Bunge laazimia Serikali inunue ndege nyingine kwa ajili ya kuhudumia viongozi

Ze Heby

JF-Expert Member
Jun 22, 2011
5,251
5,316

Bunge la Tanzania limeazimia kuwa Serikali iangalie umuhimu wa kununua ndege nyingine mpya kwa ajili ya kuwahudumia viongozi wakuu wa kitaifa.

Taarifa hiyo imetolewa leo Februari 13, 2024 na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria Joseph Mhagama, ambaye ameeleza kuwa nia ya azimio hilo inatokana na Wakala wa Ndege za Serikali kushindwa kuwahudumia kwa wakati viongozi wakuu pale zinapotokea safari kwa wakati mmoja.

Kwa mujibu wa Mhagama kamati yake imebaini kuwa kwa sasa kuna ndege tatu zinazowahudumia viongozi wa Serikali. Ndege moja inamhudumia Rais wa Tanzania, ndege nyingine mbili zinawahudumia Makamu wa Rais, Rais wa Zanzibar, Waziri Mkuu, Makamu wa Kwanza na Wa Pili wa Rais wa Zanzibar na viongozi wengine wa kitaifa.

“Hali hii husababisha Wakala [wa Ndege za Serikali] kutekeleza jukumu la kuwahudumia viongozi kwa kuchelewa pindi zinapotokea safari za viongozi wote kwa wakati mmoja,” Mhagama anasema.

“Kwa hiyo basi Bunge linaazimia kwamba Serikali ione umuhimu wa kufanya ununuzi wa ndege nyingine ili kuboresha utoaji huduma za usafiri wa anga kwa viongozi wakuu wa kitaifa".

Source: The Chanzo

Nini maoni yako kuhusu azimio hili?
 
Bunge la Tanzania limeazimia kuwa Serikali iangalie umuhimu wa kununua ndege nyingine mpya kwa ajili ya kuwahudumia viongozi wakuu wa kitaifa.

Taarifa hiyo imetolewa leo Februari 13, 2024 na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria Joseph Mhagama, ambaye ameeleza kuwa nia ya azimio hilo inatokana na Wakala wa Ndege za Serikali kushindwa kuwahudumia kwa wakati viongozi wakuu pale zinapotokea safari kwa wakati mmoja.

Kwa mujibu wa Mhagama kamati yake imebaini kuwa kwa sasa kuna ndege tatu zinazowahudumia viongozi wa Serikali.

Ndege moja inamhudumia Rais wa Tanzania, ndege nyingine mbili zinawahudumia Makamu wa Rais, Rais wa Zanzibar, Waziri Mkuu, Makamu wa Kwanza na Wa Pili wa Rais wa Zanzibar na viongozi wengine wa kitaifa.

“Hali hii husababisha Wakala [wa Ndege za Serikali] kutekeleza jukumu la kuwahudumia viongozi kwa kuchelewa pindi zinapotokea safari za viongozi wote kwa wakati mmoja,” Mhagama anasema. “Kwa hiyo basi Bunge linaazimia kwamba Serikali ione umuhimu wa kufanya ununuzi wa ndege nyingine ili kuboresha utoaji huduma za usafiri wa anga kwa viongozi wakuu wa kitaifa.”
 
Hii nchi ina maigizo mengi sana.
Shule hazina vyoo, madawati, madarasa, hospitali NHIF mna sema hawawezi kuhudumia afya za Watanzania, umeme una suasua kwa vile mitambo ime choka, ati mna taka kununua ndege ya viongozi.
Shame on you!!!!
 
Bunge la Tanzania limeazimia kuwa Serikali iangalie umuhimu wa kununua ndege nyingine mpya kwa ajili ya kuwahudumia viongozi wakuu wa kitaifa.

Taarifa hiyo imetolewa leo Februari 13, 2024 na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria Joseph Mhagama, ambaye ameeleza kuwa nia ya azimio hilo inatokana na Wakala wa Ndege za Serikali kushindwa kuwahudumia kwa wakati viongozi wakuu pale zinapotokea safari kwa wakati mmoja.

Kwa mujibu wa Mhagama kamati yake imebaini kuwa kwa sasa kuna ndege tatu zinazowahudumia viongozi wa Serikali.

Ndege moja inamhudumia Rais wa Tanzania, ndege nyingine mbili zinawahudumia Makamu wa Rais, Rais wa Zanzibar, Waziri Mkuu, Makamu wa Kwanza na Wa Pili wa Rais wa Zanzibar na viongozi wengine wa kitaifa.

“Hali hii husababisha Wakala [wa Ndege za Serikali] kutekeleza jukumu la kuwahudumia viongozi kwa kuchelewa pindi zinapotokea safari za viongozi wote kwa wakati mmoja,” Mhagama anasema. “Kwa hiyo basi Bunge linaazimia kwamba Serikali ione umuhimu wa kufanya ununuzi wa ndege nyingine ili kuboresha utoaji huduma za usafiri wa anga kwa viongozi wakuu wa kitaifa.”
Aisee hawa watu wamekosa huruma kabisa na binaadamu wenzao yani shida zote hizi za mabarabara wao wanawaza anasa, wakati kutoka dar tu hadi moro watu tunatumia masaa sita kwa ufinyu wa barabara kwa nini hizo pesa kama zipo wasipeleke huko?
 
Back
Top Bottom