Usaliti wa IPP kwa wanahabari; Unachukuliaje?

Mcheza Karate

JF-Expert Member
Jun 30, 2011
690
350
Wana Jf,
hakuna mtu ambaye hakusikia, kuona au kusoma matamko ya wanahabari wa baadhi ya mikoa kuwa hawatoripoti habari za jeshi la polisi.

Wanahabari wa mikoa ya Iringa na Ruvuma walijitamka mapema kabisa kuwa jeshi la polisi lisahau kuona habari zao kwenye vyombo vya habari

Walikusudia kufanya hivyo ili kushinikiza haki itendeke juu ya hatua za kisheria za kuchukuliwa juu ya polisi waliomuua mwanahabari wa kituo cha luninga cha Channel ten marehemu DAUD MWANGOSI.

kilichonishtua na kunishangaza na tena kuamsha ghadhabu zangu ni juu ya wanahabari wa IPP kuendelea "kuwapa promo polisi".

"waziri ambaye tutajutia akijiuzulu" bwana "dk." JOHN NCHIMBI wakati akifungua wiki ya nenda kwa usalama kwa niaba ya "mpiga misele", mkuu wa kaya, wanahabari wa ITV na radio one wakaripoti habari hiyo. Tena na wakamhoji mnadhimu wa polisi usalama barabarani mkoa wa Iringa.

Haa! Si ndo hawa ITV na radio one ndo walimsogeza pembeni "waziri tunayempenda" na kuanza kumuhoji ujumbe aliokuja nao pale jangwani. Sasa walimfukuza kwa lipi wakati wanapenda kusikiliza ujumbe wake?

ANGALIZO KWA WANAHABARI: CCM ni dola inayoelekea kuanguka msiogope vitisho na msipokee zawadi wala mlungula..

Kwani dola yoyote inapotaka kuanguka hutumia mabavu, vitisho, rushwa, uongo na hadaa. Kama tunavyoona CCM wanafanya. Kwani ndo dalili ya dola inayoanguka.

Tunajua mmiliki wa IPP ni kadi mwaminifu wa CCM au anawalazimisha kuwasaliti wanahabari wenzenu, mnasaka u DC kama NORVATUS MAKUNGA, BETTY MKWASA mliokuwa nao hapo mnapiga nao mzigo? Mna lipi lenu moyoni?

Mungu ibariki afrika,

mungu bariki Tanzania,

mungu bariki wanamapinduzi

Nawasisha!
 
Mmiliki wa hivyo vyombo vya habari anatakiwa awepo kwenye new list of shame
 
Je bilionea na mmiliki wa vyombo vya habari vya IPP (siwezi kumtaja jina...kutajwa jina ni haram humu JF) alitoa mchango wa kiasi kwenye msiba wa Mwangosi?

hii thread nashangaa mpaka sasa ipo hapa haijafutwa au kuhamishwa...strange!
 
mnasahau kuwa sophia simba aliposema mengi hana kadi ya ccm,mengi akionyesha kadi yake ya ccm kwenye vyombo vya habari na alikjiunga na chama tokea mwaka 1977...gamba damu hilo
 
Hii thread ikiendelea kuwepo hapa kwenye jukwaa la siasa mpaka Ijumaa naomba nipewe ban ya 24 hrs.

Je bilionea na mmiliki wa vyombo vya habari vya IPP (siwezi kumtaja jina) alitoa mchango wa kiasi kwenye msiba wa Mwangosi?

ha! ha! ha! ha! ha! ha! ha! ha!
 
Jamani huyo ni tajiri na alishaambiwa akitaka biashara zake ziende vizuri ni lazima awe CCM, tatizo lenu ninyi mnafikiri kila tajiri ni kama Sabodo, ndugu yangu inategemea utajiri wako umeupata vipi ili uwe pro au against the state!
 
Jamani,kila mtu ana uhuru wa kujiunga na chama chochote cha siasa kama vile ilivyo kwenye suala la imani.
Au wewe unaechukia Mengi kuwa ccm ulitaka awe chama gani?
kama wote wangekuwa ni wanachama wa chama unachopenda wewe (japo sina uhakika kama hata kura unapiga) unafikiri demokrasia ingekuwepo?
Kwani Mengi kuwa CCM amekuwa biased ktk kutangaza habari?
 
mh! Maoni yako ndugu. Lakini ndo utumie chombo chako cha habari kwa maslahi binafsi?
 
