Urais wa Muungano 2015 ni zamu ya Zanzibar - Maalim Seif

huu u.j.i.n.g.a wa upendeleo na kupeana nafasi bila uwezo ndio.umetufikisha hapa .... futilia mbali nafasi zote za upendeleo ... kila mtu achaguliwe kiushindani moja kwa.moja na wananchi .... wabunge wawakilishe ratio sawa wananchi kwa tanzania nzima
 
Kama haya maneno yamesemwa kweli, basi ni Upuuzi mtupu. Na wakristo wakisema safari hii lazima awe mkristo, patatosha kweli?? Ni ufinyu wa mawazo.
 
Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad amesema si haki hata kidogo Rais wa muungano atoke upande wa bara tu kila awamu.

Maalim Seif amesema kamwe haikubaliki kwani ni nchi mbili huru ziliungana. Ameongeza huu ni upendeleo wa waziwazi ambao katiba mpya itabidi iufanyie kazi kwa maslahi ya nchi hizi mbili.

SOURCE: HABARI ITV

katiba mpya ipi wakati mwenyekiti wake aliongoza walk out?? au haamini ukawa?
 
Rais atatoka bara yaani Tanganyika. Mtake msitake sababu hamna sifa kwa sasa na mnaonyesha kuwa ni wabaguzi. Hivyo, atatoka Tanganyika kwa Nyerere, mmesikia wazenji?
 
kwa katiba iliyopo siyo haki kwa rais wa muungano atokee zanzibar kwani huyu ndo anayesimamia mambo ya muungano na yale yasiyo ya muungano kwa upande wa tanzania bara ilihali pia kuna rais wa zanzibar anayesimamia maslahi yasiyo ya muungano ya zanzibar.
sasa sioni kwanini mzanzibar asimamie maslahi ya tanganyika ambayo siyo ya muungano.
km katiba mpya itatambua urais wa muungano kwa zamu itabidi pia tudai iwepo serikali ya tanganyika pia.
Kama hutaki twende kwenye tatu,Kwani nani alie wambia muchanganye kunde na mtama?
 
Wanabodi,

Kwa kuanzia naomba kwanza tukubaliane kuwa siasa kweli ni mchezo mchafu!. (Politics is a dirty game!).

Tulipoungana ile 1964, aliyeomba muungano ni Karume, sababu sote tunazijua!. Wakati akiomba kuungana alimwambia Nyerere, wewe rais, mimi makamu!.

Akimaanisha urais ungeshikwa na mtu wa Tanganyika na Zanzibar ingetoa makamu!.

Muungano ulipofika mahali fulani, Karume akasema muungano ni kama koti, likikubana, unalivua!.
Kilichofuatia sote tunakijua!.

Alipokuja Jumbe, mambo yake yalikuwa safi mpaka alipouchokoa muungano!, kilichompata sote tunakijua!.

Mwalimu Nyerere alipoamua kuachia madaraka, kwa nia njema kabisa aliamua kujenga mazingira ya kupokezana!. Maadamu yeye ametoka bara, anayemfuatia lazima atoke visiwani, ndipo akaja Mwinyi.

Mwinyi alipomaliza ilikuwa ni zamu ya bara hivyo akaja Mkapa. Mkapa alipomaliza ilikuwa iwe ni samu ya Zanzibar, wakati wa kipindi cha Mkapa, iliisha julikana huyo Mzanzibari ambaye angekuja ni nani, ila sote tunajua ni nini kilimkuta!, hivyo ikabidi zamu irudi bara ndipo JK akaingia!.

Japo haijaandikwa popote, ila kwa vile 2005 ilikuwa iwe zamu ya Zanzibar, lakini ikashikwa na rais kutoka bara, hivyo ili kuwatendea haki wenzetu Wazanzibari, kiukweli kabisa kama tunafuata haki bin haki, mgombea wa CCM kwa mwaka 2015, anapaswa kutoka Zanzibar ili kuwatendea haki zamu yao ambayo ilibidi kupokwa na bara!.

Swali ni jee CCM itawatendea haki wenzetu Wazanzibari?.

Kama tutawatendea haki, jee ni Mzanzibari gani ndani ya CCM mwenye sifa na uwezo wa kuchagulika kuwa rais wa JMT ili kuwatendea haki wenzetu hawa nao watioe rais wa JMT maana haiwezekani 2015 ikawa ni zamu ya bara tutakuwa tumetoa rais kwa vipindi vitatu mfulilizo as if wenzetu hawana mtu mwenye uwezo wa urais?!.

Naomba kuwasilisha.

Pasco.
Nawatakia maadhimisho mema ya sikukuu ya muungano.
Paskali
 
Makamu wa kwanza wa rais wa Zanzibar Maalim Seif akizungumza na waandishi wa habari, ametaka suala la zamu ya urais wa muungano kati ya bara na zenj iingizwe kwenye katiba mpya. Je mnaona ni sahihi kuingiza zamu kwenye utawala wa nchi?
Sio sahihi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom