Vyombo vya habari vinavyo milikiwa na watu binafsi viangaliwe kwa makini

DaudiAiko

JF-Expert Member
Dec 2, 2012
302
274
Wanabodi,

Kwanza kabisa napenda kutoa shukrani za dhati kwa wale wote walio husika katika kuhakikisha kwamba vyombo vya habari vinachukua nafasi kubwa katika suala zima la kuwa elimisha wananchi kuhusu masuala mengi tofauti tofauti. Serikali ya Tanzania inajivunia kwa ongezeko kubwa la vyombo vya habari ndani ya muda mfupi. Lakini je ongezeko hili lina ashiria kwamba vyombo hivi viko huru na ni huduma isiyo tetereka kwa wananchi?. Mada hii inahusu tasnia ya habari na umiliki wa vyombo vya habari na kama haya yanachangia habari zinazo wafikia wananchi au maoni ya wananchi kuhusu serikali yao.

Tasnia ya habari siku zote, ni tasnia ya hadhi. Wana habari wanatakiwa kuwa watu wenye upeo mkubwa wa changanua masuala mbalimbali kwenye jamii kwa weledi wa hali ya juu. Hali iliyopo nchini Tanzania, ni vyombo vya habari kutupilia mbali uwezo na ufanisi huu katika kupendelea wanahabari wenye sauti nzuri ya utangazaji au uandishi mzuri.

Kathalika, ni vyema kufahamu athari ya vyombo vya habari kumilikiwa na mtu mmoja au mtu anayeweza kushawishiwa na watu wengine kuchapisha habari au kuchochea mwenendo wowote nchini. Gazeti la Mwananchi linalosomwa na watanzania walio wengi lina milikiwa na Nation media group ya Kenya. Nation Media group siyo kampuni binafsi, bali ina milikiwa na watu 7500 kwenye soko la hisa la Nairobi.

Shirika la IPP media ambalo lilikuwa lina milikiwa na marehemu Reginald Mengi, lina miliki magazeti ya Nipashe, Alasiri, The Guardian, Komesha, Kasheshe, Lete raha, Sunday observer, financial times na this day. ITV, EATV, Radio one na East Afrika FM navyo vipo chini ya IPP media.

Serikali haitakiwi kumiliki chombo chochote cha habari, mtu binafsi anaweza asiwe na malengo ya kudumisha demokrasia na kwasababu hiyo anaweza kurubuniwa. Kikatiba, idadi ya wamiliki wa vyombo vya habari inatakiwa kujulikana. Wamiliki haya hawatakiwi kuwa na controlling stake kwenye chombo chochote za habari au kama watakuwa na controlling stake, katiba inatakiwa kuwabana wasiwe na maamuzi yoyote kwenye kazi zinazofanywa na wanahabari. Soko la hisa, ni njia nyingine inayoweza kutatua changamoto hii

Haya ni maoni yangu, ningependa kusikia kutoka kwako...
 
Ya kwamba Azam media inamilikiwa na mtu/watu wanaoweza kurubuniwa na kwenda kinyume na misingi ya taifa letu?!!
 
Anzisha chombo chako halafu kila siku tangaza kilimo kwanza.

Uone kama utapata wateja wa kulipia mishahara ya watangazaji.
 
Back
Top Bottom