Utaratibu wa kumiliki ndege ndogo Tanzania ukoje?

FaithClass

Member
Jul 16, 2023
14
114
Ninamaanisha dege ndogo ya kawaida (aeroplane) yenye uwezo wa kubeba abiria watatu na helikopta yenye uwezo wa kubeba abiria watatu.

Naomba kufahamishwa:
A. Bei yake ikijumuisha gharama za ununuzi, usafirishaji na usajili

B. Makadirio ya gharama za kuihudumuia kwa mwezi. Wastani wa safari zake kwa mwezi ni kutoka Mwanza kwenda Dar Es Salaam Asubuhi na kurudi Mwanza Jioni

C. Kuna ulazima (Kisheria) wa kuwa na "pilot" zaidi ya mmoja?

D. Kuna unafuu wa gharama (tozo za Serikali) ikiwa itamilikiwa na taasisi ambayo ni non-profiti organization?

E. Utaratibu ukoje kuhusu parking?

F. Sheria inaruhsu kupaki helikopta nyumbani au kwenye uwanja wa ofisi ya taasisi?

Ikiwa kuna taarifa zingine zozote ninazopaswa kufahamu naomba nisaidiwe.

Asante.
 
Matatizo ya ajira yanafanya watu wanadata.

Maana wenye vimilion 15 vya kununuwa IST tu unajuwa bei za magari utapata kwenye websites za used car kama Be forward, SBT Japan and likes, isitoshe google haijawahi kushindwa jambo ambalo lipo online.
Unaifahamu website husika? nimejaribu kuigoogle lakini sijafanikiwa kuipata.
 
Back
Top Bottom