Ununuzi wa ndege 6 ulipangwa bajeti ipi?

Kuna mhimili umeenda chini sana..bahati mbaya sijui chini kwa mita za kisima cha kuchimba kwa mkono au mashine...
 
Mkuu Molembe, bajeti ya kununua ndege ilipitishwa na ule mhimili mkuu ambao mizizi yake imejikita chini zaidi.!
 
Ndio maana wanafunzi wanakosa mikopo,kumbe yy anahamisha bajeti kiholela.
 
Jana wakati tunaadhimisha miaka 55 ya uhuru wa iliyokuwa Jamhuri ya Tanganyika (sasa Tanzania), Mhe rais alisema mpaka sasa tumeishanunua ndege sita za kubebea abiria.

Naomba kujua wakati wa bunge la bajeti pesa za kununua ndege zilikuwa zimepangwa kiasi gani na kupitia wizara gani? Je, mpaka sasa ni kiasi gani kimetumika kununua ndege hizo?

Na kama bunge halikupanga kununua ndege hizo, Rais haoni kuwa anaingilia mhimili mwingine ambao kimsingi ndio wenye mamlaka ya kupanga bajeti na matumizi yote ya serikali.

Je, tunahitaji bunge?
Mkuu siyo kweli kuwa Tanganyoka sasa ni Tanzania. Tanzania ni muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Ukisema Tanganyika sasa ni Tanzania maana yake umeitenga Zanzibar
 
Pakipatikana Katiba nzuri. Magufuli atakuja kushtakiwa huko mbeleni.
Kushitakiwa haiwekani kwa vile Katiba inamlinda rais mstaafu. Ila kibaya ni kuwa atamkabidhi nchi rais ajaye ikiwa inevurugwa na hukumu za mahakama za ndani na nje, ikiwa imevuruga separation of power, na kwa kweli aliyosema kuwa nchi ilifika pabaya ndivyo naye atavyosemwa.
 
matatizo na umaskin wa watz ni kutokana na katiba mbovu sana inayompa Raisi kufanya maamuzi yeye mweywe na ashishtakiwe
 
na cs300..sisi tutakuwa wa kwanza kuzitumia afrika nzima....ila magu kwa usafiri wa anga ametisha....maana watu bado hawaamini kila saa porojoo mara kajipangia bajeti mara nini.....ila ingia youtube uone boeingdreamline....ni shiiiiiiiiiiiiiiiiiiiidaaaaaa
Hiyo hela katoa mfukoni mwake?
 
Jana wakati tunaadhimisha miaka 55 ya uhuru wa iliyokuwa Jamhuri ya Tanganyika (sasa Tanzania), Mhe rais alisema mpaka sasa tumeishanunua ndege sita za kubebea abiria.

Naomba kujua wakati wa bunge la bajeti pesa za kununua ndege zilikuwa zimepangwa kiasi gani na kupitia wizara gani? Je, mpaka sasa ni kiasi gani kimetumika kununua ndege hizo?

Na kama bunge halikupanga kununua ndege hizo, Rais haoni kuwa anaingilia mhimili mwingine ambao kimsingi ndio wenye mamlaka ya kupanga bajeti na matumizi yote ya serikali.

Je, tunahitaji bunge?
Hapo 10%inaenda chato
 
Mimi nadhani, ni vema tukayaacha hayo mambo yaendelee bila kujali serikali imetumia budget ipi coz kuyajua hayo yanahitaji taaluma na kuijua hiyo budget yenyewe ya mwaka huu. Naimani CAG yupo macho, mwakani atatuambia which is which kama mtoa mada alivyouliza.
 
Magufuli anafanya anayotaka kutokana na mfumo wetu kwamba Rais ni sehemu ya Bunge.

Tukiacha hili pia Wabunge wenyewe wanaishi kwa hofu, hawaamini nguvu yao.

Ikifika sehemu bunge linakuwa butu basi kuna kuwa hakuna maana ya Bunge.

Wabunge wetu wamechagua maisha haya.
Ni wakati wa wananchi kujitetea wenyewee
 
Bunge kwa kipindi hiki halina kazi yoyote nazani ,rais angekutumia mamlaka aliyopewa kufanya bunge wawe wanakutana mara moja kwa mwaka, pesa tunayookoa hapo itumike kujenga viwanja vya ndege vya maana kila mkoa.
 
Back
Top Bottom