Mkuu wangu kwanza shukran sana kwa kutoa tahadhali iliyopo mbele ya chama. Nachoweza kuongezea tu leo hii ni kwamba swala la UMRI kupunguzwa tayari limekwisha pitishwa ni swala kusubiri lini itatangazwa kuwa sheria.. Na hii imetokana pia kuwa moja ya silaha ya CCM kuitumia dhidi ya CDM baada a kugundua kutaleta mgogoro mkubwa kwao ktk uchaguzi ujao.Nasema ILIBIDI kwa kuwa sina uhakika kama hili litatokea kutokana na sababu kadhaa ambazo tayari wananchi tunazijua. najaribu kuiona Tanzania baada ya 2015 na ninaona picha ambayo si njema sana kwa upanzani. CCM iko katika mikakati mingi sana ya kujipanga. Toka leo hadi 2015 si muda mwingi lakini kisiasa si muda mchache hata kidogo. CCM ina nafasi na faida kubwa ya kushika tena Dola pindi ikiamua kuweka japo 1/3 ya kasoro zake kando, na kwa akili za watanzania ni wazi kuwa njia yao itakuwa nyeupe.
CCM inahitaji mpinzani madhubuti ifikapo 2015. Kiukweli inahitaji damu changa ambayo itaongozwa na mawazo ya wazee wa chama. Na viongozi wa chama waanze kujipanga tangu sasa kumuandaa huyo damu changa tangu sasa kwa kuwa katika hali halisi ukimuacha Dk Slaa, ni Zitto pekee anayekubalika kitaifa japo yuko upinzani. Zitto simjui na kwa maana hiyo hanijui.
Jambo la kufanya sasa hivi ni kuona kuwa maoni ya kutosha yanapatikana katika kipengele cha kupunguza umri wa kugombea nafasi ya Urais. Nasema naiona Tanzania baada ya 2015 na karata za upinzani zisipopangwa vyema ni wazi kuwa upinzani utapoteza tena. Mbaya zaidi upinzani ukipoteza hapo 2015 ni vigumu kuendelea kuwa na nguvu ya kipinzani iliyoko sasa, toka kwa wananchi pamoja na upinzani wenyewe.
Katika kuona pia kuwa mgombea anaandaliwa kuanzia sasa, itampa huyu mgombea ari na shauku na moyo wa kujipanga katika kufikia lengp la chama na Taifa kwa ujumla. Kama lengo si kushika Dola basi Zitto asiteuliwe, ila kama lengo ni kushika Dola basi ateuliwe, japo ccm wanaweza kutumia mbinu chafu kama walizotumia 2010.
Katika uchaguzi wa 2015, Zitto atakuwa na nguvu za kiushawishi kama alizokuwa nazo Dk Slaa kipindi kilichopita. Kama itajulikana kuwa umri utarekebishwa katika kipengele cha urais basi cdm isisite kufanya haya maamuzi mazito kwa mustakabali wa chama na Taifa. Viongozi wa cdm watazame huu ujumbe kwa mtazamo tofauti kidogo maana baada ya uchaguzi mkuu unazi utawasuta kama hawatataka kubadilika.
Kadhalika pale ambapo patahitaji muungano wa vyama katika kukipiku ccm, basi vyama visisite kufanya hivyo.
Hivyo wana CDM jiandaeni mapema na swala hili maana Zitto lazima agombee na mkianza kuparuzana leo hii sijui itakuwaje Mwaka 2015 maana makundi yenu ndani ya chama tayari yamewapa CCM mwanya wa kuwalisha chambo..Kubadilisha kwa miaka (kushushwa) hakutakuwa na madhara kwa CCM maana wao tayari wameisha jipanga vizuri..