Usafiri wa Dar-Mwanza ukoje?

Tiger

JF-Expert Member
Nov 30, 2007
1,747
386
Wana jf,
Naomba mchango wa mawazo.
Ninatarajia kusafiri mwezi wa 12 kutoka Dar kwenda Mwanza(sijaenda miaka mingi sana).
Kuna mtu mmoja mwenyeji wa Mwanza(hajaenda siku nyingi kidogo) anasema wakati wa mvua safari za kutoka Dar kwenda Mwanza huwa zinasumbua kwakuwa barabara ni mbovu na train hujaa sana tena mapema, lakini jana kuna mtu mwingine aliniambia kuwa sehemu kubwa kwa sasa kuna lami hivyo bara bara si tabu tena na huenda mpaka miezi hiyo kutakuwa na lami toka Dar mpaka Mwanza.

Nombeni mchango wenu kwa wale mnaofahamu.
Asnteni.
 
Chukua PrecisionAir. Ingawa wanatumia ndege za pangaboi zinazochukua takribani saa tatu kufika mwanza, lakini utakuwa na uhakika wa safari kuliko kutumia kusafiri wa ardhi kipindi hicho krismasi. Boeing huchukua dakika 45 tu lakini sina uhakika kama bado tuna huduma ya namna hiyo tena.
 
mkuu, kila mtu hujikuna mkono unapofikia,na isitoshe kipindi huyu jamaa anataka kwenda huwa ni peak season bei inakuwa juu vile vile....kama kuna anayefahamu barabara zimefikia wapi kwa matengenezo atujulishe tafadhali
 
Barabara kwa wastani imemalizika kwa asilimia 95. Ni kipande kidogo tu kutoka Manyoni unapoelekea Singida, kama kms 16 hivi ambacho hakina lami lakini kipo katika matengenezo ya kumalizia. Kwa hiyo kama uwezo ni mdogo namshauru achukua basi tu na atalala siku hiyo hiyo Mwanza. Kuna mabasi mengi sana ya kwenda Mwanza.

Precision wana Boeing na inachukua saa 1 dk 20 mpaka Mwanza. Ila hawatumii Boeing sana kwa route hiyo ndio maana juzi watu waligandishwa Airport za Dar/Mwanza wakisubiri itoke Nairobi kwa routine maintenance.
 
Nawashukuru nyote mliochangia.
Nadhani jibu limetolewa vizuri na waliotaka kufahamu kama mimi, wameshafahamu.
Asanteni sana Kichuguu, Preta na Chief.
 
Chukua PrecisionAir. Ingawa wanatumia ndege za pangaboi zinazochukua takribani saa tatu kufika mwanza, lakini utakuwa na uhakika wa safari kuliko kutumia kusafiri wa ardhi kipindi hicho krismasi. Boeing huchukua dakika 45 tu lakini sina uhakika kama bado tuna huduma ya namna hiyo tena.

hiyo ya pangaboi (Dash 8), inachukua masaa mawili tu mpka mwanza na safari ni saa moja asubuhi, kwa hiyo by saa tatu unakuwa upo mwanza, hiyo boeng hipo siku mojamoja tu especially kama kuna abiria wengi wa kwenda Nairobi au Uganda
 
ATR 42 or ATR 72
 
Kama unataka kustudy vizuri na kujionea maendeleo na mapungufu ya kipindi cha miaka yote hiyo tumia basi. Kuna ba si muhamed Trans na mabasi mengine.
Kuna siku gari linaondoka dar linalala shinyanga. Kwa wanatoka dar kuna abiria wanafika siku hiyo hiyo mida yaka ya saa tano usiku.

Kama huna haraka na uko fit basji jaribu basi japo once to or from . bara bara ni 80%. rami
 
Back
Top Bottom