Ushauri kwa UKAWA, njia pekee ya kuitoa CCM madarakani

Kwa hali na tabia ya watz kubadilika haraka kama bendera. Mpaka viongozi wa dini wanaokemea mabaya ya viongozi nao wanabadilika. Miaka mitatu iliyopita Viongozi wa dini hawa hawa na watz walikuwa wanamsema vibaya mh LOWASA sasa hali imebadilika na mh lowasa anakubalika kila kona kila sehemu mpaka makanisani na misikitini...maofisini..vyuoni...bodaboda...matajiri...n.k. Niwaombe UKAWA wasisimamishe mgombea URAIS wajikite na ubunge ndio pona yetu sisi walala hoi. Urais umeshaonekana njia ni ya mh LOWASA hilo halina ubishi...angalia vyombo vya habari kama wiki vilivyotekwa na mh. Bila nape kuzuia mafuriko ya wageni sijiui ingekuwaje...Lingine kuna hiki chama cha ACT nacho kimekuja kuvuruga upinzani badala ya kutetea wanyonge sasa kinapigana vita na chadema badala ya wanaotawala.
Mwisho watz bado sana kwenye siasa CCM ITATAWALA MILELE Nchi kama kenya zambia n.k zimepiga hatu kubwa sana kwenye siasa.
Nawakilisha hoja!!
 
Wew una sema safari bado ni ndefu wakatu kwetu sisi tunaojitambua safar imeshafika mwisho! Ndege imeshatua salam tunasubir ruban afungue mlango hapo tarehe 31 october
 
Lowasa apange watu na kuwapa Rushwa mwenyewe sisi tukaogope kusimamisha mgombea? Mtanzania achague mbunge UKAWA na achague Rais CCM? unachekesha sana
 
Ndugu zangu wapenda mapinduzi kwa ushauri wa bure fanyeni hivi, Wenyekiti wote wa vyama vya upinzani warudi bungeni kwa kugombea ubunge kupitia majimbo ya uchaguzi.

Kuna ulazima wa kuimarisha nguvu bungeni.Tunaomba Lipumba, Slaa, Mbowe, Mbatia, Zitto nk warudi bungeni kama wawakilishi.
 
Nakuhakikishia kati ya wote hao hakuna hata mmoja mwenye uhakika wa kushinda jimbo
 
Katika Kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu nimeona nitoe ushauri wangu wa bure labisa bila kuwa na faida maslahi binafsi zaidi ya mustakabali mwema wa Taifa letu .

Ushauri wangu ni kuhusu mgombea wa urais kupitia UKAWA.
Litakuwa ni jambo baya na la fedhea na la kukatisha tamaa endapo CCM itarejea madarakani mwaka huu kupitia sanduku halali la kura.
Kuna kila sababu kwa UKAWA kuchukua nchi.
Tatizo ninaloliona ni UKAWA kushindwa kuafikiana kwenye kusimamisha mgombea wa nafasi ya urais.

Minong'ono mingi imesikika kutoka kwa wanazuoni mbalimbali na ndani ya CCM kuhusu ruzuku kuwa kikwazo kikubwa cha ushirika wa UKAWA kumsimamisha mgombea mmoja wa urais. Hii ni changamoto isiyo na mashiko sana kama kuna nia ya dhati ya kuleta mabadiliko. Lakini kwa viongozi wa vyama vya upinzani tuliowazoea hiki kwao ni kikwazo kinachoweza kuvunja UKAWA .
Ni lazima viongzi wa UKAWA sasa watambue kuwa watanzania wana imani na ushirika huu na wako tayari kuwapigia kura nyingi na kushinda uchaguzi ujao.
Ni vema viongozi wafahamu kuwa nje ya UKAWA hakuna chama cha upinzani kinachoweza kuiangusha CCM. Hapa na maanisha kuwa CHADEMA ijiepushe sana na siasa zake zilizojaa Ubinafsi na hila kwa kujidanganya kuwa kinaweza kushinda peke yake.

UKAWA watambue kuwa wanatakiwa kupata wabunge zaidi ya 200 na madiwani zaidi ya 4000 nchi nzima. Bila ushirika wa kweli itakua ni vigumu mno.

UKAWA watambue kuwa hata kama vyama vyao vitasimamisha kila chama mgombea wake bado CHADEMA itaongoza kwa idadi ya kura za urais. CUF itafuatia ,NCCR na NLD wataambulia kura chache za ushiriki.

Kwa hiyo ni vyema sana mgombea Urais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania akapitia CHADEMA ili nguvu kubwa iliyobaki ipelekwa Zanzibar ili kuhakikisha kuwa CUF inashinda na Maalim Seif anakua Rais wa Zanzibar.

CUFinabidi wawe wavumilivu na wakubali kuiachia chadema nafasi ya urais. Faida kubwa watakayoipata CUF ni kuwa watakua na nafasi kubwa ya kupata viti vingi sana vya ubunge visiwani na bara. Kuna uwezekano CUF ikapata zaidi ya viti vya ubunge 35 Tanganyika na madiwani wengi sana. Hivyo bado ruzuku itaongezeka maradufu wakati huo wakiwa wanaongoza serikali ya mapinduzi Zanzibar.

Mgombea urais wa chadema atakapopata urais atumie katiba na madaraka yake kuwateua Prof. Lipumba ,Makaidi na wengine kuwa Wabunge . Kitu cha kwanza kiwe ni kufyeka makada wa CCM waliojazana kwenye mikoa na wilaya kama wakuu wa wilaya na mikoa. Pia muswada upelekwe haraka bungeni ili kuweka kipengele cha kuunda serikali ya kitaifa ili kuwajumlisha wana UKAWA pamoja.

Naomba wengine waje tuendelee kutoa ushauri kwa UKAWA na mbinu za ushindi bila migogoro kabla na baada ya uchaguzi kupita.

KARIBUNI WOTE
 
Back
Top Bottom