Bashungwa aongoza harambee ujenzi wa kituo cha Masista, Milioni 237 yakusanywa

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944

BASHUNGWA AONGOZA HARAMBEE UJENZI WA KITUO CHA MASISTA, MILIONI 237 YAKUSANYWA.

Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ameongoza harambee ya kuchangia ujenzi wa Kituo cha huduma cha Masista wa Shirika la Dada Wadogo kinachotarajiwa kujengwa eneo la Bagamoyo ambapo jumla ya kiasi cha Shilingi Milioni 237 imekusanywa.

Harambee hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam tarehe 5 Januari, 2024 katika ukumbi wa Marantal Msimbazi Centre ambapo pamoja na mambo mengine lengo kuu lilikuwa ni kukusanya Shilingi Milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho.

Waziri Bashungwa amelipongeza Shirika hilo kwa kazi kubwa wanayoifanya na kuwatia moyo kuwa ataendelea kushirikiana nao katika zoezi hilo la Ujenzi wa Kituo hicho.

Viongozi Wakuu waliochangia katika Harambee hiyo ni pamoja nana Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista J. Mhagama, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila pamoja na Viongozi wengine wa Serikali.

Aidha, Waziri Bashugwa kwa kushirikiana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Mhe. Jenista Mhagama wameeahidi kuendelea kushirikiana bega kwa bega na Shirika hilo katika ujenzi wa kituo hicho hadi kitakapokamilika

Akisoma Risala, Kiongozi wa Mradi kutoka Shirika la Dada Wadogo Mtakatifu Francisko (Little Sister of St. Francisko), Sista Bahati Leah ameeleza kuwa Shirika hilo kwa upande wa Tanzania wanafanya utume katika majimbo manne ikiwemo Jimbo kuu la Arusha, Same, Shinyanga, Morogoro naBagamoyo.

Ameeleza kuwa Shirika hilo linatoa huduma mbalimbali zikiwemo huduma za kiroho, kimwili, kusaidia walemavu, masikini, vipofu, wazee, wagonjwa na watoto walioko kwenye mazingira hatarishi.

Naye, Mhasibu Mkuu kutoka Taasisi za Marian Bagamoyo, Padre Felix Jabu, ametoa ahadi kwa niaba ya Taasisi hiyo kuwa itatoa tofali zote zitakazotumika katika ujenzi wa Kituo hicho, Mchanga, Kokoto pamoja na mafundi ujenzi wa kituo hicho.

Kwa Upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Ujenzi wa Kituo hicho Bw. Benard Kileghe amesema kuwa zoezi hilo lilianza mwezi wa 11, 2023 likiwa na lengo la kupata kituo kikubwa cha Huduma cha Bagamoyo kitachotoa huduma kwa wahitaji na wahudumu wa Shirika hilio.

Miongoni mwa walioshiriki harambee hiyo ni pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Jonas Mpogolo, Diwani kata Nyabiyonza kutoka Karagwe, Thomas Rwentabaza pamoja na Kwaya ya Makuburi.

Shirika la Dada Wadogo Mtakatifu Francisko ni Shirika la Jimbo Katoliki ambalo lilianzishwa mwaka 1923 huku makao yake makuu yakiwa nchini Uganda na mpaka sasa lina wafuasi 800 wanaofanya utume katila nchi nne Uganda, Kenya, Tanzania na Marekani (USA).
 

Attachments

  • GDONF3CXwAAdXju.jpg
    GDONF3CXwAAdXju.jpg
    211.6 KB · Views: 2
  • GDONF3BW4AAVg-8.jpg
    GDONF3BW4AAVg-8.jpg
    222.1 KB · Views: 3
  • GDONF2-XEAAkdld.jpg
    GDONF2-XEAAkdld.jpg
    249.6 KB · Views: 1
  • GDONF3AXwAAoeBf.jpg
    GDONF3AXwAAoeBf.jpg
    306.8 KB · Views: 2
  • GDONLHsW0AIcSrA.jpg
    GDONLHsW0AIcSrA.jpg
    299.8 KB · Views: 2
  • GDONLHxX0AAfRFt.jpg
    GDONLHxX0AAfRFt.jpg
    227.2 KB · Views: 2
  • GDONLHnWUAEk9ao.jpg
    GDONLHnWUAEk9ao.jpg
    171.2 KB · Views: 3
  • GDONLHkW4AAGBlT.jpg
    GDONLHkW4AAGBlT.jpg
    229.9 KB · Views: 3
Nasikia "eti" anaandaliwa kuwa moja ya top 3 za nchi, ila namuona siku hizi "gari limewaka", anachapa kazi sana wizara ya ujenzi, na ni kama watu wanaanza kumuelewa. Akimaliza na daraja la jangwani, njia nne mwanza, superhighway Dar-Moro, daraja la mto simiyu na kuisuka upya lami ya mwanza shinyanga, na nyanguge musoma, CV yake itatoboa dari.

Hata kitendo cha Fatma Mwassa kumfanya mgeni rasmi kwenye shughuli ya kuwakumbusha wahaya kwamba kwao wameacha mapagale, aliongea kwa busara sana na utulivu, kale ka woga kameisha. Mwijage ni kiongozi wa wabunge wa mkoa wa Kagera, lakini heshima alipewa Bashungwa.

Anapenda sana wapiga kura wake vijijini, kwa hiyo huyu ni mtu wa kukaa na watu wa kawaida, na nilimuona kwenye saluni moja ya kijijini sana akinyoa nywele, na pia alimtembelea mzee mmoja mwenye mashine ya kusaga akamsalimia. Bila kusahau, alishiriki katika omulamba.
 
Nasikia "eti" anaandaliwa kuwa moja ya top 3 za nchi, ila namuona siku hizi "gari limewaka", anachapa kazi sana wizara ya ujenzi, na ni kama watu wanaanza kumuelewa. Akimaliza na daraja la jangwani, njia nne mwanza, superhighway Dar-Moro, daraja la mto simiyu na kuisuka upya lami ya mwanza shinyanga, na nyanguge musoma, CV yake itatoboa dari.

Hata kitendo cha Fatma Mwassa kumfanya mgeni rasmi kwenye shughuli ya kuwakumbusha wahaya kwamba kwao wameacha mapagale, aliongea kwa busara sana na utulivu, kale ka woga kameisha.
Na wewe Nembe unaandaliwa kuwa top 3 CHAWA?
 
Back
Top Bottom