Mkutano wa 3 kuenzi Maisha ya Maalim Seif Sharif Hamad, Novemba 26, 2023 - Zanzibar

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Taasisi ya Maalim Seif Foundation ikishirikiana na Taasisi ya Friedrich Naumann Foundation imeratibu Mkutano wa Tatu wa Kumkumbuka na Kumuenzi Maalim Seif Sharif Hamad unaofanyika kwa siku mbili tarehe 25 - 26 Novemba, 2023 katika Hoteli ya Golden Tulip Airport, Zanzibar.

Kiongozi wa Chama cha Build One South Africa (BOSA) cha nchini Afrika Kusini, Mmusi Maimane naye anashiriki katika mkutano huo.

Maudhui ya Mkutano wa mwaka huu ni “Siasa, Uongozi na Utawala: Tumekosea Wapi, Tujisahihishe Vipi?”.

Mkutano huu wa Tatu unalenga kutafakari na kutathmini maudhui hayo kwa kuangalia mwenendo wa siasa na uongozi kitaifa na kimataifa yakiwemo masuala ya kutetereka kwa maadili na misingi ya siasa na uongozi;

Mambo yanayoathiri ushindani ulio sawa katika uwanja wa siasa; ushindani wa kisiasa ulioacha misingi na kujikita zaidi kwenye siasa chafu; kuibuka kwa siasa zinazolenga kucheza na akili za watu kwa kuwapa majibu mepesi kwa maswala mazito (populism) na athari zake kwa demokrasia;

Siasa na uongozi katika zama za kidijitali na hasa mitandao ya kijamii; vipi kurudisha hamu na ushiriki wa rika la vijana katika siasa na uongozi; na vipi kuoanisha siasa na maendeleo ya nchi.

Jumla ya washiriki 180 wamealikwa kuhudhuria Mkutano huu.

Majadiliano ya leo Novemba 26, 2023 ni Siasa zetu kwa mtazamo wa Waandishi wa Habari – Je, Vyombo vya Habari vimeweza kutimiza wajibu wake kama mhimili wa nne kwenye nchi kwa kuibua siasa za masuala, kuilinda demokrasia na kusimamia uwajibikaji?
  • Absalom Kibanda, Salma Said, Hawra Shamte, Khalifa Said
  • Mwenyekiti wa Majadiliano: Mohamed Ghassani

  • Mwenyekiti wa Majadiliano: Mohamed Ghassani
  • Absalom Kibanda, Salma Said, Hawra Shamte, Khalifa Said
Kiongozi wa chama cha upinzani cha Afrika Kusini, Build One South Africa, Mmusi Maimane ni mgeni mwalikwa katika tukio hili.

SALMA SAID: KAMA VIONGOZI WA JUU HAWAAMINI? KWA WANANCHI ITAKUWAJE?
ZANZIBAR: Taasisi ya Maalim Seif Foundation imeandaa mkutano wa Tatu kuuenzi mchango wa Maalim Seif Hamad katika uongozi Tanzania, Kauli Mbiu ya mkutano huu ni Siasa, Uongozi na Utawala: Tumekosea Wapi, Tujisahihishe Vipi?

Akichangia mada kuhusu Vyombo vya Habari, Mwanahabari Salma Said anasema hakuna usawa katika kuripoti taarifa za viongozi wa Kijamii kwa kuwa vinaanzia juu na kuonesha hali ya ubaguzi hadi katika nafasi za juu.

Amesema “Kama viongozi wa juu wanabaguana na hawaaminiani huku kwa Wananchi itakuwaje? Kunatakiwa kujengwa imani ya juu kuanzia viongozi wa juu wa Serikalini.”

KHALIFA SAID: TASNIA YA HABARI INA HALI MBAYA LAKINI WAPO WANAOFANYA MAMBO MAKUBWA
Mwanahabari Khalifa Saidi amesema tasnia ya Habari kwa jumla ina hali mbaya lakini kuna watu wanaendelea kufanya vizuri.

Amesema Serikali ya Tanzania inapenda mambo ya udhibiti, hali hiyo sio tu kwenye Tasnia ya Habari bali hata sehemu nyingine ikiwemo katika Siasa na kwenye Taasisi Binafsi zinavyofanya kazi.

KHALIFA SAID: KUNA VYOMBO VYA HABARI VINAENDESHWA KINYUME CHA SHERIA
Mwanahabari Khalifa Saidi ameeleza Sheria ya Habari ya Mwaka 2016 imesababisha baadhi ya taasisi zijiendeshe kinyume cha Sheria huku Serikali ikiwa kimya kwa kuwa anaamini mamlaka zinaweza kuja kutumia Sheria hiyo dhidi ya Taasisi au Kampuni zinazojiendesha kinyume cha utaratibu.

WAKILI AWADH SAID: KATIBA HAIJATAJA CHAMA TAWALA KUSIMAMIA SERIKALI
Wakili Awadh Said anasema “Tunaona Watendaji wa Chama Tawala wanaingilia Utumishi wa Umma, tabia hiyo itakua, Itazoeleka na itaota mizizi, Katiba ya Zanzibar haijakwambia kabisa kuwa Itikadi, Ilani ya Chama tuliyopeleka kwenye uchaguzi ndio itasimamia Serikali, chama ni kama Mshenga tu.”

