindi cha corona ndipo aliweza kupata muda mwingi wa kuongea nae na hii ikasaidia wao kufufua upya mawasiliano yao na kuanza kuwa karibu hadi kijana kuanza tena mpigia simu.

Mawasiliano yamekwenda na kijana kama ameanza kurejesha mawasiliano vizuri tena kwa bi dada. Sasa anasema kwa hivi sasa yeye na huyu jamaa anaeishi nae hakukaliki na wanawashiana moto balaa. Amezungumza na huyu kijana wa Dar japo akamtembelee na kijana amekubali na inaonyesha hana mwanamke maana wamekuwa wakiongea hata saa sita za usiku na hata kuchati na simu hajaonyesha dalili ya kuchat nae kwa mashaka so hana mtu anaishi nae.

Sasa bi dada ndipo akanipa scenario kama hivyo akitaka ushauri. Yeye anataka kumuacha huyu jamaa na hataki amwambie maana ataleta upinzani na fujo anataka amfanyie ambush. Anasema huyu jama alishazaa na wanawake wawili kabla yake na anawatoto nao na amewaacha huko haangaiki nao.

Yeye ndio hivyo ameshamzalisha watoto wawili. Anachotaka anajua akiondoka na hao watoto watakuwa ni mzigo wake pekee na yeye plan yake ni kuwa na huyu kijana wa Dar maana ameshaona ndie aliyetakiwa kumfuata tokea mwanzo. Sasa anataka kuwaacha watoto kwa baba yao ili asijekumpa huyu kijana mzigo maana yeye akiondoka na hao watoto na kwasasa hana uwezo wa kuwalea anahisi atakuwa mzigo kwa yule kijana na hataki kumpoteza kwa maana alishachezea hiyo nafasi mwanzoni.

Roho inamuuma sana kutaka kuwaacha watoto. Ameshamuuliza huyo kijana endapo anaweza mpenda yeye na kufanya nae maisha katika hali ya sasa, vipi watoto, kijana wa Dar alimjibu kuwa yeye hawezi jihusisha na maswala ya watoto kwasababu ni swala la wazazi wawili wanaotakiwa amua hatima ya watoto wao, yeye hawezi semea chochote.

Sasa bibi dada yupo njia panda, jamaa kamwambia anytime aende akijisikia. Yeye anawaza hawa watoto, ataanza nao vipi maisha mapya, au je awakabidhi kwa jamaa apambane na damu yake yeye akaanze ukarasa mpya na jamaa yake... Na jamaa wa Dar amemwambia haina shida kama anataka kwenda.

So, yupo njia panda afanyaje, hana jibu.

Naombeni maoni yenu wakuu nikamshauri rafiki yangu yupo katika wakati na kipindi kigumu sana. Yeye ni 23 years kijana wa dar ni 29. Huyu jamaa yake ni 37 na hana uelekeo wa maisha, wamepanga chumba sebule, jamaa akipata pesa anatapanya yote, hataki mshirikisha mipango yake, hajui anafuture gani na wala ahangaiki kuwaza.... Anampa wakati mgumu huyu binti.
 
Lazima apoteze sehemu moja ili abaki na moja na asipoangalia atapoteza sehemu zote mbili.

Iko hivi, jamaa wa dar ameshajua kuwa yeye ni kama spea tairi tu na ndio maana yule wa mwanzo alivoahidi kutulia basi bibie na kitumbua katoa.

Asitarajie akija dar atayapata yale mapenzi tarajiwa (labda amroge na kama angekuwa fundi wa kuroga basi angemroga baba watoto wake ili atulie) kwa sababu tajwa hapo juu na akijichanganya akaja na watoto ndio kabisaaa watamwagikana kabla hakujapambazuka.

