DOKEZO URGENT: Binti wa miaka 16 ameozeshwa kwa lazima kama mke wa pili, huko Laela, Sumbawanga

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Kwani sheria ya ndoa ya serikali ya Tanzania inasemaje kuhusu ndoa kama wazazi wa binti wa miaka zaidi ya 14 wameridhia aolewe? Serikali si ilishindwa kwenye kesi ya Rebecca Gyumi kupinga ndoa za utotoni serikali ikakata Rufani ikashindwa tena ikashauriwa irekebishe sheria hiyo ya ndoa lakini mpaka hakuna muswada wowote wa wa mabadiliko ya hiyo sheria ya ndoa uliofikishwa bungeni .Kama serikali haipendi hizo ndoa za utotoni kwanini walikata rufani waliposhindwa mahakamani na Rebecca Gyumi? Haya mnayotuambia hapa ni maigizo tu,kama kweli serikali inadhamira ya dhati a basi hiyo sheria ya binti wa miaka 14 kuolewa ibadilishwe mara moja vinginevyo serikali ikae kimya tu
Habari za jioni ndugu yangu katika JMT. Nadhani utakuwa umefuatilia mrejesho wa serikali kuhusu hoja uliyoleta. Mara kadhaa kumekuwa na mrejesho kuhusu hatua zinazochukuliwa na serikali juu ya ajenda hii. Hata hivyo, sidhani kama ni sahihi kutotoa msaada na ushirikiano kwa hoja iliyopo sasa dhidi ya manusura ambaye anahitaji msaada kwamba, tukae kimya tu kwa kuwa bado ile hoja ya awali haijafikia mwisho.

Sidhani kama kukaa kimya bila msaada ni sahihi. Hivyo, Kila jambo tutafanyia kazi katika kudhibiti ukatili wa kijinsia kulingana na lilivyo sasa kwa mazingira ya Sasa na wakati ujao nao utafanya kazi kwa mazingira ya wakati huo. Tumeshampata mtoa taarifa Ili kumsaidia manusura wetu. Ahsante Sana, ubarikiwe. usiku mwema,
 
Niko hapa tayari, nimepokea, nampigia sasa hivi. Huwa napatikana binafsi kwa ujumbe kupitia simu namba 0765345777 na 0734124191. Pia siku hizi Wizara tumezindua JAMII CALL CENTER siku na saa za kazi simu na. 0734986503 na 026 2160250. Karibuni sana Wadau JF na jamii yote kwa ujumla. Umoja ni nguvu, ukatili wa kijinsia haukubaliki.
Muheshimiwa kwa hili pongezi nyingi zikufikie nakuahidi kukufikishia taarifa za unyanyasaji pale tu nitakapobaini watoto wanateseka sana maeneo ya vijijini
 
Asante sana mh waziri kwa wepesi wako wa kuzingatia matatizo ya wtz kwa haraka. Mungu akubariki sana.
Hujielewi ,kama wao

Serikali ipeleke mswada wa mabadiliko ya Sheria ya ndoa Kwa umri 14yrs ,kimsingi bint amekizi vigezo vya kuolewa miaka 17

Labda awe mwanafunzi
 
Ahsanteni sana Wadau wa JF kwa taarifa hii. Huu ndiyo ushirikiano wa jamii tunaohitaji. Tunashughulikia. Ahsanteni kwa mawasiliano ya namba ya simu.

Uwajibikaji ni moja ya sifa muhimu kwa kiongozi. Mheshimiwa Waziri Dkt. Gwajima katika hili unastahili pongezi za dhati.

Tunakuombea kwa Mwenyezi Mungu akujalie uzima na siha njema ili uendelee kufanya kazi kwa weledi.

Tunahitaji kusonga mbele kwa pamoja na kujenga jamii salama ambayo itakuwa chachu ya mabadiliko katika taifa letu.

Kwa mara nyingine tena pongezi kwako Mheshimiwa.
 
Niko hapa tayari, nimepokea, nampigia sasa hivi. Huwa napatikana binafsi kwa ujumbe kupitia simu namba 0765345777 na 0734124191. Pia siku hizi Wizara tumezindua JAMII CALL CENTER siku na saa za kazi simu na. 0734986503 na 026 2160250. Karibuni sana Wadau JF na jamii yote kwa ujumla. Umoja ni nguvu, ukatili wa kijinsia haukubaliki.
Asante Sana mh.waziri

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Kwani sheria ya ndoa ya serikali ya Tanzania inasemaje kuhusu ndoa kama wazazi wa binti wa miaka zaidi ya 14 wameridhia aolewe? Serikali si ilishindwa kwenye kesi ya Rebecca Gyumi kupinga ndoa za utotoni serikali ikakata Rufani ikashindwa tena ikashauriwa irekebishe sheria hiyo ya ndoa lakini mpaka hakuna muswada wowote wa wa mabadiliko ya hiyo sheria ya ndoa uliofikishwa bungeni .Kama serikali haipendi hizo ndoa za utotoni kwanini walikata rufani waliposhindwa mahakamani na Rebecca Gyumi? Haya mnayotuambia hapa ni maigizo tu,kama kweli serikali inadhamira ya dhati a basi hiyo sheria ya binti wa miaka 14 kuolewa ibadilishwe mara moja vinginevyo serikali ikae kimya tu

Vuta pumzi kidogo!

Binti hataki kuolewa wazazi na ndugu wanamlazimisha.

Haki za Binti zinasimamiwa na serikali chini ya wizara ya Doctor Gwajima, Tatizo liko wapi?
 
ila wahuni mtaani wakimtafuna wakamtia mimba fresh au sio! waafrica inatakiwa tuachane na mentality za kipuuzi za kumezeshwa na wazungu.
Kwa niaba ya wahuni hapa sumbawanga nimekutumia inbox"TAMKO LA BARAZA WAHUNI LAELA,SUMBAWANGA" Lisomwe stendi zote nchini
 
Back
Top Bottom