Ushauri kwa UKAWA, njia pekee ya kuitoa CCM madarakani

hii chati yako hairepresent jamii ya kitanzania labda ya kikaskazini. siwezi kuipa kura hii chati yako maisha na milele. kwa kifupi kama hakuna society representation msahau kushinda.


Chadema ilishinda uraisi ccm wakachakachua sasa 2015 kura za chadema + kura za nccr + kura za cafu=Usindi wa 80%. Maisha ccm ata wachakachue vipi hawataweza ukawa ndio habari ya mjini.
CHATI YA 2015
1. Slaa Rais
2. Lipumba Waziri wa fedha.
3. Maalim sefu- rais znz.
4. Mbowe waziri mkuu
5. Mbatia Makamu wa Rais

WENGINE JAZIA
 
Mimi naomba kwanza wapiganie sheria za vyama vya siasa nchini ambayo ikibadilishwa itaruhusu muunganiko wa chama zaidi ya kimoja..mfano tukisema UKAWA kisheria sio registered political party.

Katiba ya sasa inasema mgombea wa uraisi lazima atoke kwenye chama chq siasa kilichosajiliwa..sasa tukisema asimamishwe mgombea wa uraisi mmoja then atakuwa anatoka chama gani??.na vipi kuhusu kuwaelimisha wananchi kuhusu muunganiko huo..kumbuka kuna wafuasi wengine wa CDM hawapendi CUF na pia wa NCCR halikadhalika.

Wapiganie mabadiliko ya sheria kama walivyofanya kenya na kuunda union kama vile JUBELEE na CORD..hii itasaidia sana kuongeza nguvu kwenye kampeni japokuwa union hizi huwa zinaleta shida sana kwenye mgawanyo wa madaraka hususan yule ambaye ni rais kupendelea watu wa chama chake kama upande wa RUTTO wanavyolalamika..na hapa itasaidia sana kwenye UNION maana hakuna chama kitakachokufa ila ni muungano pekee na vyama vitaendelea kuwepo
 
Napenda kuwapa ushauri wa bure nyie viongozi wa ukawa la sivyo mtapigwa goli la kisigino.

Kwa kuwa tayari kanuni za bunge la katiba zimebadilishwa ili kuruhusu wajumbe walioko nje ya ukumbi (ndani au nje ya nchi) kuna uwezekano baadhi ya wajumbe wakarubuniwa kwa njia yoyote ile.

Sasa nawashauri kama mnaweza itisheni mkutano wa wajumbe wote wa ukawa na wale wanaowaunga ikiwemo kundi la 201 mkutane ama dar es salaam au kokote kule mpige kura zenu za wazi mbele ya wanasheria kuwa mnaikataa rasimu iliyopendekezwa ili kutotoa mwanya wa uchakachuaji ambao unaweza kufanyika.

Kura hizo baada ya kupigwa zitume kwa fax kama ambavyo bunge limeamua. Mkisubiri mtapigwa goti la kisigino. Kuna wajumbe wenzenu wanaweza kurubuniwa wapige kwa siri.

Najua hamkushiriki kujadili ila hatari iliyopo ni kutumia kigezo cha wanaukawa kupata theluthi mbili ya zanzibar.

Hasa ikizingatiwa watu wanaweza kununuliwa.

Ni ushauri tu lakini.
 
Kama kweli Ukawa/Chadema wana nia dhati kuchochea hasira za wananchi dhidi ya chama tawala na serikali yake wanahitaji wajipange kisayansi zaidi! Ni kweli swala la maandamano linasaidia kiasi fulani kuibua "public awareness" lakini linabakia kwa kundi/tabaka fulani tu la wananchi!

