Unamshaurije huyu dada?

Babu kwa makavu hahaha! Same goes for men, stukaa!
So unachomaanisha ni kuwa unavyomkuta mwenza na kumpenda muache hapo hapo kwa hadhi yake na usihangaike kumnyanyua? Manake wanawake tunastruggle, mwanaume umempenda hana kitu. Mnajenga na kununua magari ya maana huku ukiafanya 'maarifa' yale ya The Boss. Lakini mambo yakinyooka anatafuta mrembo wa haja wa hadhi yake na anaejua kutembelea red carpet! Labda kazi ya maendeleo iwe entirely kazi ya mume?
Huyu mwanamke ana akili sana,

Apewe moyo na ushauri wa kumalizana na muuza genge...Hawa ni kama matope na maziwa....hawawezi kuishi pamoja hata kwa mtutu wa bunduki.

Wanawake wenye akili zao huwa hawadate wadogo zao au watu ambao wana hadhi ya chini yao.

Kama kuna mwanamume hajui ukweli huu basi maumivu ni halali yake!!

Babu DC!!
 
Last edited by a moderator:
Babu kwa makavu hahaha! Same goes for men, stukaa!
So unachomaanisha ni kuwa unavyomkuta mwenza na kumpenda muache hapo hapo kwa hadhi yake na usihangaike kumnyanyua? Manake wanawake tunastruggle, mwanaume umempenda hana kitu. Mnajenga na kununua magari ya maana huku ukiafanya 'maarifa' yale ya The Boss. Lakini mambo yakinyooka anatafuta mrembo wa haja wa hadhi yake na anaejua kutembelea red carpet! Labda kazi ya maendeleo iwe entirely kazi ya mume?

Komando wangu@King'asti,

Kama unahisi kuwa utakachomfanyia mpenzi wako kitamrusha viwango...basi kaa mkao wa tahadhari kwani kuna uwezekano mkubwa wa kukuacha....especially kama bond yenu ni loose!

Hata hivyo, hili suala linawapa taabu wanawake zaidi kuliko kwanaume. Sababu kubwa ni kuwa wanaume wanaweza kuwa na mke wa nyumbani (mama watoto hata kama ni wa kwango cha chini sana) na wakati huo wakawa na mtoto bomba huko mitaani ambaye ni photogenic...I mean wa kutoka naye na kujidai!

Kwa wanawake, ni bahati mbaya kwamba hili ni gumu sana. Hata akitokea kulifanya wakati ni mke wa mtu, haweza kuwa na uhuru na huyo partner wake wa nje linapokuja suala la kutoka naye kwenye public.

Uzoefu wangu ni kwamba, mwanamke akipanda sana chat na wakati huo mume wake akabaki chini...na endapo hakuna uwezekano wa kumfanyia make up huyo mwanamume.....automatically huyo baba atakuwa ametolewa nje ya game....very unfortunate for us....Ila nawaelewa sana wadogo na wajukuu zangu!

Babu DC!!
 
Hahaha! Katushikaje masikio poo? 7+4+2+1 idle year+3 univ. Alianza std 1 akiwa 3 yrs old. Chezeiya magomeni?


Hata mimi nimeliona hilo...ila nimejikita kwenye subject yenyewe badala ya mhusika ambaye kwa kweli hawezi kuwa amemaliza college kwa sasa...may be ni super genius!

Babu DC!!
 
we lazima mgonjwa acha tamaa!we umechukua hela za muuza genge! halafu leo unaleta ugolo wako hapa! mtaka cha uvunguni sharti ainame,inama sasa! nawachukia sana watu kama wewe!mnaoana kuendeleza maisha na sio kuanzisha maisha!
 
ndio maaana nimeshindwa hata kuchangia hii mada maana ni uongo mtupu

Mi mwenyewe nililiona hilo ila nikajiuliza pengine amemaliza kacertficate!! na ningeweza kuedit pia!! ila lengo langu ni nyie kujikita kwnye mada husika mana inaweza ikakutokea hata ww, na kilichonichanganya zaidi mimi na mpango w kumsomesha shore mmoja nikataka nione wadau mtasemaje!!!
 
