Upigaji Uyui: Waziri Mkuu ashangazwa kibanda cha Mlinzi VETA kujengwa kwa Tsh. milioni 11, aagiza waliyosimamia ujenzi kukamatwa

Bati miloni 7,
Rangi milioni 2
Tofali zake ni special sh milioni 1
Fundi milioni 1
 
Hii ni mnayoiona bwana main ni invisible ilijengewa kwenye meza ya Bar 🤣🤣
 
Style ya serikali kutoa kazi kwa contractors na kuchelewesha malipo wakati mwingine husababisha haya mambo.

unapewa tenda ya 6mil unalipwa mwakani December, au unaweza kudhulumiwa kabisa.

Serikali ihakikishe tendering zinafanyika kwa uwazi bila konakona, serikali iwe inalipa cash au advance au cash baada tu ya kazi kukamilika na kukaguliwa Ok ikatoka.

Wapigaji ndani ya serikali wanaosababisha urasimu ndio husababisha hizi overpricing ili watu walipee rushwa na mkandarasi apate chake, mkandarasi hana namna anaweka hela zaidi ili wahusika wampe kazi na pia wamrahisishie alipwe kwa wakati.
 
Incompetency na Wizi ni shida kuu katika nchi hii, watu Incompetency wameshindwa kuset proper system kuondoa urasimu na ujinga kwenye mifumo, Wezi nao hutengeneza njia za upigaji kila siku kupitia mifumo dhaifu na pumbavu. Tafrani kila siku.
 
WALIOSIMAMIA UJENZI WA VETA UYUI WAKAMATWE- MAJALIWA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) Mkoa wa Tabora, Musa Chaulo kuwakamata watu wote wanaohusika na usimamizi wa ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) wilaya ya Uyui mkoani Tabora kwa tuhuma za ubadhilifu wa fedha za mradi huo.

Amechukua hatua hiyo baada ya kukagua mradi huo na kuonesha kutoridhika na gharama za ujenzi wa baadhi ya majengo ikiwemo kibanda cha mlinzi ambacho ujenzi wake umegharimu shilingi milioni 11. “Sitamvumilia yeyote atakayemuhujumu Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, watafutwe na wachukuliwe hatua.”

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Alhamisi, Septemba 8, 2022) baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa chuo cha VETA wilaya ya Uyui mkoani Tabora ambapo amesema hajaridhishwa na ujenzi wa chuo hicho ambacho majengo yake yanejengwa kwa gharama kubwa tofauti na uhalisia kwa kutumia mfumo wa nguvu kazi ya ndani (force account).

Mbali na ujenzi wa kibanda cha mlinzi, pia Waziri Mkuu ameonesha kutoridhishwa na ujenzi wa nyumba za watumishi chuoni hapo ambapo nyumba moja yenye uwezo wa kuchukua familia mbili inajengwa kwa gharama ya shilingi milioni 114 na tayari wameshatumia zaidi ya shilingi milioni 70 na bado haijakamilika.

“Nyumba moja yenye uwezo wa kuchukua familia tatu Wizara ya Afya inajenga kwa shilingi milioni 90 na Ofisi ya Rais (TAMISEMI) wanajenga nyumba za walimu zenye uwezo wa kuchukua familia mbili kwa gharama ya shilingi milioni 57 na wanajenga kwa mfumo wa force account kama mnavyojenga hapa, hii haikubaliki.”

Kutokana na kutoridhishwa na ujenzi wa chuo hicho unaosimamiwa na VETA, Mheshimiwa Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Burian asimamie ujenzi wa chuo hicho ili uweze kukamilika kwa wakati. “Mkuu wa mkoa simamia vizuri ujenzi wa chuo hiki, tunataka ukamilike kwa wakati.”
 
Attachments

  • IMG-20220908-WA0156(1).jpg
    IMG-20220908-WA0156(1).jpg
    76.6 KB · Views: 2
  • IMG-20220908-WA0155(1).jpg
    IMG-20220908-WA0155(1).jpg
    108 KB · Views: 1
Pesa zipo za kuchota tu tena siyo za kuhangaikia kama zamani. Watu wanakula maisha tu. Nchi hii ni ya ajabu sana.
Nchi inajengwa kwa tozo. Sasa hivi Internet ni anasa
Incompetency na Wizi ni shida kuu katika nchi hii, watu Incompetency wameshindwa kuset proper system kuondoa urasimu na ujinga kwenye mifumo, Wezi nao hutengeneza njia za upigaji kila siku kupitia mifumo dhaifu na pumbavu. Tafrani kila siku.
 
Kuna wakati ni vigumu sana kufananisha ujenzi kwa kutumia force account kuoka eneo moja na lingine.

Kuna baadhi ya maeneo wananchi wanajitolea nguvu kazi na kukusanya mchanga pamoja na mawe.Maeneo mengine kila kitu unanunua kuanzia mchanga.
 
Style ya serikali kutoa kazi kwa contractors na kuchelewesha malipo wakati mwingine husababisha haya mambo.

unapewa tenda ya 6mil unalipwa mwakani December, au unaweza kudhulumiwa kabisa.

Serikali ihakikishe tendering zinafanyika kwa uwazi bila konakona, serikali iwe inalipa cash au advance au cash baada tu ya kazi kukamilika na kukaguliwa Ok ikatoka.

Wapigaji ndani ya serikali wanaosababisha urasimu ndio husababisha hizi overpricing ili watu walipee rushwa na mkandarasi apate chake, mkandarasi hana namna anaweka hela zaidi ili wahusika wampe kazi na pia wamrahisishie alipwe kwa wakati.

Hilo la kudhulumiwa liko sana. Wanakukopa wanachelewa kukulipa miaka kadhaa wakijua umefilisika na kampuni haiko wanakuja wanakuambia wanataka kukulipa ulete leseni ya sasa na address ya ofisi wakati wanajua fika hunavyo.. Serikali inanjia nyingi za kudhulumu basi tu.
 
Back
Top Bottom