Kama vipi atulie tu na baba wa watoto wake labda atatulia huko mbele ya safari maana huku dar alishachezea shilling chooni na wanasema bahati haiji mara mbili. Na jamaa akimkubalia kuishi naye basi ajiandae kupokea wake wenzie na hamna wivu, ye kayaanzisha wacha mshikaji ayamalize.
 
kijana wa Dar alimjibu kuwa yeye hawezi jihusisha na maswala ya watoto kwasababu ni swala la wazazi wawili wanaotakiwa amua hatima ya watoto wao, yeye hawezi semea
Hii sentensi aitafakari sana huyo rafiki yako ina maana kubwa sana, Alipo haribu rafiki yako kupata mimba ya mtoto wa pili. Huyu mwanaume wa dar kishaondoa uaminifu kwake, kama atakwenda dar aende peke yake kwanza ayajenge mapenzi upya na uaminifu aufanye wa hali ya juu kabisa yaani hata kama anataka kuongea na watoto wake, jamaa wa dar lazima awepo ili kuondoa wasiwasi kwa jamaa wa dar. Baadae penzi likisha simama vyema anaweza mvuta mtoto mmoja mmoja, lakini cha muhimu arudishe uaminifu kwanza wa hali ya juu kabisa.


Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
Mabinti wengi wa kizazi hiki hawana akiri, kuzaa na mtu kusikufanye ukawa mtumwa kwake. Achana nae anza maisha yako tulia na Mungu atakupa kilicho bora.

Hapo ata akienda dar yanaweza kutokea kama yanayo mtokea sahv tu maana bado ajajitambua
 
Hii ngoma ngumu sana, swali langu vp kuhusu uyo baba mtoto wake hizo tabia zake za mibangi na mipombe vp zinarekebishika au lah? Na je alishafanya jitiada za kumbadilisha au? Labda niongee kitu dada angu uyo rafiki yako kashalikoroga tayali kikubwa ninacho kiona mimi uyu jamaa wa dar ni ngumu sana kufanya nae maisha Cha msingi ambacho inapaswa afanye apambane hili uyo baba watoto wake aache pombe inawezekana kabisa, kama amtafutie dawa za asili amwekee kwenye chakula hili aache pombe kama kwenye maombi sijui kwa shehe ndio ajitaidi mana hakuna namna Ila mawazo yangu ni ayo ajitaidi atafute dawa za kienyeji huwa zinasaidia natumaini akiacha mapombe uyu mjomba basi atatulia na familia yake
 
Duuh huyo alishaharibu ajipange kuondoka kwa mmewe akalee tu watoto wake peke yake maana akija Dar ataletewa tu wake wenzake huko mbeleni na hatoweza kuhoji
 
Nashindwa kumlaumu, kwanza ni kutokana na umri alionao na msingi mbaya ambao ameupata tokea akiwa mdogo, alikosa upendo, akakosa uangalizi, akakosa usimamizi, akakosa ushauri akakosa role model yaani inshort amepitia mambo mengi magumu katika umri mdogo sana, yupo kwenye kundi la umama wakati bado ni binti mdogo sana, hapo kwanza anahitajii msaada wa kisaikolojia, so decision na mistake zoote ambazo amezifanya its not her fault maskini, i feel so sory for her.

Nnachoweza kukwambia wewe rafiki ni hivi, mwambie asithubutu kuacha watoto wake, yeye ni victim tayari wa kukosa malezi mazuri akiwa mdogo na ni kwasababu alikosa wazazi akabakia na walezi walioharibu future yake, asirudie kosa hilo kwa watoto wake, the way umeelezea huyo baba yao alivyo akiachiwa watoto pata picha wataishi maisha gani? watakuja kuwa watoto wa aina gani? sana sana na yeye ataenda kuwabwaga kwa ndugu ajinafasi vizuri kwa bangi na pombe na wanawake wengine.

