Urais wa Muungano 2015 ni zamu ya Zanzibar - Maalim Seif

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad amesema si haki hata kidogo Rais wa muungano atoke upande wa bara tu kila awamu.

Maalim Seif amesema kamwe haikubaliki kwani ni nchi mbili huru ziliungana. Ameongeza huu ni upendeleo wa waziwazi ambao katiba mpya itabidi iufanyie kazi kwa maslahi ya nchi hizi mbili.

SOURCE: HABARI ITV
 
Nimeamini kweli Maalim Karudi CCM. Haya ni matamshi ya chini kwa chini ya CCM Zanzibar. Tanzania hatuachagua rais kwa kuangalia anatoka wapi bali Tanzania kama nchi tunachagua mtu yeyote atakayetupeleka mbele.

Urais si kitumbua cha kula na kuachiana. What if Zanzibar hakuna aliyequalify? yaani tumuweke mtu tu hata kama mwendawazimu?. Wanzibar waliisigina nafasi adhimu sana mwaka 2005 kwa kuacha kumuunga mkono Salim. Wao wenyewe walimuanzishia fitina kuwa ni Hizbu kwa ahadi za vyeo toka kwa wanamtandao. Sasa leo hii wapo nje ya vyeo wanamtumia Hamad Seif Sharif.

Kwa mzanzibar kupata urais wa Tanzania ni mpaka atakapopatikana mtu kma Dr Salim na hii itawachukua miaka hamsini ijayo.
 
Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad amesema si haki hata kidogo Rais wa muungano atoke upande wa bara tu kila awamu.Maalim Seif amesema kamwe haikubaliki kwani ni nchi mbili huru ziliungana.Ameongeza huu ni upendeleo wa waziwazi ambao katiba mpya itabidi iufanyie kazi kwa maslahi ya nchi hizi mbili. SOURCE HABARI ITV.

What is wrong?? Wazanzibar wajitokeze kugombea, bara wajitokeze wagombee, vyama vitachuja!! WE need the right President!! Hakuna kubebana!!
 
Makamu wa kwanza wa rais wa Zanzibar Maalim Seif akizungumza na waandishi wa habari, ametaka suala la zamu ya urais wa muungano kati ya bara na zenj iingizwe kwenye katiba mpya. Je mnaona ni sahihi kuingiza zamu kwenye utawala wa nchi?
 
maalim seif, kumbuka cheo ni dhamana na hatutachagua rais eti kwa kuangalia uzanzibar wake au utanganyika wake.tunamchagua mtu kwa vile ana sifa tunazozihitaji kwa kipindi hicho.
 
kwa katiba iliyopo siyo haki kwa rais wa muungano atokee zanzibar kwani huyu ndo anayesimamia mambo ya muungano na yale yasiyo ya muungano kwa upande wa tanzania bara ilihali pia kuna rais wa zanzibar anayesimamia maslahi yasiyo ya muungano ya zanzibar.
sasa sioni kwanini mzanzibar asimamie maslahi ya tanganyika ambayo siyo ya muungano.
km katiba mpya itatambua urais wa muungano kwa zamu itabidi pia tudai iwepo serikali ya tanganyika pia.
 
Miaka ishirini hatujakwaa rais wa muungano, sasa zamu yetu,venginevo twapandisha bendera ya ASP.
 
Heri kutoungana kuliko kuwa na utaratibu wa namna hii. Haya ni mawazo ya ujima. Urais unafuata uwezo. Kesho atasema tuwe na utaratibu wa kuangalia asili ya mtu eg uarabu, uasia. Kwani weusi wametawala mno.
Huyu achinjiwe baharini asije sababisha watu kuanza kudai uraisi uwe zamu kikanda.
 
Duh! Maalim ameanza kumchonoa Profesa? Ina maana hataki Lipumba agombee tena na mgombea wa CUF atoke Zenji?
 
maalim seif, kumbuka cheo ni dhamana na hatutachagua rais eti kwa kuangalia uzanzibar wake au utanganyika wake.tunamchagua mtu kwa vile ana sifa tunazozihitaji kwa kipindi hicho.

Nimeamini kweli Maalim Karudi CCM. Haya ni matamshi ya chini kwa chini ya CCM Zanzibar. Tanzania hatuachagua rais kwa kuangalia anatoka wapi bali Tanzania kama nchi tunachagua mtu yeyote atakayetupeleka mbele. Urais si kitumbua cha kula na kuachiana. What if Zanzibar hakuna aliyequalify? yaani tumuweke mtu tu hata kama mwendawazimu?. Wanzibar waliisigina nafasi adhimu sana mwaka 2005 kwa kuacha kumuunga mkono Salim. Wao wenyewe walimuanzishia fitina kuwa ni Hizbu kwa ahadi za vyeo toka kwa wanamtandao. Sasa leo hii wapo nje ya vyeo wanamtumia Hamad Seif Sharif.

Kwa mzanzibar kupata urais wa Tanzania ni mpaka atakapopatikana mtu kma Dr Salim na hii itawachukua miaka hamsini ijayo.
Agombee tuu tutamchuja kwenye uchaguzi mkuu au anataka wagombee wazanzibari tuu; kumbe unaweza kuwa na nafasi ya juu tu serikalini ila ukawa huna uwezo wa kufikili
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom