Jamani! Siku hizi imekuwa ni kawaida sana kwa mwanamume na mwanamke(ambao wanategemea kuoana) kuishi pamoja kama mke na mume. Si ajabu ukakuta mwanamke anakaa mkoa X lakini kila weekend au likizo anaenda mkoa Y eti kumsalimia"mchumba wake" ambaye kwa muktadha wa post hii na maadili ya jamii zetu na imani zetu za kidini huyo si mchumba bali ni MZINZI MWENZAKE au HAWARA YAKE. Na mbaya zaidi unakuta wanaishi maisha ya uzinifu kwa muda mrefu then wanaamua eti kubariki ndoa.
Viongozi wetu wa dini nao wanakubali kufungisha ndoa za wazinzi hawa bila aibu. Na si ajabu siku hizi kuona wazinzi wawili(mwanamke na mwanamume) wakiwa wameongozana wakienda ktk ibada iwe kanisani au msikitini. Sijui wanaenda kuabudu au kumkejeli muumba wao.
Kama wewe halijakutokea inawezekana umeliona kwa rafiki, ndugu au hata kwa adui yako.
NINI MAONI YAKO: NI KUMONG'ONYOKA KWA MAADILI AU NI MAENDELEO?