econonist
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 15,818
- 21,816
Hakuna wakati muafaka Kama huu kwa chama Cha CHADEMA kwenda kuwekeza nguvu Zanzibar. Sababu zangu kwa ombi Hilo ni zifuatazo.
1. Kwanza, Kwa Sasa harakati za kisiasa Zanzibar zimepoa baada ya Maalim seif Kuondoka duniani. Hivyo kwa Sasa upinzani Zanzibar hauna political figure kama ilivyokuwa kwa Maalim Seif. Akina Ismail jussa ni kama wapo kimya na wameshindwa kuwa key figures.
2. Pili, chama Cha ACT kipo kwenye serikali ya umoja Zanzibar,hivyo kufungwa gavana kutokana na makubaliano. Hii inaipa CHADEMA nafasi ya kujijenga Kama chama kikuu Cha upinzani Zanzibar kisichofungamana na serikali ya Zanzibar ambacho kitakiwa huru kuelezea agenda ya wazazibari bila hofu.
3. Tatu, CHADEMA kujijenga na kuwekeza nguvu Zanzibar kutaifanya kuwa chama Chenye sura ya Muungano. Maana kwa Sasa kinaonekana Kama chama Cha bara pekee. Na hivyo kuleta ushindani wa kisiasa.
4. Nne, CHADEMA watumie kukubalika kwao kwa baadhi ya wapinzani Zanzibar kujijenga. Kwa mfano kwenye uchaguzi wa 2020 wakati wa kampeni za urais CHADEMA, wazanzibar wengi walijitokeza kumsikiliza Mgombea Tundu Lissu na walimwelewa Sana. Hii inammanisha Kuna wazanzibar wanaiamini Sana misimamo ya CHADEMA na wangependa kiwe active kule visiwani.
Nihitimishe kwamba, kwa Sasa Zanzibar inakihitaji chama Cha CHADEMA kuliko wakati wowote, na kikiingia kule ni miaka mitano tu kitakiwa kimejisimika. Aliyeipa nguvu ACT ni Maalim Seif, Sasa hayupo wanategemea zaidi Makamu wa kwanza wa Rais ambaye hajawa influencial Kama Maalim Seif alivyokuwa.