Kididimo
JF-Expert Member
- Sep 20, 2016
- 3,794
- 3,361
Ikumbukwe, nchi yetu imewahi kuwa na Wanawake nguli katika harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika na baada ya kujitawala.
Kwa uchache kulikuwa na kina Lucy Lameck, Bibi Titi, Bi Sofia Kawawa nk. Historia inaonyesha kuna mahala Bibi Titi aliwahi kumgomea Mwl. Nyerere kwa maamuzi aliyoyafanya Mwl bila utashi wa Wanachama wa TANU. Taarifa zilizothibitika baadae,Mwl. alikiri kosa,na kazi ikaendele bila kwa yeyote kujiondoa Uanachama na mafanikio ya kupata Uhuru tuliyaona.
Sina historia sahihi sana ya Halima Mdee katika medani za siasa nje ya CHADEMA. Ila ndani ya CHADEMA ninamfahamu vizuri. Ni moja kati ya Wanachama ambao, hata leo nisikie amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, sitakuwa na shaka yoyote.
Umahiri wake niliuona pale alipoisimamia vyema BAWACHA,licha ya misukosuko kibao iliyokuwepo,ikajulikana pote nchini na hata nje ya nchi.
Aina ya siasa za Bawacha na harakati za kuingiza wanachama wapya kwa wingi, zilifanana sana na enzi zs UWT ya TANU ya kina Sofia Kawawa enzi hizo.
Hii inatuonyesha kuwa huna namna unaweza kusema unaimarisha Chama cha Siasa hapa nchini kwa kuwaacha wanawake nyuma.
Kwa hali ya mrengo wa Kisiasa ulivyo nchini hivi sasa na kwa kuzingatia Raisi ni Mwanamke, Chadema itahitaji sana BAWACHA imara kuelekea 2025. Siyo siri,kura nyingi 2025 zitatoka kwa kundi la Wanawake.
Nikiri wazi mimi siyo Mwanachama wa Chadema,bali napenda sana mtu makini, mwenye maono,asiyetetereka na anayetia chachu ya Maendeleo kwa nchi yangu.
Nilisema simpendi Halima Mdee kwa sababu zangu binafsi, ila napenda umahiri wake wa kupigania jambo kwa hoja, na ni Political material kwenye siasa za wakati huu.
Binafsi nawasihi Baraza Kuu la CHADEMA,fikirieni vyema,umuhimu wa kundi la kina Mdee na wenzake ndani ya Chama chenu. Anzeni upya, pale mlipokosana, tumieni muda mfupi sana kusameheana, endeleeni kukijenga Chama.
Nchi ilikofikia sasa mnahitajika kuliko tulikotoka. Unganeni, nchi itawaelewa. Msipofanya hivyo,sina maneno sahihi ya kusema kitakachotokea kuelekea uchaguzi 2025.
Mh,Mbowe, Tundu Lisu, Sugu,Mnyika, Heche, Wenje nk. Kina Mdee ni Dada zenu,wasameheni bure,wamalizie Ubunge wao,hamtapungukiwa kitu, mrudi kama zamani,tuwasikie bungeni nchi isonge mbele.