Ungependa nani awe rais wako kati ya hawa?

Jamani kila siku naomba rais awe DOVUTWA, knachonvutia kwake ni ile sera yake ya kununua silaha za kisasa na kwa wingi.
 
WOTE hawafai labda kingunge ngombare mwiru. makamu sheikh simba, waziri mkuu kakobe, spika mama rwakatare
 
CCM wanamuaandaa NAPE NNAUYE kugombea urais! Ongeza na huyo kwenye orodha.
 
Sijampenda hata mmoja kati ya hao katika majina . Maana hakuna hata mmoja aliyethubutu kujenga maktaba katika jimbo lake iwe alipokuwa mmbunge au hivi sasa. Hakuna hata mmoja aliye na mtoto anyesoma ya secondari za kata kwa sababu hawataki kuziboresha humo katika majimbo yao wala kupigania zijengewe maabara! Kwangu mimi bora arudi mkoloni tuu. Labda mkoloni,atajua umuhimu wa maktaba kwa raia waishio wengi vijijini. Ukifika ulaya na marekani swiming pool zipo mpaka vijijini lakini tanzania hakuna kabisaa. Hivi wananchi hawataki recreation centres?
 
Tundu Lissu ndiye anafaa kwa 2015.
P.S ; kwenye magamba bado sijaona, ila Lowassa kidogo anaonekana kuwa yuko serious.
 
Dr Slaa anastahili,ndio mgombea pekee aliyetayari kula mhogo pale ikulu ili watoto wa masikini waende shule!!
 
Pinda anafaa kuwa raisi kutokana na uadilifu wake na uwezo wake wa kuongoza!
 
Kaka Muanzisha mada (Eiyer),katika majina yako hayo yachuje na ubakize Dr.Ibrahim Lipumba,Dr Wilbroad Slaa,Prof.Asha Rose Migiro,Benard Membe,Dr.Mohamed Gharib Billal na Edward Ngoyai Lowasa.Sasa katika mchujo huo utaona kuwa Uteuzi na hali ngumu itakuwa ndani ya CCM kwa sababu kuna makundi makubwa ya kutaka nafasi hiyo ya juu katika Uongozi wa Nchi.Ndani ya vyama vya Upinzani kuna ustaarabu wa Juu na Hekima ya kuchagua nani asimame.Mpaka sasa duru za siasa za vyama vya Upinzani hazizungumzii sana nafasi hiyo ya Urais,Lakini bado inaonekana wale waliosimama ktk uchaguzi wa 2010 wana nafasi tena 2015 pamoja na kwamba Mzee Slaa anasema hafikirii kusimama tena!
 
tunahitaji raisi mwenye nia ya kuleta ukombozi kwa nchi yetu. tumewaona marais wetu waliopita na huyu aliyepo. ukimtoa mwl, waliobaki hawapishani sana. rais wa awamu ya tatu alionyesha karama ya kuwa kiongozi japo alizidiwa na tamaa ya kujilimbikizia mali na hicho ndicho kilichomponza. hawa wawili naweza kusema hakuna kitu tulisukuma muda na tunasukuma muda tena kwa mara nyingine. ifike sehemu watanzania tumshirikishe mungu katika hili. watanzania tuamke, tusitangulize maslahi yetu mbele katika kuchagua viongozi wetu. lakini hata viongozi wetu wamwogope na mungu kama wameshindwa kutuheshimu sisi tunaowapa madaraka. rasilimali za nchi hii sio za kwao na watoto wao, bali ni haki ya kila mtanzania.
 
mambo yote tisa kumi ni kwa spika wao, aisee akipewa urais yule maza watanzania tutaipata. uspika tu tayari ameshachafua bungeni. anahalalisha posho kubwa anachofanya hakionekani.
 
Wilbrod Peter Slaa. binafsi sijaona ubaya wa huyu mtu japo siwezi kushuhudia uzuri wake kiundani. nikiwa kama mpiganaji naipenda cdm saaaaaaaaaaaaana nama wanaonyesha nia ya kuwa wapiganaji. jamani watanzania tunamaisha magumu mno. tembeeni vijijini muone watanzania wenzetu wanavyoteseka na ugumu wa maisha.
 
Back
Top Bottom