Wafanyakazi wa Sahara media waendelea kulia, wadai mabilioni ya fedha kwa malimbikizo ya stahiki zao

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,016
9,885
Chama cha Wafanyakazi wa Vyombo vya Habari Tanzania (JOWUTA) kimesajiliwa rasmi tarehe 26 Machi, 2018. JOWUTA imesajiliwa na Msajili wa Vyama vya Wafanyakazi na Waajiri chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu chini ya kifungu cha 48 (5) cha Sheria ya Ajira na Mahusiano sehemu za kazi ya mwaka 2004 na kupewa cheti cha usajili namba 035.

Chama hiki kinaundwa na wanahabari na wafanyakazi wengine katika vyombo vya habari kutoka mikoa yote Tanzania bara ambapo jukumu lake kubwa ni kutetea na kulinda maslahi ya wafanyakazi sehemu zao za kazi, kwa kuzingatia Sheria Namba 6 ya Mwaka 2004 sura ya 366 na Kanuni zake.

JOWUTA imekuwa ikipokea malalamiko kutoka kwa wanachama wake kuhusu maslahi yao na haki zao katika vyombo vya habari nchini ikiwepo kutolipwa mishahara, kutopewa mikataba licha ya kufanyakazi kwa muda mrefu, na kutopata stahiki nyingine kama walivyo wafanyakazi wa sekta nyingine. Pia, kumekuwepo na changamoto ya wafanyakazi kufukuzwa au kusimamishwa kazi bila kufuata sheria na taratibu zilizopo nchini.

Aprili 7, 2023, viongozi wa JOWUTA walifanya ziara ya kikazi mkoani Mwanza, kuzungumza na wafanyakazi wa Sahara Media ambao wanafanyakazi Radio Free Afrika (RFA), Kiss FM, na Star TV, ambao wamekuwa na madai ya kutolipwa mishahara na stahiki zao zaidi ya shilingi bilioni 2.5. Madai haya tayari yamesajiliwa Idara ya Kazi Mkoa wa Mwanza hadi kufikia mwaka 2022 na sasa madeni yameongezeka.

Idara ya Kazi mkoa Mwanza tayari ilikamilisha mchakato wake wa kufikishwa Mahakamani suala hilo tangu mwezi Aprili mwaka huu kwa kukabidhi nyaraka muhimu Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka Kanda ya Ziwa iliyopo mkoani Mwanza. Hata hivyo, suala hilo bado halijafikishwa mahakamani na hivyo kuendelea kuathiri haki za wafanyakazi.

Viongozi wa JOWUTA wamefanya jitihada kubwa ikiwemo kuonana na Viongozi wa Wizara ya Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu na Kamishna wa Kazi nchini ili suala hilo kifikishwe katika vyombo vya sheria, lakini bado hatua hazijachukuliwa.

Hivyo, JOWUTA inaiomba Serikali kulifikisha Mahakamani suala hili kwani majadiliano nje ya Mahakama na mwajiri yamekwama, na kibaya zaidi wafanyakazi ambao wamekuwa wakilalamikia maslahi yao wameendelea kuondolewa kazini bila kulipwa stahiki zao, na wengine kuendelea kutaabika kwa kukosa stahiki zao.

JOWUTA ina imani kubwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kuwa anaweza kuagiza suala hili kushughulikiwa na Wizara husika ili haki za Wafanyakazi wa Sahara Media na vyombo vingine vya habari nchini ziheshimiwe na waajiri.

Pia, JOWUTA inaomba kukutana na Kamati Maalum iliyoundwa na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mheshimiwa Nape Nnauye. Kamati hii ilimaliza kazi yake mwezi Mei 2023, lakini bado haijakutana na JOWUTA, chama chenye haki kisheria kutetea maslahi ya wafanyakazi, hivyo wanataka kuwasilisha maoni yao juu ya maslahi ya wanahabari nchini.

JOWUTA inasisitiza kuwa uchumi wa vyombo vya habari ni lazima uendane na maslahi bora kwa wafanyakazi katika vyombo vya habari nchini.
 
Dunia inachekesha kweliii......watetezi wa jamii wanashindwa kujitetea, wanaripoti habari za wenzao,za kwako wanashindwa kujitetea.....Bora ualimu kuliko kuwa mwanahabari,......pumbavuuu
 
Back
Top Bottom