Mcheza Karate
JF-Expert Member
- Jun 30, 2011
- 690
- 350
Wana Jf,
hakuna mtu ambaye hakusikia, kuona au kusoma matamko ya wanahabari wa baadhi ya mikoa kuwa hawatoripoti habari za jeshi la polisi.
Wanahabari wa mikoa ya Iringa na Ruvuma walijitamka mapema kabisa kuwa jeshi la polisi lisahau kuona habari zao kwenye vyombo vya habari
Walikusudia kufanya hivyo ili kushinikiza haki itendeke juu ya hatua za kisheria za kuchukuliwa juu ya polisi waliomuua mwanahabari wa kituo cha luninga cha Channel ten marehemu DAUD MWANGOSI.
kilichonishtua na kunishangaza na tena kuamsha ghadhabu zangu ni juu ya wanahabari wa IPP kuendelea "kuwapa promo polisi".
"waziri ambaye tutajutia akijiuzulu" bwana "dk." JOHN NCHIMBI wakati akifungua wiki ya nenda kwa usalama kwa niaba ya "mpiga misele", mkuu wa kaya, wanahabari wa ITV na radio one wakaripoti habari hiyo. Tena na wakamhoji mnadhimu wa polisi usalama barabarani mkoa wa Iringa.
Haa! Si ndo hawa ITV na radio one ndo walimsogeza pembeni "waziri tunayempenda" na kuanza kumuhoji ujumbe aliokuja nao pale jangwani. Sasa walimfukuza kwa lipi wakati wanapenda kusikiliza ujumbe wake?
ANGALIZO KWA WANAHABARI: CCM ni dola inayoelekea kuanguka msiogope vitisho na msipokee zawadi wala mlungula..
Kwani dola yoyote inapotaka kuanguka hutumia mabavu, vitisho, rushwa, uongo na hadaa. Kama tunavyoona CCM wanafanya. Kwani ndo dalili ya dola inayoanguka.
Tunajua mmiliki wa IPP ni kadi mwaminifu wa CCM au anawalazimisha kuwasaliti wanahabari wenzenu, mnasaka u DC kama NORVATUS MAKUNGA, BETTY MKWASA mliokuwa nao hapo mnapiga nao mzigo? Mna lipi lenu moyoni?
Mungu ibariki afrika,
mungu bariki Tanzania,
mungu bariki wanamapinduzi
Nawasisha!