Uongozi UDSM wasema hapana kwa Zitto Kuunguruma

Huyo mkuu wa chuo atakuwa mjinga kweli kama ataona njia ya kuzuia hoja ya Zitto ni kumzuia asiongee. Hoja hujibiwa kwa hoja, waandae hoja badala ya kutumia manguvu.

Ningelikuwa mimi ningempa Zitto uwanja wowote anaoutaka. Wanaofuatilia haya mapambano ya fikra wanajua wazi Zitto akiachiwa atambe anavyotaka, itafika mahali baadhi ya chenga zake hazitakuwa na maana tena, lakini ukizuia wananchi wasimsikie ndivyo watakavyokuwa na hamu ya kumsikia.
 
siwezi kusema kwa hakikika kama DARUSO,RAAWU na UDASA walikuwa wanamuunga MKANDALA mkono moja kwa moja. ila ukweli ni kuwa katika hili kila mmoja na hasa wahadhiri walikuwa wana maoni yao huku wengine wakipinga na wengine wakimsupport.

Hili linahitaji utafiti wa hal ya juu mno.....
 
Endeleeni kutuelimisha politics za Mlimani ... sikujua kama uteuzi wa VC huwa umegubikwa na politics na dirty games!
 
kwa mujibu wa kiongozi wa juu wa DARUSO,ZITTO Amekataliwa kuingia mlimani..
utabiri umetimia,katiba inavunjwa waziwazi,angalia jinsi kijana wa sekondari ya pius msekwa anavyofuatwa na INTELIGENSIA!...MWALIMU FUFUKA UONE MADUDU YA ULIOWAKATAA,
hii itakuwa ni AMRI ya ndanda kosovo tu..si amerudi dar?
kuna kampeni itaanza karibuni ya kuwajibu wapinzani,stay tunned..
 
Nahisi hapo wamezidi uchochea moto wa Zitto! Sidhani wana sababu zipi za msingi za kumzuia? Inatisha na kusikitisha!
 
kitakachofuata ..waliondaa public talk watafuatwa na USALAMA,
ndg mkandara mshauri muungwana afute ibara ya 18 na 22 ili muwe mnafanya mambo yenu na watu wasitoe maoni,
nawapa moyo vijana wa DUPSA wasivunjike moyo!
aluta continue..endeleeni kuwazomea na msiwaombee hawa wezi
 
wanafunzi wameshasambaa maeneo ya theatre..taarifa nilizopewa ,zito alifanikiwa kuingia ndani ila uongozi wa chuo ukawatakalia kuzungumza na wanafunzi,
kweli tutafika?sasa tangu lini VC Akampangia mwanachuo mambo ya kuelezwa?
mie sijui tunakoenda-
 
Ndo maana inabidi katiba ibadilishwe, Raisi kapewa mamlaka makubwa mno ya kuteua teua watendaji! Hapa Mkandala/uongozi wa chuo unalinda tu vitumbua vyao! Yaani sasa kila mtendaji anakuwa mwana siasa kwa vile nafasi kateuliwa?? Inaboa sana!
 
Hii inatia mashaka sana tu,

Wakati ule tulikuwa tunasikia akina Mtikila kuwa walitemebelea sana pale Nkrumah Hall, iweje wakati huu wengine wakataliwe. Again, haya ndio tunaita makosa ya kiufundi kwa upande wa serikali................na hii inadhihirisha kuwa Zitto ana hoja inayochoma, na serikali wamekosa mafundi wa kuwajibia HOJA.

Zitto ni kama jipu linalowasumbua CCM, na CCM wanashindwa kuelewa ya kwamba
Dawa ya JIPU (Zitto) liache mpaka liive halafu litumbue halafu paka dawa, Ukilizuia wakati changa litaibuka sehemu nyingine ambayo yaweza kuwa mbaya zaidi....im afraid!!

Kwani ile Rev Square haipo tena siku hizi..............au ile Rev Square ni kwa ajili ya wanafunzi tu?
 
Yah, Rev, ni ya wanafunzi,

Ila hapa mi naona wamezidi likoroga, hata wale ambao walikuwa hawana mpango wa kumsikiliza Zitto ndo kwaaaanza wameawaamsha, subiri tu time will tell.
 
Wakuu heshima mbele, ninajaribu ku-read between the lines sipati the juice bado on this ishu,

kwa hiyo labda ningeomba more facts, kuanzia kibali cha Mbunge kuruhusiwa kuongea hapo chuoni, na sheria zote zinazohusiana na suala zima la kiongozi yoyote kuruhusiwa na uongozi wa shule kuongea hapo shuleni,

It is a high time sasa kwenye JF tukufu tuache songi songi, na tuweke facts kwanza, ili tuzichambue ipasavyo,

However, shukrani kwa wale mnaojitahidi kutuhabarisha na yanyojiri huko shuleni!
 
