liongo. Miaka 20 af amesoma ad 6 na kamaliza chuo??? Kudadadeki
Mimi ni msichana wa miaka 20 naishi magomeni jijini dar nimejitokeza kwenu kushare tatizo langu. mimi sina wazazi wote walifariki kwa ajali ya gari mwaka 1998, Mimi waliniacha nasoma shule ya msingi. Sasa baada ya kumaliza nilifanikiwa kujiunga na sekondari nilisoma hadi form 4 nikamaliza pia nikapass mitihani yangu. nikatakiwa kidato cha tano,kabla sijaenda shule nilibahatika kupata mchumba muuza genge na akaahidi kunisomesha kwani mimi nilikosa ada. Nashukuru mungu kanisomesha hadi chuo kikuu na nimemaliza hadi sasa nimepata kazi yangu. siwezi kuishi na muuza genge hata siku moja kwanza hajui kuvaa akapendeza pili hana elimu.Sasa je nifanyeje kumwambia ukweli kwamba mimi siwezi kuishi na yeye bila kuumiza moyo wake.
"NIMEIKUTA MAHALI NIKASHIKWA NA BUTWAA NIKASHINDWA KUCOMMENT .........HIVI MTU KAMA HUYU UTAMSHAURI NINI!!"
Hapo kweli mkuu Maprosoo, tena mfano ukumfungilia biashara anaanza kupendeza wajanja wanaanza kumuona sasa hapo ni kumwachia mungu tu kama ni wako atakuwa wako kama sio ndio imekula kwako
Aisee
-"Wanawake wenye akili zao huwa hawadate wadogo zao au watu ambao wana hadhi ya chini yao."-
.......Swahiba, is this really coming from you au ni usingizi tu ulikupitia?
No wonder wanaume wengi wenye mawazo pumba hawakubali wake zao kujiendeleza kielimu na hata kuchukia wake zao wanapopata mafanikio ya kikazi au kibiashara (uanaume wao usijeshuka hadhi!)
JF ni kiboko, naona umeanza ku-link matukio na umri na kugundua haiwezekani ni kisa cha kutunga, but all in all kabla ya kuingia kwenye committment ya kumtunza mtu lazima mjiulize kitu gani kinachowafanya kushindwa kuingia kwenye ndoa sasa huku anasoma chuo na badala yake unaacha mpaka anamaliza chuo wakati hata kama walikuwa hawatambuliki kama wanandoa but still walikuwa karibu kama mtu na mpenzi wake kitu ambacho kinawezekana kabisa wakawa karibu kama mke na mume huku anasoma.
Kama muuza genge ameweza kumsomesha mpaka akafika chuo kikuu maana yake huyu jamaa na skill ya ujasiamali hivyo kuna possibility kabisa kama atatumia degree yake na kumbadilisha mpenzi wake kutoka kuuza genge na kufanya biashara nyingine ambayo mwanamke ataona ni ya hadhi yake (na hii ndio kazi ya msomi na si kuwa na cheti na kutegemea kuajiriwa tu). hata hao anaoona wanaendana akifuatilia miaka 6 nyuma ukute walikuwa warugaruga tu kwani sifa ya binadamu ni kubadilika hivyo hata huyo muuza genge ana nafasi ya kubadilika na wakaendana (kila kitu kinawezekana mbele ya fedha)
Aisee hapo patachimbika jamaa hatomwelewa kabisa huyo dada tena huo ni utapeli,kingine mamen mwanamke is undifined leo yuko fresh kesho anakutia maumivu yani hasa kabila la ........................hakishajua kuna mali atakupa fake love mwisho anaweza kukuua hata kama mna watoto xo careness ni muhim kwa hawa watu!!!nawasilisha!!
Ukistaajabu ya musa utaona ya Firauni!!!! Wanawake, wanawake, wanawake!!!! Hivi pia haijawahi kutokea mwanamke akamsomesha mume wake, mwishowe mwamaume anamwona mke ni tambara bovu?
Nina kesi moja ya mwanaume ameajiriwa tena Wizara ya Sayansi, Teknolojia na Mawasiliano ambaye mke wake alijinyima akawa anamlipia sehemu ya ada akiwa anasoma dedree ya pili. Ila tu mwanaume yule hakuwa na uungwana na mkewe. Kwa sasa baada ya kupata mafanikio na kuanza ujenzi, au kama ameshamaliza basi akachukua wanawake wengine lukiki na sasa hata mke mwenyewe kashatimuliwa na watoto watatu!!! Sasa anajiandaa kufunga ndoa na kidosho wa mjini ambaye hakuwahi hata kumsaidia!!
Kwa hiyo haya mambo yako pande zote mbili!! Ndiyo maana siku hizi ndoa nyingi ni kwa machale sana!!! Hakuna mwanaume au mwanamke anajitoa full kwako!! Huo ndiyo ukweli, wanandoa wanachekeana kiunafiki ili siku zisonge tu!!
