DOKEZO URGENT: Binti wa miaka 16 ameozeshwa kwa lazima kama mke wa pili, huko Laela, Sumbawanga

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Asante Mkombee Asante karesaa....tutenzi taaa....
Laela palikuwa na nuru ya maendeleo lakini.......
 
Niko hapa tayari, nimepokea, nampigia sasa hivi. Huwa napatikana binafsi kwa ujumbe kupitia simu namba 0765345777 na 0734124191. Pia siku hizi Wizara tumezindua JAMII CALL CENTER siku na saa za kazi simu na. 0734986503 na 026 2160250. Karibuni sana Wadau JF na jamii yote kwa ujumla. Umoja ni nguvu, ukatili wa kijinsia haukubaliki.
Aisee Dr.nime appreciate......that's Bravo...you cut the cake....hapan'shaka na wengine wataiga mfano.
 
Kwani sheria ya ndoa ya serikali ya Tanzania inasemaje kuhusu ndoa kama wazazi wa binti wa miaka zaidi ya 14 wameridhia aolewe? Serikali si ilishindwa kwenye kesi ya Rebecca Gyumi kupinga ndoa za utotoni serikali ikakata Rufani ikashindwa tena ikashauriwa irekebishe sheria hiyo ya ndoa lakini mpaka hakuna muswada wowote wa wa mabadiliko ya hiyo sheria ya ndoa uliofikishwa bungeni .Kama serikali haipendi hizo ndoa za utotoni kwanini walikata rufani waliposhindwa mahakamani na Rebecca Gyumi? Haya mnayotuambia hapa ni maigizo tu,kama kweli serikali inadhamira ya dhati a basi hiyo sheria ya binti wa miaka 14 kuolewa ibadilishwe mara moja vinginevyo serikali ikae kimya tu
Kwenye snario ya hiyo ya mleta mada jukwaan Binti Hana consent na hiyo ndyo inaleta lose hapo Kuna force imetumika,

Hiyo case uliyotumia kama reference karudie kuisoma
 
Hata Mimi nimejishtukia balaaa.

#YNWA
Huku hakuna noma...kama kuna jambo we funguka tu....tapika yoote...toa sumu mwilini.....kwa lugha za staha.......halafu huyoooo kalale....ila mie nikipata uchungu...natukana kidooogo.🙂🙂🙂
 
Ahsante Sana nimewasiliana naye tayari. 🙏
Asante sana kwa kuchukua hatua kwa haraka.
Tutafurahi pia kama ukituletea mrejesho wa hili suala baada ya kuwa mmelifanyia kazi ili hili dokezo liwaze kupata 'Closure', itakua pia ni motisha nzuri kwa watumiaji wa hili jukwaa kuendelea kuripoti matukio ya namna hii na kufichua mengine mengi.
Hivyo, kama hautajali mheshimiwa waziri utuletee mrejesho hapa hapa baada ya timu yako kuwa imelifuatilia, kulifanyia uchunguzi na kulimaliza hili suala.
Asante sana.
Dkt. Gwajima D
 
Niko hapa tayari, nimepokea, nampigia sasa hivi. Huwa napatikana binafsi kwa ujumbe kupitia simu namba 0765345777 na 0734124191. Pia siku hizi Wizara tumezindua JAMII CALL CENTER siku na saa za kazi simu na. 0734986503 na 026 2160250. Karibuni sana Wadau JF na jamii yote kwa ujumla. Umoja ni nguvu, ukatili wa kijinsia haukubaliki.
UKO VIZURI MUHESHIMIWA MBUNGE NA WAZIRI!

NIMEPENDA UWAJIBIKAJI WAKO!!

HONGERA SANA!
 
Binti wa miaka 16 anaitwa Recho, yuko kijiji cha NITU, wilaya ya LAELA, Mkoa wa Rukwa.

Ameozeshwa kwa kulazimishwa na wazazi wake pamoja na kaka zake, ambao wamechukua mahari ya shilingi 700,000, tena ameozeshwa kwa mzee kama mke wa pili.