Wafanye analysis ya kiasi cha fedha kilichotumika na Tume ya Warioba mpaka walipoikabidhi Rasimu kwa Bunge Maalum la Katiba kwamba kingalitosha kufanya miradi gani ya maendeleo/kutoa huduma gani za kijamii/kulipa mishahara na marupurupu ya walimu wangapi, wa daraja gani, na kwa muda gani nk. Baada ya hapo wafanye analysis ya kiasi cha fedha kilichotumika na BMK kuandaa "Kanuni" kwamba zingetosha kufanya nini kwa mambo niliyoyataja hapo juu! Kisha wafanye analysis ya kiasi cha fedha kilichotumika na BMK tangu lilipoanza rasmi mijadala mpaka "Kanuni" zilipovurugwa mno na wao kuamua kutoka, kwamba zingetosha kufanya nini! Mwisho wafanye analysis ya kiasi cha fedha kilichokwisha kutumika na BMK tangu wao wasusie mpka sasa kwamba zingetosha kufanya nini!
Kisha waitishe "Press Conference" kubwa wawasilishe analysis hiyo, pia wahakikishe inafikia Taasisi zote za Elimu ya Juu ili kuibua mijadala, vyama vya wafanyakazi, vikundi vya wanaharakati nk.

Baada ya hapo waweke strategies za maandamano ili kwa pale maandamano yatakapofanyika analysis iwe imefanyika kwamba kwa eneo husika ni nini kingaliweza kufanyika kwa kiasi hicho cha fedha.

Kama mpaka hapo hasira ya wananchi dhidi ya dhuluma hii haitatosha kuwatoa madarakani chama tawala na serikali yao basi nawashauri waachane na siasa wakafundishe wananchi elimu ya uraia kwanza!
 
Nipashe walifanya analysis ya namna hiyo na kuifanya kuwa habari yao kubwa katika Gazeti lao la Septemba 15, 2014 chini ya kichwa, "BUNGE LA KATIBA HASARA: Mabilioni yake yangetosha kujenga zahanati 600: Noti zikipangwa barabarani ni Dar hadi Bukoba." Habari hiyo imewasababishia Nipashe kuandikiwa barua na Msajili wa Magazeti, Kumb Na. FB 77/319/01/80 ya tarehe 16 Septemba 2014 inayowataka wajieleze kuhusu "habari hiyo ya uchochezi" !!!! Hiyo ndiyo CCM bhana!!!!! Ni yaleyale ya maandamano !!!!!!!
 
Asante mkuu gumegume kwa update hiyo juu ya yaliyowapata Nipashe! Ila naamini UKAWA/CHADEMA wakilifanyia kazi vizuri hilo swala na kuwa na vielelezo muhimu CCM watapaswa kuishia kupumulia mashine kwani kwa huo mziki hawatapata pa kupumulia!
 
Ungekuwa karbu ningekununulia soda.
Thanx very much. You are a great thinker.

Please katika mkutano hakikishen utaratibu wa kuapishwa wajumbe wa ukawa na upigaji kura ya waz unarekodiwa na kuambatanishwa wakati wa utumaji hizo kura.
VIONGOZ WA UKAWA CHUKUEN HATUA HARAKA.
 
Kwanza niwapongeze ukawa kwa hatua nzuri waliyofikia ya kuungana na kuwa wamoja. Nimefarijika na hatua hii kwani ni wakati muafaka wa kuanza kuwashughulikia mafisadi wote..
Ninachowaomba Ukawa ni kwamba wanapofanya mikutano kuelezea watu kupigia kura ya hapana katiba pendekezwa ya mafisadi wawaelezee watu ni vipengere gani vimetolewa na vilikua na umuhimu gani..wasiishie kusema ikataeni tu watu wengine ni wagumu kuelewa kwani watasema wanapelekeshwa..ccm wao wanapita na kuwaeleza watu kua katiba pendekezwa imewajar wakulima, wafugaji na kila idara hivyo ukienda mwingine kuwashawishi wanakushangaa..plz jitahidini kufanya hivyo il watu wajue katiba na maoni yao yamechakachuliwa vip..
 
Moderators Tafadhali Sana hii thread msiunganishe na zingine.

Kutokana na uchaguzi wa serikali za mitaa kugubikwa na kasoro kibao. Ushauri wangu kwa vyama pinzani vinavyoshiriki uchaguzi huu unaotarajia kufanyika December 14, 2014 visishiriki huu uchaguzi. kwani ushiriki wao katika uchaguzi huu uliojaa wimbi la ujanjaujanja, mwisho wa siku watakuja na lawama kibao.

