Miaka 47 ya CCM, Shiriki Uchaguzi kwa Uadilifu na Kazi lendelee

Hamduni

Senior Member
Apr 25, 2020
155
108
HERI YA MIAKA 47 YA KUZALIWA KWA CCM

Historia inaturudisha nyuma tarehe 5 Februari, 1977 baada ya kuungana kwa Vyama vya Tanganyika African National Uniona (TANU) kilichokuwa kikitawala Tanzania Bara na Afro-Shirazi Party (ASP) kilichokuwa Chama Tawala cha Zanzibar wakati huo, Ndipo kikazaliwa CHAMA CHA MAPINDUZI.

Huu ulikuwa umoja na mshikamano mzuri kutoka kwa Waasisi wetu Mwl. Julius Nyerere (akiongoza TANU) na Aman Karume (akiongoza ASP).

Kwa miaka yote hio mpaka sasa ni miaka 47 na CCM imeendelea kuwa Imara kutokana na nguvu ya ushawishi kwa Watanzania, lakini pia Utekelezaji wa Ilani, na ahadi zake kwa Watanzania.

Chama cha Mapinduzi kimezidi kuimarika chini ya Mwenyekiti wetu Ndugu Samia Suluhu Hassan, sisi Wana CCM tunaendelea kuwa na Imani naye na tunamuunga mkono kwenye kila jitihada anazozifanya za kukijenga Chama chetu na kuwaletea Watanzania Wote Maendeleo.

Kauli Mbiu;
"Miaka 47 ya CCM, Shiriki Uchaguzi kwa Uadilifu na Kazi lendelee"

#Miaka47YaCCM
#Kazilendelee
IMG-20240205-WA0035.jpg
 
Happy birthday CCM Chama changu sijawah kupigia kura Chama kingine zaidi yako
 
HERI YA MIAKA 47 YA KUZALIWA KWA CCM

Historia inaturudisha nyuma tarehe 5 Februari, 1977 baada ya kuungana kwa Vyama vya Tanganyika African National Uniona (TANU) kilichokuwa kikitawala Tanzania Bara na Afro-Shirazi Party (ASP) kilichokuwa Chama Tawala cha Zanzibar wakati huo, Ndipo kikazaliwa CHAMA CHA MAPINDUZI.

Huu ulikuwa umoja na mshikamano mzuri kutoka kwa Waasisi wetu Mwl. Julius Nyerere (akiongoza TANU) na Aman Karume (akiongoza ASP).

Kwa miaka yote hio mpaka sasa ni miaka 47 na CCM imeendelea kuwa Imara kutokana na nguvu ya ushawishi kwa Watanzania, lakini pia Utekelezaji wa Ilani, na ahadi zake kwa Watanzania.

Chama cha Mapinduzi kimezidi kuimarika chini ya Mwenyekiti wetu Ndugu Samia Suluhu Hassan, sisi Wana CCM tunaendelea kuwa na Imani naye na tunamuunga mkono kwenye kila jitihada anazozifanya za kukijenga Chama chetu na kuwaletea Watanzania Wote Maendeleo.

Kauli Mbiu;
"Miaka 47 ya CCM, Shiriki Uchaguzi kwa Uadilifu na Kazi lendelee"

#Miaka47YaCCM
#KazilendeleeView attachment 2894816
Miaka 47 ya wakoloni weusi waliofeli vibaya katika masuala ya utawala. Kila nyanja muhimu ya maisha inashuhudia ubabaishaji wa kutupwa, huku hamasa kubwa ya watawala ikiwa ni kufanya ufisadi, wizi na hujuma kwa mali za umma.

Kutokana na utawala huu uliofeli wa CCM hii iliyochoka kifikra, hakuna mhimili hata mmoja hivi sasa hapa nchini wenye tija kwa umma wa Watanganyika, serikali yenyewe ni mzigo, bunge limejaa wababaishaji waliopata ubunge kwa njia ya wizi wa kura, mahakama ipo ipo tu, tena imejisalimisha na kujipendekeza ili kuendana na upepo na utashi wa watawala, ili kuwaridhisha na kutaka kuwafurahisha.

Wakati watawala wanajificha nyuma ya takwimu za uongo za maendeleo ya kiuchumi na kijamii ili kuonyesha maendeleo, hali halisi ya Mtanzania wa kawaida inawasuta na kuwaumbua. CCM inalaghai kwa kufanya "quantification & making comparison on statistical data" lakini haithubutu kuonyesha "quality beyond those data" Siku zote CCM imezoea kujiwekea malengo finyu sana ya kimaendeleo ambayo ni rahisi sana kuyafikia. Lakini kutokana uzwazwa wa watawala, kupitia takwimu potofu hutangaza matokeo yenye hadaa nyingi kwa mbwembwe nyingi na kisha kuanza kushangilia kuwa wamevuka malengo, na kumsifu kinafiki Kiranja wao mkuu kwa utekelezaji wa ilani.

Ndiyo! Miaka 47 imepita. Lakini vipi kuhusu uhakika na upatikanaji wa huduma bora za kijamii!? Hadaa nyingi inafanyika kupitia itolewaji wa takwimu za uongo, lakini vipi kuhusu ubora wa huduma hizo zinazotolewa na serikali katika sekta mbalimbali!? Kuna cha kujivunia kuhusu elimu, huduma za afya, umeme, maji safi, waste management, police services, mahakama, n.k.

Ni vyema chama hiki kikajitathimini kama kinastahili kuendelea kudhamiria kuiba kura na kuzidi kubaka demokrasia ili kuzidi kung'ang"ania kubakia madarakani kwa nguvu. Kwa tathimini yangu binafsi, hii miaka 47 ya toka kuzaliwa kwa CCM, hili ni kama tu genge la wadangaji na mateja waliokubuhu na kushindikana, ambao wapo ndani ya nyumba ya ibada yao, wakiwa wamelewa na huku wakisifu na kuabudu na kumshukuru mungu wao kwa ajili ya matendo makuu anayowatendea kwa kila siku iitwayo leo..
 
Back
Top Bottom