Hayati Magufuli kwanini alificha jalada la ununuzi wa ndege?

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
49,242
103,943
Sifa kubwa ya madikteta ni usiri na kuficha mambo ya umma kama masuala binafsi.

Ndivyo ilivyokuwa kwa Mwendazake wakati anafanya mpango wa kununua ndege.

Umewahi kujiuliza kwanini mamlaka ya mdhibiti na mkaguzi mkuu haikuwahi kutoa maoni yao juu ya ununuzi wa ndege?

Taarifa zilizopo ni kwamba kulikuwa na usiri mkubwa juu ya nyaraka za manunuzi.

Nyaraka alikuwa anatembea nazo Magufuli mwenyewe. Hakutaka umma ujue chochote kama vile zilikuwa ndege binafsi.

Mdhibiti alipoomba kuona chochote walimwambia aende kwa Rais. Hii ilikuwa tafsida tu ila ilimaanishwa endelea na mambo mengine. Kitaalamu tunaita Intimidation Threat.

Mpaka anafariki hakukuwahi kujibiwa kwanini kulikuwa na usiri kwenye mchakato.

Je, alipiga cha juu? Mteteeni basi na hili. Msiseme alishaondoka asisemwe ile sio mali binafsi ni ya umma.
 
FB_IMG_1679375835512.jpg
 
amewanunulia ndege, endesheni shirika sasa lilete faida na liwe na manufaa kwa watanzania.

Shirika lilikuwa na ndege moja tu choka mbaya na mamia ya wafanyakazi wakilipwa mishahara ya bure na wengine hewa.

Kawanunulia midege na kuajiri watendaji sambamba na idadi yan ndege.
 
Same old story everyday, hebu tutajie mkataba mmoja tu uliowahi kuwekwa wazi na serikali ya CCM tukauona?

Ukishindwa kufanya hivyo, tujibu; kwanini tusiamini nyie wapinzani maslahi mnatumiwa na walamba asali ili kufanikisha malengo yao?
 
Aaah.. Wewe si unataka upewe usome?.

Kama hiyo bei hujui kwa nini unang'ang'ania ndege ? .

Kiluuu
Narudia tena aliyeweka hilo takes hakua mjinga. Teteeni panapofaa. Penye walakini nyoosheni mikono mkemee. Halafu kwa upumbavu unafikiri biashara ya kimataifa unafanya kwa sport money. Kuna mbinu za kulipia baada ya muda Fulani.

Ujinga ni kufikiri alikua mtakatifu. Sijui yupo wapi ila alikosa mengi kuliko alikopatia. Fungueni macho. Kama mna hamu nchi ifike mahali lazima mjenge taasisi yenye misingi imara. Ukabila ulijaribu kuja ila haukupenya. Unajua kwa nini?

Kwa sababu Nyerere kwenye udhaifu wake alituunganisha kwa misingi ya kitaifa. Hiyo aloyevunja Sheria ndio mnamsifia. Asiyetaka kukaguliwa. Unafanya kazi na watu mia tano ikulu halafu mafaili hutaki kuyachunguza utafikiri unajua kila kitu.

Hata Yesu aliyeweza kila kitu alifundisha watu kumi na mbili wa kurithi kazi yake aliondoka duniani. Wale kumi na mbili Leo ni mabilioni ya watu.

Ukitaka kufika mapema kimbia mwenyewe ila ukitaka kufika point b ili umkabidhi kijiti mwingine kimbia na watu. Kwa njia hiyo utapata wa kumpa kijiti ukichoka.
 
Back
Top Bottom