Upole!!

Unapenda wakali lizzy, tena wa kukupigapiga kwa marungu hata kwa vijikosa vidogo jamani? Au nimekosea bibie?
Mambo ya kupigana hamna bwana....namaanisha ambae ataweza kusimamia kitu nielewe hata kama nilikua najaribu kua mbishi!!Sio ambae nikimwambie leo silali nyumbani anakubali tu kirahisi kwasababu hataki kunikasirisha!!!
 
Kwa ukorofi nilionao napenda nikutane na mtu kama mimi siyo mpole yani kila kitu anakubali maana inaboa. Haiwezekani kitu sijakosea nikawa mdogo au mpole. Nikikosea naomba msamaha na yeye akikosea aombe msamaha. Nukta
 
Binafsi mi naogopa kua na mtu wa aina hii kwenye mahusiano kwasababu najijua ni mkorofi kidogo kwahiyo naona kama ntamuonea sana.Iwe kwa makusudi au la najua mwisho wa siku ntaishia kujisikia vibaya na ntakua nimeshamuonea tayari!!Napenda mtu ambae nikikosea atanipa live na sio kwakunibembeleza maana wakati mwingine mtu akikwambia kitu kwa utaratibu ni rahisi kupotezea ila ukiona kakasirika kweli usikilizaji na uelewaji unaongezeka!!

Michango tafadhali......

Hi Lizzy.... I believe uko poa...Nice thread.

Nakubaliana nawe moja kwa moja na hio paragraph yako ya purple hapo juu. Among the qualities ninayopenda mwenza wangu awe nazo ni mtu anayejujua/jitambua na kujiamini (not over confident).... Because hivyo vitu vinacheza nafasi kubwa kwa a guy kuwa mpole au mkali. A guy ambae anajitambua na kujiamini yuko huru kufanya lolote juu yako cha haki maadamu tu awe atakupenda kwa dhati, na ninaposema lolote nina maana pale unapostahili kupongezwa wewe kama mwanamke wake atakupongeza (sio sifa za kijinga kila saa ooh lips zako sexy, mara miguu yako sijui imekaeje-ndio inaweza ikawa kweli but isiwe issue...). Na pale ambapo umekosea anakubadilikia kwa level tofauti tokana na ukubwa wa kosa ulofanya....

Nimesema hivyo sababu kama katika mahusiano the guy ndo ana an upper hand (sio ya kukubuhu) and he takes care of you kwa his level best kama anakupenda ni lazma a react kutokana na kitu ulichofanya, hivyo kuku treat kama partner wake.... Akiwa mpole kwa kila kitu ina maana kakuchulia kama mtoto akili yako na pia hakuna tension hata kidogo .... Lizzy personaly naweza boreka....
 
afazali leo umetuongelea wanaume wapole, yaani tunanyanyaswa kweli aisee.

Wewe si juzi tulienda kwa kalumanzila akupe dawa ya kukupunguzia ukali kwa mkeo???
Umejipaka ule unga wa mihogo leo mchana??? Maana msahaulifu kweli wewe
 
Upole asilia hauji kwa kuamua kichwani bali anakuwa nao mtu tangu anakua.
Wewe hata sasa huwezi tena kuwa mpole.
Binafsi sijazoea kufokea mtu, kumkasirikia mtu au kumpiga, especially kama nimfanyie haya mke (nikija kuoa). Why???

Nilivyokuwa nakua (nilivyokuwa primary school 1987 - 1993) nimepitia yote hayo.
So najua uchungu wake na jinsi mtu unavyokosa amani.
Najiuliza siku zote, hivi hakuna njia nyingine ya kumfundisha mtu na kumuelimisha kwamba hiki na kile hakitakiwi zaidi ya kumkaripia, kumpiga, kumfokea n.k???

Huo wa asilia ndo nnaouongelea!!
Kua tofauti na hivyo haina maana uwe unakaripia karipia tu watu ovyo na kufoka bila breki.....

Pole kwa kuonewa primary!!!
 
Nimeona hapo tu kwingine sijaona wala kusoma kabisa
 
Mimi naomba tu nikusalimua dawa ya Malaria.....habari yako mkuu?
dah! yaani hili bahati la leo kuliko kushinda lotto, hapa shwari tu Mrembo wangu, nimepoteza kilo kadhaa kwa kukumiss mawazoni mwangu, hope uko sawa na unanimiss pia, ukisema hukunimiss nagoma kukoga siku tatu mfululizo, pliz say u missed me.

bek to ze topik: wewe unapenda mpole kama mimi, au twanga twanga kama uporoto?
 
UNAJUA NYIE MABINTI MNA MAtatizo sana, mwanamke ukimpenda kupita kiasi na ukiwa mpole sana kwake anakuita *****,zobalangu n.k.na anaweza kukuletea bwana mwingine hivihiviiiiiiiii. ukiwa mkali kila cku unampa kichapo anapokosea,mnasema mnanyanyaswa, ukiwa haueleweki wakati mwingine unakuwa mkali sana wakati mwingine mpole, utasikia oooh, hili bwana langu hata silielewi, sijui lLINANIPENDA KWELI? WALA HALIELEWEKI, MIM "I PREFER TO BE UNPREDICTABLE"

Taituza usichanganye kati ya upole na uzezeta, a guy anaweza akawa mpole but ana msimamo, wewe kama mke unajua kabisa kua hapa nicheza vibaya sina langu hapa.... But napenda aspect yako ya kua Unpredictable ..... not good but good....
 
