Upole!!

Kwa faida ya kina kaka embu wadada tujuzane mnapenda wapenzi/wenzi wenu waweje linapokuja swala la upole.Hapa siongelei ule upole wa muda kwamba ikitokea ugomvi mara moja moja anaweza kujishusha ...naongelea ule upole ambao ndio tabia yake.Yani kila kitu ye anakua mdogo tu....hata kama kosa sio lake anakua mdogo...hata kama anaonewa anakua mdogo!!

Binafsi mi naogopa kua na mtu wa aina hii kwenye mahusiano kwasababu najijua ni mkorofi kidogo kwahiyo naona kama ntamuonea sana.Iwe kwa makusudi au la najua mwisho wa siku ntaishia kujisikia vibaya na ntakua nimeshamuonea tayari!!Napenda mtu ambae nikikosea atanipa live na sio kwakunibembeleza maana wakati mwingine mtu akikwambia kitu kwa utaratibu ni rahisi kupotezea ila ukiona kakasirika kweli usikilizaji na uelewaji unaongezeka!!

Michango tafadhali......
Sina cha kuchangia nakusalimia tu Lizzy wa ngara mtoni!
 
Mi nina gf wangu mnyarwanda...yani ni mpole kushinda hata hayo maelezo ya mtoa mada!!siku za mwanzo za mahusiano nikimwangalia nilikuwa najisihi kulia-lia tu,coz ni decent,kapole hadi kanatia huruma...ingawa sasa hivi etlist ninampa maujanja. bt i real like her

Hongera mkaka ila usi take advantage ya upole wake huko mbeleni endelea kumpenda hivohivo.... na mwanamke mpole mwanaume mkali ni afadhali kuliko the opposite
 
Basi nimetubu mamii, usiende kwa kolokuwini

Kosa gani mimi nililokukosea wanitupa

Mrembo mwenye hadhi, pokea tena waraka
Usome na kuhifadhi, Yote nilioyoyandika
Nilipi lililokuudhi, Hebu niambie haraka

Fanya haraka muhibu, unipe hili hakika
Uneleze taratibu, Nipate kutoa shaka
Ni ipi hiyo sababu, Ilokupa kunepuka

Muhibu Lizzy nasema nawe, Hebu mwepushe shetani
Nyonda sinizuzuwe, Kanitia fedhehani
Toka kuniepuka wewe, Nimengia matesoni

Usione ni mzaha, mwenzio ni maradhini
Umenitia jeraha, La huba ndani kwa ndani
Naishi sina furaha, Kwa yondi lako Fulani

Kukurai si aibu, maadamu nakutaka
Na lau kama muhibu, Liko kosa limetuka
Basi mwana nimetubu, Msamaha nautaka

Kaditama tafadhali, wata kunihangiasha
Mwenzio kucha silali, Kwa huba huwa nakesha
Kumbuka na jambo hili, Kwako mahaba sijesha

dah! huu wimbo wa koffi olomide umeamua uutafsiri kwa kiswahili halaf utongozee? khaaa! hapa imekula kwa lizzy.
 
Kwa faida ya kina kaka embu wadada tujuzane mnapenda wapenzi/wenzi wenu waweje linapokuja swala la upole.Hapa siongelei ule upole wa muda kwamba ikitokea ugomvi mara moja moja anaweza kujishusha ...naongelea ule upole ambao ndio tabia yake.Yani kila kitu ye anakua mdogo tu....hata kama kosa sio lake anakua mdogo...hata kama anaonewa anakua mdogo!!

Binafsi mi naogopa kua na mtu wa aina hii kwenye mahusiano kwasababu najijua ni mkorofi kidogo kwahiyo naona kama ntamuonea sana.Iwe kwa makusudi au la najua mwisho wa siku ntaishia kujisikia vibaya na ntakua nimeshamuonea tayari!!Napenda mtu ambae nikikosea atanipa live na sio kwakunibembeleza maana wakati mwingine mtu akikwambia kitu kwa utaratibu ni rahisi kupotezea ila ukiona kakasirika kweli usikilizaji na uelewaji unaongezeka!!

Michango tafadhali......

Are you from Mara Region?
 
Huu wimbo uliimbwa na CPU sambamba na Asha D
ukiendelea kubisha nitalembea album zima la koffi hewani, bora ukuwe mpole tu kama sredi inavyosema. halaf mbona Keren Happuch simuoni tena aisee! nimeanza kupoteza nguvu za kutype hafla!
 
Back
Top Bottom