Kwa nini nimeshauri kihivyo. Huu uchaguzi Kama nilivyokwisha chunguza toka harakati zianze, umegubikwa na maajabu au kasoro nyingi tu na za msingi. Mojawapo ya kasoro hizo ni Kama zifuatazo hapa chini.

1. Ucheleweshwaji wa mwongozo au sheria kwa washiriki. Hapa namaanisha washiriki kwa maana ya vyama na wagombea. Kwa taarifa rasmi ni kwamba mwongozo kwa wagombea umechelewa kufika kwa wagombea jambo lililopelekea wagombea wengi kukosea katika ujazaji wa fomu na kusababisha wagombea wengi kuwekewa mapingamizi.

2. Zoezi kusimamiwa na Tamisemi chini ya ofisi ya waziri mkuu. Makubaliano ya vyama shiriki pamoja na serikali ni kwamba uchaguzi huu ulipashwa kusimamiwa na Tume ya uchaguzi Tanzania.

3. KUkosekana kwa Elimu ya uraia juu ya umhimu wa zoezi hili. Hapa kijijini kwetu hatujawahi kuona hata kusikia kwenye vyombo vya habari uhamasishaji wowote buy ya huu uchaguzi.

4. Muda mfupi wa uhandikishaji wa daftari la mpiga kura. Kipindi cha uhandikishaji majina ya wapiga kura wa wiki moja iliyotimika hakika ni muda mfupi Sana na umepelekea watu wengi kutojihandikisha.

5. Ukiukwaji wa sheria ya mapingamizi. Sheria inatamka kuwa pingamizi zote zianzie ngazi ya chini kwa msimamizi wa uchaguzi na pingamizi lifanywe na mgombea usika. Jambo hili limekiukwa katika baadhi ya maeneo unakuta pingamizi linatolewa na viongozi wa vyama wa juu tena kwa kuanzia wilayani au mkoani.

6. Chama tawala kutumia njia au mbinu chafu katika kuwawekea mapingamizi wagombea wa vyama pinzani. Unakuta msimamizi wa uchaguzi anaambiwa na Marisa usalama kuwa tu atumie namna yeyote ile mgombea pinzani anayekubalika jina lake lisitoke Kati ya wale watakaoingia kinyang'anyironi siku ya kupigiwa kura.

7. Chama tawala kupanga kivuruga na hata kuiba kura. Hii ni mini inayotumikaga siku zote kwa chama tawala kujipatia ushindi na hii ndiyo kete yao ya mwisho kushinda.


Naishia hapa na Kama kuna mengine utaongezea utapo changia.


Baada ya uchaguzi endapo ushauri huu utapuuzwa basi turidi hapa kwa mjadala na ushauri zaidi.
 
Mimi ni mwana CCM ila naomba nitoe ushauri ufuatao kwa UKAWA ;
Katika uchaguzi wa serikali za mitaa imeonekana wamejitaidi kushinda kwa kiwango kikubwa kuringanisha na miaka iliyopita kwaiyo wanapaswa wafanye yafuatayo ili kuweza kuendeleza ushindi katika uchaguzi mkuu 2015
1.kuonesha mabadiliko ya kimaendeleo katika sehemu usika,nikimanisha waweze kuboresha pale ambapo chama changu cha CCM walishindwa kufikia.

2.Kuwajengea imani watanzania kuwa wanaweza ata wakipewa nchi ili waiongoze hawatatuangusha.

3.Kutopokea rushwa au kutoa rushwa, nmekuwa nikishudia wenyekiti wa mitaa wakipokea kitu kidogo ili waweze kutekeleza wajibu wao.
4.Wasiongoze kwa kutumia uchama ,wanapaswa wajue kuwa wanaongoza watanzania siyo UKAWA.
KWAKUFANYA HAYO WANAWEZA KULETA UPINZANI MKUBWA KWA CCM MWAKA 2015.
 
Back
Top Bottom