Huyo binti yeye hataki kuolewa na kwa sasa ametoroka, yupo nyumbani kwa mchungaji amejificha. Namba ya mchungaji alipo binti ni 0629 518702, mchungaji anaitwa Baba Irene. Huyu binti anahitaji msaada wa haraka sana, aokolewe kutoka katika hili janga.

Viongozi wa kijiji husika hawana msaada katika hili, kwani wao wanaona ni jambo la kawaida, wameshazoea mabinti huko huwa wanaozeshwa kilazima tu, wala si jambo la kushangaza.

NAOMBA SERIKALI IMSAIDIE HUYU BINTI.
Binti wa miaka 16 ni mtu mzima kabisa....punguza utaahira mkuu!!....

Turning back the hands of time,.....
Mzazi wangu wa kike alibeba ujauzito wangu akiwa na miaka 15... Mwaka mmoja pungufu wa hiyo....!!!

Hakuna mtoto hapo!!!... Na visheria vyenu uchwara sijui sheria ya mtoto!!! ...

Eti mtoto!!... Mtoto!?...mtoto anaukimbilia mshedede!!?.... Get serious man!
 
Nilipoona "binti ametoroka" halafu ukaweka details zote za alipo kwaasa baad ya kutoroka, nikajua ndio walewale
 
Asante sana kwa kuchukua hatua kwa haraka.
Tutafurahi pia kama ukituletea mrejesho wa hili suala baada ya kuwa mmelifanyia kazi ili hili dokezo liwaze kupata 'Closure', itakua pia ni motisha nzuri kwa watumiaji wa hili jukwaa kuendelea kuripoti matukio ya namna hii na kufichua mengine mengi.
Hivyo, kama hautajali mheshimiwa waziri utuletee mrejesho hapa hapa baada ya timu yako kuwa imelifuatilia, kulifanyia uchunguzi na kulimaliza hili suala.
Asante sana.
Dkt. Gwajima D
Hakika nitaletea mrejesho Ili kuimarisha ushirikiano na jamii. Ahsante sana kwa maoni yako, ubarikiwe 🙏🏽
 
Watu mnaotetea bhn mnashangaza.Hivi nyie hao watoto wenu waliopo huko shule akisema hataki shule anataka kuolewa wew utamruhusu?Tatizo ni watu wanaropoka simply kwa sababu sio ndugu,dada,mtoto wao.Pelekeni ujinga wenu huko huko kwenye koo na vijiji vyenu
 
Niko hapa tayari, nimepokea, nampigia sasa hivi. Huwa napatikana binafsi kwa ujumbe kupitia simu namba 0765345777 na 0734124191. Pia siku hizi Wizara tumezindua JAMII CALL CENTER siku na saa za kazi simu na. 0734986503 na 026 2160250. Karibuni sana Wadau JF na jamii yote kwa ujumla. Umoja ni nguvu, ukatili wa kijinsia haukubaliki.
Lete mrejesho
 
Habari za jioni ndugu yangu katika JMT. Nadhani utakuwa umefuatilia mrejesho wa serikali kuhusu hoja uliyoleta. Mara kadhaa kumekuwa na mrejesho kuhusu hatua zinazochukuliwa na serikali juu ya ajenda hii. Hata hivyo, sidhani kama ni sahihi kutotoa msaada na ushirikiano kwa hoja iliyopo sasa dhidi ya manusura ambaye anahitaji msaada kwamba, tukae kimya tu kwa kuwa bado ile hoja ya awali haijafikia mwisho.

Sidhani kama kukaa kimya bila msaada ni sahihi. Hivyo, Kila jambo tutafanyia kazi katika kudhibiti ukatili wa kijinsia kulingana na lilivyo sasa kwa mazingira ya Sasa na wakati ujao nao utafanya kazi kwa mazingira ya wakati huo. Tumeshampata mtoa taarifa Ili kumsaidia manusura wetu. Ahsante Sana, ubarikiwe. usiku mwema,
Tumwache mh afuatilie hili, ndo kazi zao viongozi kuokoa taia pale wanapopatwa na sintofahamu. Huyu binti hakupaswa kuolewa sababu hajaridhia hivo wazazi na mwoaji kosa lao lipo hapo
 
Back
Top Bottom