Mtoa thread kauliza swali la msingi sana. Nahakuna mchangiaji aliyetoa jibu lenye maana.
Sera ya CDM inaelekea ni kuipinga CCM , sera ambayo naona si mbaya ila haina filosofia ya kule wanakoelekea wana CDM.
Kwa post kama hii ndio unaona jisi CDM vipofu wanavoongoza vipofu wenzao.
Zaidi ya ufisadi,suala linaloweza kudfanywa vizuri tu ma wanaharakati, CDM haina muono wala sera ya muelekeo kifilosofia.
Kama ni mafisadi CDM wako tele na wanafahamika.
Ni vyema tukaelewa kuwa kama CDM ikikamata nchi uchumi utakuwaje,siasa ya ukulima itakuwaje, wafanyakazi wattendewa vipi. Nasuala la uwekezaji umekaa vipi kulingana na rasilmali za waTanzania.
Nina uhakika watakachokuja nacho ni kama chama tawala tu maana CDM haina jipya zaidi ya kuingia madarakani.
Lole acha kukurupuka: Je unajua kwamba Chadema ni chama kinachoamini katika mrengo wa wakati na falsafa ya umma? Au ni uvivu wa kusoma?chadema inaamini katika kujenga tabaka la kati la wafanyakazi, wakulima na wafanyabiashara.
Chini hapa ni extract kutoka official website ya Chadema kuhusu itikadi na mwelekeo!
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ni chama mbadala kinachokua na kinachoongozwa kwa Falsafa ya Nguvu ya Umma na kuamini katika itikadi ya Mrengo wa Kati. CHADEMA inawataka watanzania kuelewa kwamba mabadiliko ya kweli yataletwa na kubadilisha mfumo wa utawala. Maendeleo ya kweli hayawezi kuletwa na mafisadi walewale wa chama kile kile chenye uoza ule ule wakiendeleza yale yale kwa ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya. CHADEMA inatambua kwamba kwa falsafa ya Chukua Chako Mapema (CCM), Tanzania yenye neema kamwe haitawezekana. Lengo la CHADEMA ni kusimamia mabadiliko ya kweli na uhuru wa kweli ili kuunda Taifa la watu walio huru na lenye kuzingatia misingi ya utawala bora na linalotoa fursa kwa wananchi wake kushiriki katika kuboresha maisha yao. Tanzania endelevu, yenye haki na isiyovumilia ukandamizaji wa aina yeyote kwa wananchi wake-ndiyo nchi tunayoitaka. CHADEMA inafanya kazi kuhakikisha kuwa vyombo vya utawala na viongozi wanafanya maamuzi ya busara na makini yanayowaletea wananchi nafuu ya maisha na kuwapa matumaini ya kuendelea kupiga hatua za kimaisha katika nyanja zote za maendeleo.