Kama ndoa imemshinda, kwa huyo jamaa aanze upya maisha yake na watoto wake apambane afanye biashara, kama aliweza kupambana at 16 alipopewa uja uzito na jamaa akamkana na dada ake hakuwa na msaada, atashindwa sasahivi? Huko dar anakotaka kukimbilia yatamkuta majuto ya zaidi ya kwanza, asijidanganye eti huyo jamaa hana mwanamke, anataka kuniamba siku zote jamaa alikuwa amekaa tu anamsubiri yeye? may be alikuwa na mapenzi ya kweli the first time lakini hii mara pili ama telling u atakuja kujuta kuliko majuto anayoyapata kwa huyu mumewe wa sasa, hakuna rangi hataiona, mwisho wa siku anaweza hata kuishia kujitoa uhai maana tayari moyo wake una mengi, na watu wa hivyo wengi huwa furaha yao inategemea kupendwa na watu wengine sasa wanapokosa ule upendo wanaoutarajia ni balaa
 
kwanza pole yake huyo dada maana ameanza kupitia mazingira magumu akiwa na umri mdogo, mi namshauri aende dar sie wanaume hua tukipenda hua hatujali sana mambo ya watoto, kwa mujibu wa stori yako huyo bwana anampenda sana rafiki yako, kuhusu watoto ni bora aondoke nao maana huyo mumewe hana mwelekeo
 
Akienda kwa huyo wa Dar atabugu mbaya. Jamaa hana mzuka naye kama wa zamani, na kaingiwa baridi zaidi alipozalishwa mtoto wa pili.

Alibugi alipobeba ujauzito wa pili, so bora avumilie tu hapo hapo kwa mzazi mwenzie.

Na wewe sijui kwanini hukumshauli rafikiyo achomoe huo ujauzito wa 2
 
Nashindwa kumlaumu, kwanza ni kutokana na umri alionao na msingi mbaya ambao ameupata tokea akiwa mdogo, alikosa upendo, akakosa uangalizi, akakosa usimamizi, akakosa ushauri akakosa role model yaani inshort amepitia mambo mengi magumu katika umri mdogo sana, yupo kwenye kundi la umama wakati bado ni binti mdogo sana, hapo kwanza anahitajii msaada wa kisaikolojia, so decision na mistake zoote ambazo amezifanya its not her fault maskini, i feel so sory for her. Nnachoweza kukwambia wewe rafiki ni hivi, mwambie asithubutu kuacha watoto wake, yeye ni victim tayari wa kukosa malezi mazuri akiwa mdogo na ni kwasababu alikosa wazazi akabakia na walezi walioharibu future yake, asirudie kosa hilo kwa watoto wake, the way umeelezea huyo baba yao alivyo akiachiwa watoto pata picha wataishi maisha gani? watakuja kuwa watoto wa aina gani? sana sana na yeye ataenda kuwabwaga kwa ndugu ajinafasi vizuri kwa bangi na pombe na wanawake wengine. Kama ndoa imemshinda, kwa huyo jamaa aanze upya maisha yake na watoto wake apambane afanye biashara, kama aliweza kupambana at 16 alipopewa uja uzito na jamaa akamkana na dada ake hakuwa na msaada, atashindwa sasahivi? Huko dar anakotaka kukimbilia yatamkuta majuto ya zaidi ya kwanza, asijidanganye eti huyo jamaa hana mwanamke, anataka kuniamba siku zote jamaa alikuwa amekaa tu anamsubiri yeye? may be alikuwa na mapenzi ya kweli the first time lakini hii mara pili ama telling u atakuja kujuta kuliko majuto anayoyapata kwa huyu mumewe wa sasa, hakuna rangi hataiona, mwisho wa siku anaweza hata kuishia kujitoa uhai maana tayari moyo wake una mengi, na watu wa hivyo wengi huwa furaha yao inategemea kupendwa na watu wengine sasa wanapokosa ule upendo wanaoutarajia ni balaa

Ushauri mzuri kabisa huu, kikubwa n malezi ya watoto asikubali maisha aliyoyaishi yeye na watoto wake wayaishi.
 
Back
Top Bottom