Sasa mmiliki anahusika vp hapa? yeye ndo head of news kwani? acheni kuropoka na kubwatuka msio yajua!
 
Susieni na vyombo vya habari vya IPP itakua mzuka Tanzania daima kama chombo pekee cha habari kinatosha.
 
ndomana waandishi wa tz hamuheshimiki, mnapoteza muda kufanya mambo msoyaweza na yasiyokuwa na tija kwenye jamii.

Hamuyawezi kwakuwa nyie ni waajiriwa, mwenye uwamuzi wa mwisho muandike nn au msiandike nini ni mmiliki na sio nyie kwahiyo hamuwezi kukiuka hilo unless mmeacha kazi.

Na hatakama mngeweza kufanya hivyo, hakuna manufaa yozote kwa mtanzania wa kawaida, mnamnyima haki yake ya kupata habari.

Jambo la busara ni kuendelea kuwaandika polisi zaidi hasa wanapo kosea ili wajirekebishe.
Mnapoacha kuwaandika mnawapa nafasi zaidi ya kutenda madudu.
 
Nyie mnalaumu ITV bure, hao chanel 10 ambao mwenzao aliuwawa, wiki iliyopita walikuwa wanamhoja kamanda mpinga juu ya wiki ya nenda kwa usalama, je wengine watafanya nini? Tatizo hao waandishi wa habari wenyewe hawana msimamo wanafanya wasichoamini.
 
Wana Jf,
hakuna mtu ambaye hakusikia, kuona au kusoma matamko ya wanahabari wa baadhi ya mikoa kuwa hawatoripoti habari za jeshi la polisi.

Wanahabari wa mikoa ya Iringa na Ruvuma walijitamka mapema kabisa kuwa jeshi la polisi lisahau kuona habari zao kwenye vyombo vya habari

Walikusudia kufanya hivyo ili kushinikiza haki itendeke juu ya hatua za kisheria za kuchukuliwa juu ya polisi waliomuua mwanahabari wa kituo cha luninga cha Channel ten marehemu DAUD MWANGOSI.

kilichonishtua na kunishangaza na tena kuamsha ghadhabu zangu ni juu ya wanahabari wa IPP kuendelea "kuwapa promo polisi".

"waziri ambaye tutajutia akijiuzulu" bwana "dk." JOHN NCHIMBI wakati akifungua wiki ya nenda kwa usalama kwa niaba ya "mpiga misele", mkuu wa kaya, wanahabari wa ITV na radio one wakaripoti habari hiyo. Tena na wakamhoji mnadhimu wa polisi usalama barabarani mkoa wa Iringa.

Haa! Si ndo hawa ITV na radio one ndo walimsogeza pembeni "waziri tunayempenda" na kuanza kumuhoji ujumbe aliokuja nao pale jangwani. Sasa walimfukuza kwa lipi wakati wanapenda kusikiliza ujumbe wake?

ANGALIZO KWA WANAHABARI: CCM ni dola inayoelekea kuanguka msiogope vitisho na msipokee zawadi wala mlungula..

Kwani dola yoyote inapotaka kuanguka hutumia mabavu, vitisho, rushwa, uongo na hadaa. Kama tunavyoona CCM wanafanya. Kwani ndo dalili ya dola inayoanguka.

Tunajua mmiliki wa IPP ni kadi mwaminifu wa CCM au anawalazimisha kuwasaliti wanahabari wenzenu, mnasaka u DC kama NORVATUS MAKUNGA, BETTY MKWASA mliokuwa nao hapo mnapiga nao mzigo? Mna lipi lenu moyoni?

Mungu ibariki afrika,

mungu bariki Tanzania,

mungu bariki wanamapinduzi

Nawasisha!

IPP haipo kisiasa ,bali kikazi zaidi.
 
Sasa mmiliki anahusika vp hapa? yeye ndo head of news kwani? acheni kuropoka na kubwatuka msio yajua!
Wewe ndio hujui, tanzania wenye vyombo vya habari ndio wahariri wakuu hata kama hawana taaluma hizo, ndio wanaoamua nini kisemwe nini kisisemwe na nini kifanyike kwenye vyombo vyao vya habari. nadhani hujui pia maana ya kubwatuka na kuropoka.
 
Back
Top Bottom