Aliyesababisha Radio One na ITV kuanguka kutoka kilele cha tasnia ni nani?

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,634
46,278
Kwa ujumla IPP Media katika ubora wa wake enzi za kabla ya mwaka 2016 ilikuwa ni kampuni ya kiwango cha juu kabisa katika tasnia ya habari katika ukanda huu wa Africa Mashariki kwa weledi na umahiri.

Vituo vyake vya Radio one, ITV, East Africa pamoja na magezeti yalikuwa ya weledi wa hali ya juu. Ulikuwa unapata habari ambazo unaona kweli zimefanyiwa kazi na waandishi halisi wa habari, pia katika burudani walikuwa wanafanya vizuri sana.

Waliweza ku-balance utoaji wa habari ngumu, elimu na burudani kwa weledi wa hali ya juu na kuvutia.

Tangu 2016 ni kama IPP ilipotea kabisa katika tasnia na kuliacha taifa katika ombwe kubwa la kukosa chombo cha habari kinachowasilisha maslahi mapana ya kitaifa ambacho kinawafikia watu wengi.

Kwa sasa katika taifa letu vyombo karibia vyote vinavyowafikia raia wengi ni kama vya comedy na burudani zaidi. Kuanguka kwa ITV na Radio One ni moja tukio baya zaidi katika historia ya nchi yetu.
 
Kwa ujumla IPP Media katika ubora wa wake enzi za kabla ya mwaka 2016 ilikuwa ni kampuni ya kiwango cha juu kabisa katika tasnia ya habari katika ukanda huu wa Africa Mashariki kwa weledi na umahiri...
Management ilichukulia poa mageuzi ya tekinolojia na uendeshaji, media kiujanjajanja, hakuna mafunzo kwa wafanyakazi mishahara kiduchu.

Kifupi swala la tekinolojia sio la kulichukulia kimzaa mzaa na sasa kiama kinakuja kwa ambao hawata chukulia serious mabadiliko mapya ya tekinolojia ya AI watapotea vibaya mno..
 
Kwa ujumla IPP Media katika ubora wa wake enzi za kabla ya mwaka 2016 ilikuwa ni kampuni ya kiwango cha juu kabisa katika tasnia ya habari katika ukanda huu wa Africa Mashariki kwa weledi na umahiri.

Vituo vyake vya Radio one, ITV, East Africa pamoja na magezeti yalikuwa ya weledi wa hali ya juu. Ulikuwa unapata habari ambazo unaona kweli zimefanyiwa kazi na waandishi halisi wa habari, pia katika burudani walikuwa wanafanya vizuri sana.

Waliweza ku-balance utoaji wa habari ngumu, elimu na burudani kwa weledi wa hali ya juu na kuvutia.

Tangu 2016 ni kama IPP ilipotea kabisa katika tasnia na kuliacha taifa katika ombwe kubwa la kukosa chombo cha habari kinachowasilisha maslahi mapana ya kitaifa ambacho kinawafikia watu wengi.

Kwa sasa katika taifa letu vyombo karibia vyote vinavyowafikia raia wengi ni kama vya comedy na burudani zaidi. Kuanguka kwa ITV na Radio One ni moja tukio baya zaidi katika historia ya nchi yetu.
Waliungana na Yule mtu, yule Mtu Mbaya
 
Ubahili na kutokuwa proactive kumewafanya waendelee kuporomoka. Wanashindwa kujipanua tangu afariki Mengi wamebaki vilevile. Kuna mikoa redio za IPP hazipo kabisa wanazidiwa na Sahara Media ambayo imesambaa nchi nzima.
 
Back
Top Bottom