Upole!!

Mi nina gf wangu mnyarwanda...yani ni mpole kushinda hata hayo maelezo ya mtoa mada!!siku za mwanzo za mahusiano nikimwangalia nilikuwa najisihi kulia-lia tu,coz ni decent,kapole hadi kanatia huruma...ingawa sasa hivi etlist ninampa maujanja. bt i real like her
 
Njoo kwangu Lizzy,Mm ni mkali Tundu Lissu haoni ndani,halafu mkono wangu huwa mwepesi kama Sufu na ninapata joto haraka kama Petrol!!
 
Hata sikumbuki....ila misamaha leo imeisha!!
Natumaini kwa Asha utapata nafasi ya kuweka vibegi vyako!!:A S cry:!:phone:

Basi nimetubu mamii, usiende kwa kolokuwini

Kosa gani mimi nililokukosea wanitupa

Mrembo mwenye hadhi, pokea tena waraka
Usome na kuhifadhi, Yote nilioyoyandika
Nilipi lililokuudhi, Hebu niambie haraka

Fanya haraka muhibu, unipe hili hakika
Uneleze taratibu, Nipate kutoa shaka
Ni ipi hiyo sababu, Ilokupa kunepuka

Muhibu Lizzy nasema nawe, Hebu mwepushe shetani
Nyonda sinizuzuwe, Kanitia fedhehani
Toka kuniepuka wewe, Nimengia matesoni

Usione ni mzaha, mwenzio ni maradhini
Umenitia jeraha, La huba ndani kwa ndani
Naishi sina furaha, Kwa yondi lako Fulani

Kukurai si aibu, maadamu nakutaka
Na lau kama muhibu, Liko kosa limetuka
Basi mwana nimetubu, Msamaha nautaka

Kaditama tafadhali, wata kunihangiasha
Mwenzio kucha silali, Kwa huba huwa nakesha
Kumbuka na jambo hili, Kwako mahaba sijesha
 
Back
Top Bottom