Anasema “Utumishi wa Umma hautakiwi kuingizwa kwenye Siasa, hiyo ni Taasisi Imara, ndio Nchi, ndio inayoleta Maendeleo, tuuache Utumishi wa Umma ufanye kazi kwa mujibu wa Katiba, Kanuni na Sheria ndio maana anakabidhiwa muongozo wa Serikali.”

WAKILI AWADH SAID: SERIKALI NI KATIBU MKUU KIONGOZI NA MAKATIBU WAKUU WAKE
Wakili Awadh Said anasema “Katibu Mkuu wa Wizara ndio Serikali na ndiye anayesaini, Waziri hawezi kujisainia kupata hata senti tano, Katibu Mkuu Kiongozi na Makatibu Wakuu ndio injini ya maendeleo ya Nchi yeyote.”

Amesema hayo wakati wa Mkutano wa kumuenzi Maalim Seif uliofanyika Zanzibar, alipokuwa akizungumzia umuhimu wa Utumishi wa Umma.

Taasisi ya Maalim Seif Foundation ikishirikiana na Taasisi ya Friedrich Naumann Foundation imeratibu Mkutano wa Tatu wa Kumkumbuka na Kumuenzi Maalim Seif Sharif Hamad unaofanyika kwa siku mbili tarehe 25 - 26 Novemba, 2023 katika Hoteli ya Golden Tulip Airport, Zanzibar.

Kiongozi wa Chama cha Build One South Africa (BOSA) cha nchini Afrika Kusini, Mmusi Maimane naye anashiriki katika mkutano huo.

Maudhui ya Mkutano wa mwaka huu ni “Siasa, Uongozi na Utawala: Tumekosea Wapi, Tujisahihishe Vipi?”.

Mkutano huu wa Tatu unalenga kutafakari na kutathmini maudhui hayo kwa kuangalia mwenendo wa siasa na uongozi kitaifa na kimataifa yakiwemo masuala ya kutetereka kwa maadili na misingi ya siasa na uongozi;

Mambo yanayoathiri ushindani ulio sawa katika uwanja wa siasa; ushindani wa kisiasa ulioacha misingi na kujikita zaidi kwenye siasa chafu; kuibuka kwa siasa zinazolenga kucheza na akili za watu kwa kuwapa majibu mepesi kwa maswala mazito (populism) na athari zake kwa demokrasia;

Siasa na uongozi katika zama za kidijitali na hasa mitandao ya kijamii; vipi kurudisha hamu na ushiriki wa rika la vijana katika siasa na uongozi; na vipi kuoanisha siasa na maendeleo ya nchi.

Jumla ya washiriki 180 wamealikwa kuhudhuria Mkutano huu.

Majadiliano ya leo Novemba 26, 2023 ni Siasa zetu kwa mtazamo wa Waandishi wa Habari – Je, Vyombo vya Habari vimeweza kutimiza wajibu wake kama mhimili wa nne kwenye nchi kwa kuibua siasa za masuala, kuilinda demokrasia na kusimamia uwajibikaji?

  • Absalom Kibanda, Salma Said, Hawra Shamte, Khalifa Said
  • Mwenyekiti wa Majadiliano: Mohamed Ghassani

  • Mwenyekiti wa Majadiliano: Mohamed Ghassani
  • Absalom Kibanda, Salma Said, Hawra Shamte, Khalifa Said
Kiongozi wa chama cha upinzani cha Afrika Kusini, Build One South Africa, Mmusi Maimane ni mgeni mwalikwa katika tukio hili.

Jambo jema.
Lkn waislam tunahimizwa tifanye haya kabla ya kufa.
1. Kuwaachq Watoto wema ambao watakaokuombea dua baada ya kufariki( yaani mtoto anaeijua dini yake na hapa umuhimu wa mwanao kumpeleka madrasa badala ya kumpeleka international school tu.
2. Sadaq ljaria. Yaani kujenga madrsa', misikiti na huduma nyengine za jamii . Hapa umuhimu wa kuwa karibu na dini yako.
3. Elimu ya dini ambayo utawafundisha wengine.

HAYA NDIO MAMBO BAADA YA KUFARIKI YATAKUFAA DAIMA KTK MAISHAYAKO.MENGINE YOTE TUKIFANYIWA NA BINAADAM BAADA YA KUFARIKI NI SAWA NA 0

Huu ni ukumbusho kwa waislam wenzangu.
Au nakusea wadau?
 
Jana nilikuwa naufuatilia mkutano huu kwenye YouTube Salumu Mwalimu wa CHADEMA alimchakaza vibaya sana Kitila Mkumbo na kuweka bayana unafiki wa so called Vijana wasomi wa Tanzania aisee...nilicheka sana.
 
Hakuna mwanahabari au chombo cha habari kinaweza kusema ukweli wote haswa top secrets...hakuna. Habari karibia zote hupukwa upya. John Swinton, Mhariri mkuu wa Zamani wa gazeti la New York times ambaye walimtambua Kama mkuu wa waledi yaani The Dean of his Profession...Alisema...Iwapo utakuwa mpumbavu kuandika maoni yako halisi kesho yake utajikuta barabarani ukisaka ajira mpya...Tu mipira irukayo, wao huvuta Uzi nasi kurukaruka, talanta zetu na maisha yetu vyamilikiwa na watu wengine. Sisi ni wataaluma makahaba.

Hakuna utakachoambiwa Cha ukweli wote...lazima ukweli upotoshwe tu kwa gharama zote.
 
Attachments

  • IMG_20231126_163824_956.jpg
    IMG_20231126_163824_956.jpg
    116.3 KB · Views: 1
Back
Top Bottom