Ningekuwa bado ningemtafuta mpole lakini ningemuonea ile mbaya maana kwa ukorofi nilionao hatungewezana tunawezana na mkorofi mwenzangu.

Ila dah!!! Nashukuru kwa yuziful thread
 
Huo wa asilia ndo nnaouongelea!!
Kua tofauti na hivyo haina maana uwe unakaripia karipia tu watu ovyo na kufoka bila breki.....

Pole kwa kuonewa primary!!!

Basi ulikosea kuandika uliposema HUWEZI KUWA MPOLE coz ukisema hivi maana yake ni kitu cha kuamua, wakati ukweli ni kwamba HUNA UPOLE
 
Upole asilia hauji kwa kuamua kichwani bali anakuwa nao mtu tangu anakua.
Wewe hata sasa huwezi tena kuwa mpole.
Binafsi sijazoea kufokea mtu, kumkasirikia mtu au kumpiga, especially kama nimfanyie haya mke (nikija kuoa). Why???

Nilivyokuwa nakua (nilivyokuwa primary school 1987 - 1993) nimepitia yote hayo.
So najua uchungu wake na jinsi mtu unavyokosa amani.
Najiuliza siku zote, hivi hakuna njia nyingine ya kumfundisha mtu na kumuelimisha kwamba hiki na kile hakitakiwi zaidi ya kumkaripia, kumpiga, kumfokea n.k???

sasa CPU, hizo njia waweza kuwa umezitumia zote za upole lakini imeshindikana,
na mbaya zaidi unapopata mwanamke mkorofi kama LIZZY,
We unategemea nini,
Isitoshe wakati mwingine unajikuta baada ya kuoa tu na tabia imebadilika,
unakuwa mkali kama nini, kisa unakuta mke kakubadilisha kwa mitabia yake ya ukali uso kuwa na maana!!!!
 
Unajua Lizzy nasie huwa kama vile hatujielewi tunataka nini,ukipewa mpole unaweza muua na presha na majina kibao ,ukampatia ukipewa mkali naye vilio haviishi. Mie naona awe na vyote ili usiwe na cha kusema ukiburumbua anakuwasha sawasawa halafu mwezi mzima mpole huyo huwezi amini kama ni yeye alikuzabua.
 
Ningekuwa bado ningemtafuta mpole lakini ningemuonea ile mbaya maana kwa ukorofi nilionao hatungewezana tunawezana na mkorofi mwenzangu.

Ila dah!!! Nashukuru kwa yuziful thread

Kumbe na wewe mkurya . . .he he he he
Kajuna atakoma kulinga, mahali yote ya mazizi mawili aliyoitoa ataikumbuka
 
Hi Lizzy.... I believe uko poa...Nice thread.

Nakubaliana nawe moja kwa moja na hio paragraph yako ya purple hapo juu. Among the qualities ninayopenda mwenza wangu awe nazo ni mtu anayejujua/jitambua na kujiamini (not over confident).... Because hivyo vitu vinacheza nafasi kubwa kwa a guy kuwa mpole au mkali. A guy ambae anajitambua na kujiamini yuko huru kufanya lolote juu yako cha haki maadamu tu awe atakupenda kwa dhati, na ninaposema lolote nina maana pale unapostahili kupongezwa wewe kama mwanamke wake atakupongeza (sio sifa za kijinga kila saa ooh lips zako sexy, mara miguu yako sijui imekaeje-ndio inaweza ikawa kweli but isiwe issue...). Na pale ambapo umekosea anakubadilikia kwa level tofauti tokana na ukubwa wa kosa ulofanya....

Nimesema hivyo sababu kama katika mahusiano the guy ndo ana an upper hand (sio ya kukubuhu) and he takes care of you kwa his level best kama anakupenda ni lazma a react kutokana na kitu ulichofanya, hivyo kuku treat kama partner wake.... Akiwa mpole kwa kila kitu ina maana kakuchulia kama mtoto akili yako na pia hakuna tension hata kidogo .... Lizzy personaly naweza boreka....

Mi niko poa dear....hopefully na wewe uko shwari kabisa!!

Yani uliyoandika ndo haswaaa nnachomaanisha!!
Unakuta mtu hata ukikosea anaogopa kukwambia....kil akitu kinahusu kukufurahisha wewe..ukinuna kidogo tu hata kama wewe ndo umekosea basi anaanza kukubembeleza!!Ntaishia kuboreka mpaka mwisho!
 
Wewe si juzi tulienda kwa kalumanzila akupe dawa ya kukupunguzia ukali kwa mkeo???
Umejipaka ule unga wa mihogo leo mchana??? Maana msahaulifu kweli wewe
khaaaa! kweli wewe kibaka mzoefu! ulitokaje tokaje lile swagga la juzi baada ya kudakwa unaondoka na kiloba cha korosho?

bek to ze topik: refer to my two yuziful last posts
 
Back
Top Bottom