Tabora: Jela miaka 30 kwa kumbaka mtoto wake wa kufikia

Boran Jakutay

Senior Member
Apr 8, 2023
110
255
IMG_20230607_203044.jpg

Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Tabora imemtia hatiani mwanaume mmoja anayefahamika kwa jina la Samwel Alute na kumuhukumu kutumikia adhabu ya kifungo cha miaka 30 Jela kwa kosa la kumbaka mtoto wake wa kufikia, adhabu ambayo inakwenda sambamba na kulipa faini ya shilingi elfu 50 na kumlipa fidia muathirika wa tukio hilo kiasi cha shilingi elfu 50.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Mkoa wa Tabora, John Mdoe alisema mahakama imepitia ushahidi wa pande zote mbili na kujiridhisha kuwa upande wa Jamhuri umeweza kuthibitisha tukio la ubakaji alilolifanya Samwel kwa mtoto wake wa kufikia mwenye umri wa miaka 16 ambaye jina tunalihifadhi.

Hakimu Mdoe kabla ya kutoa hukumu hiyo alimpa mshitakiwa nafasi ya kujitetea lakini akashindwa kuitumia fursa hiyo, na badala yake akaomba apatiwe nakala ya hukumu, akieleza dhamira yake ya kutaka kukata rufaa.

Awali katika shauri hilo la jinai namba 48 la mwaka 2023 wakili wa upande wa Jamhuri, Ida Rugakingira aliieleza mahakama kuwa mshitakiwa Samwel Alute, mkazi wa Kijiji cha Ifucha Manispaa ya Tabora alidaiwa kutenda kosa hilo kwa tarehe tofauti tofauti mwezi Machi mwaka 2022 kwa mtoto huyo ambaye ni binti wa mke wake.

Chanzo: Azam TV
 
Back
Top Bottom