Ushauri wa aina ya generator

ALF

JF-Expert Member
Apr 17, 2011
207
136
Habari wanajamvi. Naombeni msaada wenu wa ushauri juu ya generator gani ni nzuri na inadumu zaidi kati ya Robi na Boss, nimekuwa nahitaji generator kwajili ya kuendeshea pump ya maji huko shambani kwangu kwakuwa hakuna umeme nilibahatika kuchimba kisima kwajiri ya kupata maji kwa shughuli za kilimo na mifugo, kutokana na gharama za uchimbaji kuwa kubwa sana nilijikuta nimeishiwa kabisa kisima kikikamilika lakini kikwazo kikabaki ni generator.

Nimejikusanya tena nikabahatika kupata 1,500,000/= kama bajeti ya kununulia generator katika zunguka zunguka yangu yangu nimepata generator aina mbili moja Robi 5.5 KV inapatikana pale mlimani city kwa 1.5milion na warant ya mwakaa mmoja. Na aina ya pili ya generator ni Boss inapatikana duka moja lipo barabara ya uhuru kama unaelekea mnazi mmoja ina 5.5KV inapatikana kwa bei hiyohiyo lakini hawana warant yoyote.

Naomba ushauri wenu ni generator gani bora zaidi na imara na inatumia mafuta kidogo zaidi kuliko nyingine?.

Natanguliza shukrani zangu.
 
Nafikiri ulitaka kuandika 5.5KW. Ni hivi ingekuwa ni mimi ningechukua iyo robi,sababu ina warrant. Hiyo ambayo haina warrant inaweza ikawa ni fake ila kama ni genuine ndio nzuri. Uchomaji wa mafuta Kwenye generator itategemea matumizi yako na kiasi cha mzigo utaobebwa na generator.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom