Ununuzi wa ndege 6 ulipangwa bajeti ipi?

"Bwana yule" anaweza kuona ni sifa kuagiza na kulipia ndege ziletwe Tanzania bila kushirikisha wadau.

Lakini kuna siku mambo haya yatamgeukia, watu hawatajali kama alikuwa anayafanya kwa nia njema au mbaya.

Yanaweza kuzuka maneno kuwa alikuwa anachukua 10% ili kuruhusu manunuzi haya.

"Bwana yule" aache kujisahau na kufikiri kuwa pesa za walipa kodi kuwa ni zake binafsi!

Bunge la bajeti ni muhimu sana kwenye "issue" kama hizi!...
 
Jana wakati tunaadhimisha miaka 55 ya uhuru wa iliyokuwa Jamhuri ya Tanganyika (sasa Tanzania), Mhe rais alisema mpaka sasa tumeishanunua ndege sita za kubebea abiria.

Naomba kujua wakati wa bunge la bajeti pesa za kununua ndege zilikuwa zimepangwa kiasi gani na kupitia wizara gani? Je, mpaka sasa ni kiasi gani kimetumika kununua ndege hizo?

Na kama bunge halikupanga kununua ndege hizo, Rais haoni kuwa anaingilia mhimili mwingine ambao kimsingi ndio wenye mamlaka ya kupanga bajeti na matumizi yote ya serikali.

Je, tunahitaji bunge?
Hah ha ha ha haaaaaaa

Hii nchi kwasasa ni kituuuukoo
 
Huwa unatabia ya kusoma bajeti?? au unaona ni maajabu kwakuwa ulikuwa umezoea chini ya uongozi wa mafisadi vitu vingi vinapigwa juu kwa juuu halafu tunaambiwa baget haitoshi?? Hizo ndege tanzania inanunua kwa cash kama mkakati wa kufikia uchumi wa kati nduguuu. Halafu ndugu huu ni utawala uliotukuka, hakuna mafisadi papa tena, waliokuwa mafisadi walishatimukia kule kwenye kile chama kinachowaoshaa. Sisi huku tunasema HAPA KAZI TU.
... Umeelewa mada? Nani kaidhinisha manunuzi hata kama ni pay cash and carry...
 
ujinga kununua ndege badala ya kujenga barabara

Kwani barabara hazijengwi? saizi tunatoka Mbinga na yutong asbh sa 10 jion tupo Mtwara, Tunatoka Mbeya asbh Saa 10 jion tupo Mpanda, tunatoka Kigoma asbh jion tupo Sumbawanga. Hizi route nilizokutajia miaka miwili iliyopita ilikua unatumia siku 2 mpaka 3
 
nivema saaana kufata taratibu,sheria na kanuni ktk uongozi. Mkikubaliana wote wakati WA matatizo mtasolv wote. Unaweza ukanunua midege mikubwa lakini biashara ikaanguka na kuingia hasara. Watu watahoji kwanini hukutupa maji tulokwambia,afya tulolilia nk. ukajiamulia kufanya ulichotaka mwishowe unatwikwa lawama na unaangushwa kisiasa. Twendeni pamoja tusitanguliwe nabaadhi Kisha wengi tufate bila kukubaliana njia niipi. Mungu ibariki Tz
 
Yaani nchi ikinunua ndege kwa fedha taslimu ndiyo inafikia uchumi wa kati?

Huwa unatabia ya kusoma bajeti?? au unaona ni maajabu kwakuwa ulikuwa umezoea chini ya uongozi wa mafisadi vitu vingi vinapigwa juu kwa juuu halafu tunaambiwa baget haitoshi?? Hizo ndege tanzania inanunua kwa cash kama mkakati wa kufikia uchumi wa kati nduguuu. Halafu ndugu huu ni utawala uliotukuka, hakuna mafisadi papa tena, waliokuwa mafisadi walishatimukia kule kwenye kile chama kinachowaoshaa. Sisi huku tunasema HAPA KAZI TU.
 
