DOKEZO URGENT: Binti wa miaka 16 ameozeshwa kwa lazima kama mke wa pili, huko Laela, Sumbawanga

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Ahsanteni sana Wadau wa JF kwa taarifa hii. Huu ndiyo ushirikiano wa jamii tunaohitaji. Tunashughulikia. Ahsanteni kwa mawasiliano ya namba ya simu.
Gwajima.

Kwa mfano binti ww umri wa chini ya miaka 18 kaona elimu haina maana kwake na karidhia kuolewa sheria inasemaje?
 
Gwajima.

Kwa mfano binti ww umri wa chini ya miaka 18 kaona elimu haina maana kwake na karidhia kuolewa sheria inasemaje?
Hoja hapa ni lalamiko la mleta maada kua Binti analazimishwa kuolewa bila ridhaa yake na Wazazi wake! Binti asikilizwe kwanza Kama hataki kuolewa, anataka nini!!??
 
Kwa taarifa ya Wanajamvi, Laela ni Kata mojawapo katika Wilaya ya Sumbawanga Vijijini, Mkoani Rukwa na si Wilaya kama ioivyoandikwa hapo juu.
 
Gwajima.

Kwa mfano binti ww umri wa chini ya miaka 18 kaona elimu haina maana kwake na karidhia kuolewa sheria inasemaje?
Said, ahsante kwa swali lako, kifupi ni kwamba; siyo haki kumlazimisha yeyote yule kufanya jambo la kuhusu maisha yake ambalo yeye anaona hayuko tayari. Ndoa ni taasisi ya maridhiano siyo lazima, vinginevyo kinachoandaliwa hapo ni maisha ya kukatiliana tu kuanzia wanandoa hadi watoto iwapo watajaliwa kuwa nao. Ana haki ya kulalamika huyu iwapo amelazimishwa na Serikali ina wajibu wa kumsikiliza. Ahsante.
 
Binti wa miaka 16 anaitwa Recho, yuko kijiji cha NITU, wilaya ya LAELA, Mkoa wa Rukwa.

Ameozeshwa kwa kulazimishwa na wazazi wake pamoja na kaka zake, ambao wamechukua mahari ya shilingi 700,000, tena ameozeshwa kwa mzee kama mke wa pili.

Huyo binti yeye hataki kuolewa na kwa sasa ametoroka, yupo nyumbani kwa mchungaji amejificha. Namba ya mchungaji alipo binti ni 0629 518702, mchungaji anaitwa Baba Irene. Huyu binti anahitaji msaada wa haraka sana, aokolewe kutoka katika hili janga.

Viongozi wa kijiji husika hawana msaada katika hili, kwani wao wanaona ni jambo la kawaida, wameshazoea mabinti huko huwa wanaozeshwa kilazima tu, wala si jambo la kushangaza.

NAOMBA SERIKALI IMSAIDIE HUYU BINTI.
TUNAOMBA MREJESHO, ULIFANIKIWA AU VIONGOZI WALIMEZEA?
 
Bora huyo kaozeshwa kuliko hawa wanaozalia nyumbani.
Wanafanya ngono kwenye huo umri mdogo na hamuwafanyi kitu. Wanatoa mimba na hamuwafanyi kitu. Hakun wa nafuu wote ni walewale
 
Wewe una akili sana. Hongera kwa kujitambua. Wengine hata angekuwemo Rais kama Rais bado wangezidisha ujinga wao.
Kile face book wanatukanagwa hao viongozi wenu mpaka basi. Mamia ya vijana huwatukana, sasa watawafunga wangapi?
Aliefanikiwa kuheshimiwa ni JKN naye alitimia ubabe.
Vitendo vta kiongozi hupelekea aheshimuwe au adharauliwe. Imagine umeme unakatika hivi nani atawaheshimu hao.
 
Back
Top Bottom