Undani wa Freeman Mbowe na Dr Wilbroad Slaa

Huo ndio ukweli fmpiganaji, umenena sina la zaidi ila kusubiri vilaza na comment zao za kuwatoa Slaa na Mbowe ili waweze kupenyeza rupia..
 
fmpiganaji, umesema kweli. Wazo la kufungua matawi kila mahali ni la msingi sana. Aidha kwa sasa inafaa waanze kuelimisha uma juu ya haki yao ya kuchagua viongozi wanaofaa ili waachane na viongozi wa magamba.
 
Hakuna kipengele kwenye katiba ya CDM kinachosema urais utagombewa na mwenyekiti, sioni kwanini uandike eti Mbowe anastahili credit kwa kumwachia Dr Slaa kugombea urais. Hiki ni chama cha kidemokrasia, hivyo mwaka 2015 mwanachama yeyote anayejiona anazo sifa za kuongoza nchi hii, ruksa kuchukua fomu. Hatutaki yaanze kujengwa mazingira ambapo mwanachama tofauti na hawa tuliowazoea akichukua fomu ataonekana msaliti au mamluki. Tuache demokrasia iamue nani atatufaa.

Mkuu kwa tabia ya viongozi wa Africa hasa Tanzania;Mwenyekiti anajiona ndiye mwenye haki ya kugombea urais na ndipo vurugu inapoanzia.Ile tu Mbowe kutambua hilo ni credit kubwa.Mkuu umesahau vurugu ya NCCR pale Mrema alipotishiwa kutokugombea?
 
Ndugu mwanamagamba, hongera kwa kuchagua avatar nzuri inayo-reflect jinsi magamba wanavyoonekana mbele ya jamii.

Ndugu siasa sio kama mchezo wa kiduku ukichuchumaa watu wanashangilia.

Kwa hiyo msipakane mafuta kwa mgongo wa chupa, sifa mnazowamwagia hawa jamaa ni sifa za kienyeji zaidi.

Mwisho wa siku mtasema Mbowe na DK Slaa, wanamzidi Obama, kwa siasa.
 
Nadhani ni wakati sahihi pia kwa chadema kupenetrate had kwa wazee kiitikad ili nao wawe transformed km wanafunzi wengi nchini walivyo kuwa transformed, kwa ufupi ni kwamba tushirikiane kujenga imani ya chama kwa makundi y RIKA ZOTE NCHINI
 
Tumeshuhudia majaribio mengi ya kuivuruga Chadema yakishindwa.Hata issue ya Shibuda jinsi ilivyo kuwa handled imeonyesha busara za viongozi hawa
 
U said it all. Sina nyongeza. Nasubiri akina FF, MS, Ritz, Mzee, Rejao waje kuchafua hali ya hewa! Maana huwa hawana hoja!!!
 
nimependa zaidi calmness yao juu ya issue ya yule kenge shibuda! kama wangekuwa kama wale ccm b na c kungeshakuwa na mtafaruku....
 
pale unaposema kuwa viongozi hawa wawili wasiguswe kwenye uchaguzi ndani ya chama ndio umeharibu kila kitu.naona unaanza kupendekeza udikteta sasa.
 
...mimi kama mwanachama hai wa chadema napongeza sana post hii...sishangazwi na wana jf wanaopinga maana katika jamii yoyote ile mkikubaliana katika kila jambo basi huenda mmoja kati yenu atakuwa hafikiri.
 
pale unaposema kuwa viongozi hawa wawili wasiguswe kwenye uchaguzi ndani ya chama ndio umeharibu kila kitu.naona unaanza kupendekeza udikteta sasa.

Mkuu msome vizuri mtoa mada ana maana gani.Kasema laiti ningekuwa mwanachama wa chadrma ningependekeza viongozi hawa wasiguswe.Hayo ni mawazo yake kutokana na utendaji wa majabali hawa.Ndio maana mjadala uko mezani wala hamna udikteta hapa
 
Ndugu siasa sio kama mchezo wa kiduku ukichuchumaa watu wanashangilia.

Kwa hiyo msipakane mafuta kwa mgongo wa chupa, sifa mnazowamwagia hawa jamaa ni sifa za kienyeji zaidi.

Mwisho wa siku mtasema Mbowe na DK Slaa, wanamzidi Obama, kwa siasa.

Mkuu heri ukae kimya unazidi kujionyesha ulivyo mtupu
 
Nadhani ni wakati sahihi pia kwa chadema kupenetrate had kwa wazee kiitikad ili nao wawe transformed km wanafunzi wengi nchini walivyo kuwa transformed, kwa ufupi ni kwamba tushirikiane kujenga imani ya chama kwa makundi y RIKA ZOTE NCHINI

Pia nadhani kwa kuongezea kidogo kwenye mada,viongozi waijenge zaidi jumuiya ya wanawake BAWACHA.Ni wakati wa kuwa na uongozi imara wa jumuiya hii.Tumieni wabunge wa viti maalum wanaotokana na jumuiya hii.CCM wana mtaji mkubwa wa wanawake wa vijijini
 
Back
Top Bottom