Unafahamu dynamics za kuendesha shirika la ndege? Unafahamu kwa nini Rwanda ambayo umeitaja haijanunua Dreamliner ingawa wanao uwezo huo? Unafahamu vigezo gani vinatumika kuamua kununua aina fulani ya ndege badala ya aina nyingine? Unafahamu mpaka ndege uione inapita angani ni mambo gani magumu yamefanikiwa kuifikisha angani? Unafahamu ili shirika la ndege liweze kupunguza gharama za uendeshaji linatakiwa lifanye nini? Unafahamu inaweza kuchukua muda gani kujenga jina na taswira ya shirika la ndege mpaka livutie biashara?
Unafahamu kuwa kununua ndege haimaanishi kufufuka kwa shirika? Unaujua muda ambao Air Tanzania italazimika kufanya kazi kwa hasara na kama itaweza kuvuka kipindi hicho na kuanza kufanya kazi kwa faida? South African Airways inafanya kazi kwa hasara na kinacholifanya shirika liendelee kuwepo ni ruzuku za serikali; Kenya Airways wanapambana na hasara wakati ambapo RwandAir wanakwenda vizuri na wanaongeza ndege kubwa; kuna mafundisho gani katika mashirika haya matatu ambayo ni muhimu kuzingatia?
DAHACO ilishauawa miaka mingi na badala yake ipo Swissport; kuna hatari gani za msingi kwa Air Tanzania katika kipengele hiki? Mkurugenzi Mkuu mpya wa Air Tanzania ana uzoefu wa kuwa "regulator" yaani msimamizi wa masuala ya anga lakini siyo "operator" yaani mwendeshaji wa shirika la ndege. Shirika la ndege ni biashara si taasisi kama EWURA au TCRA; je, imethibitishwa wapi kwamba ana uwezo wa kiwango cha wakurugenzi wa mashirika mengine duniani ili tuwe na japo na uhakika kwamba Air Tanzania itasimama imara na kufanikiwa?
Haya ni baadhi tu ya maswali ambayo baadhi yetu tunajiuliza na hatujapata majibu bado ndiyo maana hatushangilii kirahisi ujio wa hizi ndege.
ndege wamelipa malipo ya awali....na bunge lilipitisha bilioni 500..kwa ajiri ya atcl..so wamelipa malipo ya awali...ila ukweli ni kwamba kwa BOEING dreamline..magu katisha ikitua bongo sipati picha,,,maana hata rwanda walileta 737next gen,,,ila wakatamba je sisi wa 787...hongera magu..ipo siku utakumbukwa
 
Huwa unatabia ya kusoma bajeti?? au unaona ni maajabu kwakuwa ulikuwa umezoea chini ya uongozi wa mafisadi vitu vingi vinapigwa juu kwa juuu halafu tunaambiwa baget haitoshi?? Hizo ndege tanzania inanunua kwa cash kama mkakati wa kufikia uchumi wa kati nduguuu. Halafu ndugu huu ni utawala uliotukuka, hakuna mafisadi papa tena, waliokuwa mafisadi walishatimukia kule kwenye kile chama kinachowaoshaa. Sisi huku tunasema HAPA KAZI TU.
HAUJAJIBU SWALI LAKE....... umeongea ushabiki wako wa serikali hii..... jibu swali kwanza...!!!!!
 
ndege wamelipa malipo ya awali....na bunge lilipitisha bilioni 500..kwa ajiri ya atcl..so wamelipa malipo ya awali...ila ukweli ni kwamba kwa BOEING dreamline..magu katisha ikitua bongo sipati picha,,,maana hata rwanda walileta 737next gen,,,ila wakatamba je sisi wa 787...hongera magu..ipo siku utakumbukwa
Bunge ilipitisha kwenye kikao gani...????
 
Molembe
TZ ni nchi ya hovyo hovyo sana wala usijihangaishe ndugu yangu!Rais anajichotea tu Mabilion kwa vimemo BOT kwa jinsi anavyo penda yy na marafiki zake!
Sioni hata haja ya kwa nn Bunge la Bajeti linakaa!Nchi ambayo Rais anatumia mabilion ya wahanga na sisi tupo kimywa tu hata upinzani inathibitisha kabisa kuwa Rais wa Tanzania anaongoza watu wenye mtindio wa Ubongo
 
Back
Top Bottom