Huyu msichana ni very right. Kusema kweli tangu awali hakumpenda muuza genge. Alitaka pesa za kulipia masomo yake. Hakuwa na njia nyingine ya kufanya. Alipojitokeza muuza genge aliyekuwa tayari kukidhi haja yake ya kusoma ilikuwa ahueni yake. Hapakuwa na mapenzi pale. Muuza genge alitakakumdhalilisha mtoto yule kutumia pesa yake ya genge. Msichana yule angekubali kuolewa naye kabla ya kumaliza masomo, angemharibia. Mtoto wa kike alimwambia SIDANGANYIKE. Subiri ni some. Baada ya masomo anatoa maamuzi ya kiutu uzima.
Muuza genge na graduate wapi na wapi?
Kama muuza genge angekuwa na busara angemwambia aendelee na ustarabu, ikiwezekana amkumbuke katika ufalme wake
Haaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaah, inauma sana, jamani watu hawana aibu wala huruma. Imagine ingekuwa ww ungefanyaje?
hastahili kutolewa kafara.
Fanya uchunguzi kidogo, utagundua kuwa zaidi ya 70% ya wanawake ambao wamesaidiwa na mabwana wanaotafuta riziki kwa tabu, huwa wanawakimbia hao mabwana mara baada ya mambo ya hao wanawake kuwa super sana.
Ukiwauliza kwa nini? Wanakwambia hatuendani. Ukiwauliza mbona ulikuwa nae kwa mingi tu hukuliona hilo? Hawakupi jibu la kueleweka.
Hii imeshatokea kwa watu wengi tu, sio kitu cha kushangaa wala kushtuka.
Solution ni kuwa mwangalifu tu wakati una-invest kwa mwanamke, na utambue anaweza akabaki na wewe au akala kona baada ya kufanikiwa hivyo uandae jinsi ya ku-ease the pain.
Kwa upande wangu nita-invest kwa mwanamke mwenye mtoto wangu manake hata akikimbia atalea mwanangu.
Mimi ni msichana wa miaka 20 naishi magomeni jijini dar nimejitokeza kwenu kushare tatizo langu. mimi sina wazazi wote walifariki kwa ajali ya gari mwaka 1998, Mimi waliniacha nasoma shule ya msingi.
Sasa baada ya kumaliza nilifanikiwa kujiunga na sekondari nilisoma hadi form 4 nikamaliza pia nikapass mitihani yangu. nikatakiwa kidato cha tano,kabla sijaenda shule nilibahatika kupata mchumba muuza genge na akaahidi kunisomesha kwani mimi nilikosa ada.
Nashukuru mungu kanisomesha hadi chuo kikuu na nimemaliza hadi sasa nimepata kazi yangu.
Siwezi kuishi na muuza genge hata siku moja kwanza hajui kuvaa akapendeza pili hana elimu.Sasa je nifanyeje kumwambia ukweli kwamba mimi siwezi kuishi na yeye bila kuumiza moyo wake.
"NIMEIKUTA MAHALI NIKASHIKWA NA BUTWAA NIKASHINDWA KUCOMMENT .........HIVI MTU KAMA HUYU UTAMSHAURI NINI!!"[/QUOTE
Haya yanatokea sana USA mtu anabeba mzigo kusomesha mtu halafu mwanamke akigraduate tu bye .shoga Angu alimfanyia boyfriend wake hayo.
mimi ni msichana wa miaka 20 naishi magomeni jijini dar nimejitokeza kwenu kushare tatizo langu. Mimi sina wazazi wote walifariki kwa ajali ya gari mwaka 1998, mimi waliniacha nasoma shule ya msingi.
Sasa baada ya kumaliza nilifanikiwa kujiunga na sekondari nilisoma hadi form 4 nikamaliza pia nikapass mitihani yangu. Nikatakiwa kidato cha tano,kabla sijaenda shule nilibahatika kupata mchumba muuza genge na akaahidi kunisomesha kwani mimi nilikosa ada.
Nashukuru mungu kanisomesha hadi chuo kikuu na nimemaliza hadi sasa nimepata kazi yangu.
Siwezi kuishi na muuza genge hata siku moja kwanza hajui kuvaa akapendeza pili hana elimu.sasa je nifanyeje kumwambia ukweli kwamba mimi siwezi kuishi na yeye bila kuumiza moyo wake.
"nimeikuta mahali nikashikwa na butwaa nikashindwa kucomment .........hivi mtu kama huyu utamshauri nini!!"
Inawezekana unachosema kina ukweli....ila ni kwa nadharia zaidi....
Kama huamini ni sawa tu..ila ukweli ni kwamba wanawake wanapata shida kuvumia kuishi kwenye ndoa na mtu wa hadhi ya chini yake....Mtaani atasema unapaka shombo au unamtia aibu....Hawezi kutoka na mtu wa namna hiyo na kwenda naye kwenye high profile meeting au party....., Graduate na muuza genge wapi na wapi jamani??
Tuwapende tu, ila huo ndiyo ukweli kuhusu mama/dada/binti/wajukuu zetu.....!
It is a bitter fact....but it is still a fact!!
Babu DC!!