Wanaodhani wengine tunaipenda tu Chadema (kama makada wa CCM walivyo) wanakosea sana,akina Habib Mchange ni mmojawapo wa watu wanaodhani Chadema imefika hapo pa kupendwa tu.
Sina muda wa kujadili hoja zake dhaifu lakini namtahadharisha kuwa Watanzania tunataka mabadiliko kwa namna yeyote,Watanzania watampa nafasi yule waliyenae mtaani kila siku akiwatetea kwa moyo mmoja bila hila,Watanzania wanataka mtu safi na kiongozi aliyekomaa kwelikweli na amedhihirisha hivyo kwa vitendo na si kwa simulizi zake kutuambia aliyofanya kama vile sisi ni vipofu!
Hawa akina Mchange wasameheni tu ni vijana wadogo wanaodhani wameshakomaa kisiasa na sifa zinawaharibu sana.Someni makala hiyo muone kama kuna kijana aliyeiva hapo!!!
Wewe wawapi usiyejua kwamba mgombea urais atapatikana baada ya mchakato ndani ya chama,cdm ni chama kikubwa kuliko unavyoweza kufikiri na kwamba hakiwezi kuongozwa na kauli nyepesi zinazotoka kwenye akili ndogo kama yako.upatu unaoufanya haukijengi chama,kina heche wanazunguka kukijenga chama wewe umekaa kibaha ukiendelea kupiga ramli.Akili ndogo haiwezi kuiongoza akili kubwa kamwe ndani ya cdm.
John Heche anawapagawisha kwa jinsi anavyokubalika vijijini.Yule ni habari ingine,hawa wapika majungu wamebaki tu kutukana kupitia Facebook
John Heche anawapagawisha kwa jinsi anavyokubalika vijijini.Yule ni habari ingine,hawa wapika majungu wamebaki tu kutukana kupitia Facebook
Kamanda Mchange, Kamanda, Matata, Kamada Zitto, Kamanda Chagulani, Kamanda Shibuda, Makamanda Madiwani wa Arusha, fungukeni watanzania wapo nyuma yenu.
Zitto celibate man tumweke ikulu ikulu sio ya wahuni, bado anahitaji kwenda club bado anatafuta mchumba. Afanye kwanza hayo na aacha undumila kuwili he will be considered not now!
By ze wei Lile hammer na Vogue kayatoa wapi vile?
Nashindwa kumuelewa mwandishi wa makala hiyo hapo kwenye wino mwekundu.Tunauelewa mchango wa Zitto na wabunge wengine wa CHADEMA katika bunge,hapa mwadishi anajaribu kutushawishi ya kua M4C haina umuhimu au kuna mgawanyiko ndani ya CHADEMA kuhusiana na M4C.Hapo kuna hoja ya tani moja japokuwa si Zitto peke yake anayefanya vizuri bungeni kupitia CDM lakini kama wabunge wote watafanya vizuri bungeni basi huo ni mtaji wa kisiasa tosha kwa CDM. Nadhani jamaa huenda alikuwa anataka kukumbusha jinsi ambavyo wabunge wa CDM walivyomtupa mkono Zitto kwenye hoja yake ya kupinga posho za vikao!
Hivi unakijua unachoandika kweli? Mwaka 2015 Zitto atakuwa na miaka 39, na katiba ya sasa inasema mgombea urais awe na umri wa kuanzia miaka 40. Labda uniambie katiba ijayo itaruhusu mgombea wa miaka 35, jambo ambalo mimi siliungi mkono. Umri wa kugombea urais ubaki huo huo wa miaka 40. Habari za kutuwekea watu wa kwenda kufanya utoto Ikulu hatutaki. Hiyo akili ya Zitto yenyewe haitoshei hata kuwa waziri mkuu, halafu anatafuta urais. Dogo aache kujikweza huyu, awe na subira. Tumpe Slaa miaka mitano arekebishe mambo, baada ya hapo Zitto aingie. Hivi hakuna watu wenye hekima wa kumwelekeza huyu dogo apunguze uroho wa madaraka?Mkuu hujui kuna mchakato wa kuandika katiba upya na vijana wanataka umri wa kugombea urais uwe kuanzia miaka 40? Hujui kwamba ahadi ya Rais JK ni kwamba katiba mpya itapatikana kabla ya uchaguzi wa mwaka 2015? Ikiwa hivyo na bahati nzuri umri ukapunguzwa hadi miaka 40 basi Zitto atakuwa ndani ya wigo.
Kamanda Mchange, Kamanda, Matata, Kamada Zitto, Kamanda Chagulani, Kamanda Shibuda, Makamanda Madiwani wa Arusha, fungukeni watanzania wapo nyuma yenu.