Habari zilizo nifikia muda huu zinasema Ukumbi pale Chuo ujemaa pomoni na watu wana ngoja kusikia maneno mazito toka kwa Ziito. Uongozi wa Chuo umekaa chonjo unasema hapana Zitto hawezi kuunguruma pale Mlimani maana Serikali haitapenda. Hizi ndiyo habari zinazo jiri na sijui mwisho wake ni upi . Natoka naelekea kunako maeneo nikiwa na nazidi nitawauma sikio. Ila kwa sasa huu ndiyo uhalisia wenyewe.

Wanafunzi ni wengi sana ila Zitto katakiwa kutogusa maeneo hayo ambayo ni makao ya wasomi wetu .

Maskini Tanzania! kadri wanavojaribu kwa kila hali kumnyima huyu jamaa haki yake ya kikatiba ndivyo wanavyozidi kumjengea umaarufu. Tatizo ni kwamba CCM wameshachelewa na jamaa kishapata umaarufu nchi nzima kwa kuzungumza yale ambayo yanawakera Watanzania kila kukicha lakini CCM na siri kali imeyafumbia macho.
Mungi ibariki Tanzania.
 
Wakuu heshima mbele, ninajaribu ku-read between the lines sipati the juice bado on this ishu,

kwa hiyo labda ningeomba more facts, kuanzia kibali cha Mbunge kuruhusiwa kuongea hapo chuoni, na sheria zote zinazohusiana na suala zima la kiongozi yoyote kuruhusiwa na uongozi wa shule kuongea hapo shuleni,

It is a high time sasa kwenye JF tukufu tuache songi songi, na tuweke facts kwanza, ili tuzichambue ipasavyo,

However, shukrani kwa wale mnaojitahidi kutuhabarisha na yanyojiri huko shuleni!

mkuu issue ni kuwa vijana wapale mlimani waliandaa public talk kuzungumzia nafasi ya vijana wa elimu ya juu katika taifa letu tukufu la tanzania. lakini katika hali yakushangaza uongozi wa chuo wakakwamisha kufanyika kwa majadala huo eti kisa zitto atakuwa mmoja wa public speakers. hapa alikuwa amealikwa kama mtanzania mwingine na hata kama hakuwa amealikwa alikuwa na uhuru wa kuhudhuria mjadala huu wa wazi pale mlimani. kwa taarifa ni kuwa amesha wahi kuhudhuria midahalo kadhaa mingine bila hata mwaliko na wala hapakuwahi kuwa na tatizo. the only difference na wakati huu ni kuwa amekuwa maarufu kuliko mwanasiasa mwingine leo. na ni wakati ambao serikali ina kazi ngumu ya kujibu hoja juu ya ufisadi. so ndo watu wanahoji ni kwa nini uongozi wa chuo ambao ni maproffesa wanakubali kutumika kwa mabo ya siasa huku wakiwanyima wanafunzi haki yao ya kikatiba ya kupata habari na kukutanika kama katiba inavyotaka.

watu wanahoji ni kwa nini zitto azuiwe? nilisha eleza kwenye post zangu zilizo pita jinsi walivyo fanyiwa zengwe kunyimwa ukumbi! katika mazingira haya ndio watu wanahoji kama kilicho fanyika ni sahihi na nini impact yake kwenye institution na chuo kikongwe nchini?

nadhani hapo tupo wote mkuu ES... hizo ndo juice zenyewe kazi kwako
 
Hata Columbia University Wameweza kumwalika Mahmoud Ahmadinejad, kiongozi ambaye wengi katika hicho chuo na nchi wanamwona kama kiongozi wa magaidi Mashariki ya Kati!!... leo hii Tanzania mambo sivyo kabisa. Shime shime kwa wakuu wa vyuo kuwa huru na wasio fungamana na pande zozote kidini, kisiasa, kijamii n.k. katika nchi yetu!

SteveD.
 
lakini katika hali yakushangaza uongozi wa chuo wakakwamisha kufanyika kwa majadala huo eti kisa zitto atakuwa mmoja wa public speakers. hapa alikuwa amealikwa kama mtanzania mwingine na hata kama hakuwa amealikwa alikuwa na uhuru wa kuhudhuria mjadala huu wa wazi pale mlimani

Nimekusikia mkuu, kwa kusoma hii ishu mwanzoni nilifikiri the juice ni Zitto, mbunge kualikwa huko shule kutoa speech, lakini sasa ninaona ni kuwa hakuwa the main speaker ila just a guest,

sasa kama ni kweli, amekataliwa kuhudhuria kama guest speaker tu!, then something is not right ila tuendelee kufahamishana yanayojiri zaidi huko hku tukiendelea kuifuatilia hii ishu kwa ukaribu sasa!
 
Zitto akatazwa kuongea UDSM

Wanafunzi wameandamana

habari zaidi zinakuja.. stay tunned
 
Zitto akatazwa kuongea UDSM

Wanafunzi wameandamana

habari zaidi zinakuja.. stay tunned

mimi nimepata nafasi ya kuona news hiyo kupitia Television ya Taifa, wasiwasi wa hawa jamaa ni kuwa anaenda na issue ya Buzwagi, kumbe ana mwaliko wa wanafunzi. Makamu Mkuu wa Chuo anasema hajaona huo mwaliko, mwenye kufahamu tunaomba details katika hili.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom