Undani wa Freeman Mbowe na Dr Wilbroad Slaa

Hakuna cha maana ulichoandika zaidi ya kueleza historia zao ambazo kila mwanadamu hakosi historia.

Labda utuambie hizo historia zao zinaisaidia nini Tanzania?

Zimetusaidia kututoa Watanzania kwenye ujinga na kutushitua kuwa nchi yetu na raslimali zetu zinaliwa na wachache,
yaani MAFISADI waliotajwa pale mwembe yanga.Pia wamehamasisha mageuzi Tanzania! BIG UP MBOWE na SLAA!!
 
Chadema wakipata nia ya dhati ya kuwakomboa WATZ nitajiunga nao rasmi, ila kwa sasa acha niendelee kugambika.
 
Kimsingi nikupe pongezi kwa analysis nzuri.Umegusia jambo muhimu ambalo naamini kila siku kwamba ndo siri ya mafanikio ya haraka chadema.Labda kwa madhumuni ya kujifunza naomba ufafanuzi kuhusu hoja yako moja.Pale unaposema kuwa kama chadema ingeshinda urais last election ingekuwa ni mara ya kwanza katika historia kuwa na rais asiye mwenyekiti wa chake.Nakumbuka kuwa marais wote waliomfuata Nyerere waliupata urais kwanza kabla ya uenyekiti.Hii ni kuanzia Mwinyi,Mkapa na huyu wa sasa.Kwa msingi huo nadhani sio jambo geni kuwa na rais asiye mwenyekiti wa chama chake.Labda tuseme chadema wasiige tabia ya CCM ya kuwakabidhi uenyekiti marais wa nchi kupitia chama chao.Au sijakuelewa mkuu?Tuendelee kujadili
 
kwa kweli umenena hata NAPEanaisapoti, FF na M-Sugu nao wameikubali kiaina sana tu ongela sana
 
Kwani si kweli?


That has got nothing to do with us! We dont care how he got the post. Hata kama alipindua. Tunajadili amefanya nini tangu alipoingia kwenye uongozi hadi sasa amefanya nini na what is the way forward.

Karume alipindua serikali halali iliyochaguliwa na wananchi lakini anapongezwa na kutukuzwa huko znz! Wanachoangalia watu wenye akili zao ni what he did na sio how he came!

Kuhusu Mbowe, sio kweli kwamba amerithi. Hizo ni propaganda, fikra na akili za hovyo kabisa kwa mtu anayejiita Great Thinker. This makes you not to deserve in this forum!.
 
Big up CDM.Hapo magamba wameshikwa na kihoro wnatamani watafute njia ya kuwasambaratisha kama vyama vingine vinavyojiita vya upinzani. Wito wang kwa CDM msikubali kutumiwa, kazeni buti Tanzania yote tuko nyuma yenu tuikomboe upya nchi yetu inayotawaliwa na Mafisadi.
 
U said it all. Sina nyongeza. Nasubiri akina FF, MS, Ritz, Mzee, Rejao waje kuchafua hali ya hewa! Maana huwa hawana hoja!!!

Ongezea Barubaru na MAFILILI....yaani wanakazi ngumu sana ya kuuzuia upepo wa mabadiliko ya ukweli
 
Safi sana mzalendo. Baada ya review umekuja na recommendations. Natumai watazichukua na kuzifanyia kazi. Nimeipenda ile ya kuandaa watu wa kugombea kuliko fire brigade kind of operation ya kuwapokea waliotoka vyama mbalimbali na hasa hiki cha magamba ambao huishia kuwa mamluki-case of Shibuda. Well filtered, planned and organised succession sysem must be put in place. Mambo ni mengi na hawezi yote kufanywa overnight na CDM inao viongozi wasikivu, waadidilifu na wazalendo watachukua mawazo yako na mengine yatakayomiminika toka kwa wachangiaji na kuyafanya changamoto.

BIG UP
 
Suala la Udini na Ukaskazini wamelishughulikia vipi?
Tukumbuke kabla ya hawa watu hawajaingia madarakani, siasa za Tanzania hazikuwa na chembe ya udini, hata kama hii dhana ilikuwepo, ilikuwa kwa kiwango cha chini sana.
 
Back
Top Bottom