Hatuwezi laumu sana , Maisha ya siku hizi ndo yako hivyo
huyu binti asifanye haraka kumuacha Huyu jamaa maana Mungu alimtumia huyu Ili yeye afike hapo alipo ,
na kama amefika hapo .... sasa ni muda wa kutafakari kwa nini kafika hapo na si kuvunja Mahusiana na watu walio kufikisha hapo alipo.
Asifanye kama wanasiasa .....Omba kura ....pata ushindi wa kishindo .....telekeza wapiga kura wako ..... jiunge na Mafisadi hadi Kieleweke.
Mwisho wekewa sumu na mafisadi na kufa polepole kwa mateso.


Ya wezekana binti kufanya hivyo kwa misingi ya Muonekano,Pesa na Maisha . Lakini je huyu aliye kufikisha hapo anajisikiaje? Huoni kuwa bado ananafasi yake bado katika Muonekano , Pesa na Maisha?

Hujui kuwa Masikini wa Leo ni tajiri wa kesho,
Huyu jamaa alikuwa tajiri na zungu lako
kakusomesha mpaka basi tena

Binti ulikuwa hivyo kabla ya Huyu jamaa;
masiki wa mwisho, huna muonekano na huna maisha yoyote ya maana
hata ukatamani kuchumbiwa na Muuza genge
lakini huyu jamaa
(mchumba muuza genge)
hakukataa ,kakuwezesha hadi hapo.
Akajifunza kukupenda na Kusubili

Binti
Hujui kuwa Muonekana ni BANDIA siku zote, as long as the essence of life and living is.


Huyu binti haja Komaa

Ndugu yangu Bado unakazi ya kumlea kama ulivyo weza kulea hadi Chuo ,
Amekukataa ........safi sana ..... ni mtoto wako tu
(mchumba) atarudi kama alivyo kuja mwanzoni na huta juta kumpokea

Mapenzi na Ndoa Mungu ndie anajua timiza wajibu wako na mengine Mwachie MUNGU

USISAHAU KUPIMA UKIMWI
 
liongo. Miaka 20 af amesoma ad 6 na kamaliza chuo??? Kudadadeki

JF ni kiboko, naona umeanza ku-link matukio na umri na kugundua haiwezekani ni kisa cha kutunga, but all in all kabla ya kuingia kwenye committment ya kumtunza mtu lazima mjiulize kitu gani kinachowafanya kushindwa kuingia kwenye ndoa sasa huku anasoma chuo na badala yake unaacha mpaka anamaliza chuo wakati hata kama walikuwa hawatambuliki kama wanandoa but still walikuwa karibu kama mtu na mpenzi wake kitu ambacho kinawezekana kabisa wakawa karibu kama mke na mume huku anasoma.

Kama muuza genge ameweza kumsomesha mpaka akafika chuo kikuu maana yake huyu jamaa na skill ya ujasiamali hivyo kuna possibility kabisa kama atatumia degree yake na kumbadilisha mpenzi wake kutoka kuuza genge na kufanya biashara nyingine ambayo mwanamke ataona ni ya hadhi yake (na hii ndio kazi ya msomi na si kuwa na cheti na kutegemea kuajiriwa tu). hata hao anaoona wanaendana akifuatilia miaka 6 nyuma ukute walikuwa warugaruga tu kwani sifa ya binadamu ni kubadilika hivyo hata huyo muuza genge ana nafasi ya kubadilika na wakaendana (kila kitu kinawezekana mbele ya fedha)
 
liongo. Miaka 20 af amesoma ad 6 na kamaliza chuo??? Kudadadeki
Nimeona na kusikia mifano mingi ya hivyo hasa wanawake wengi wanaofadhiliwa kwa kutoa kikojoleo huwa wanageuka na kuwa hivyo, ila ninachoshauri kwa wanaume wenzangu, ukitaka kumkoga mwanamke hadi aje akukumbuke hata akiwa ameolewa na anaingia kaburini, kama unauwezo wa kumsaidia msaidie tu na katu isiwe kikojoleo ndo dhamana yake, na hata akitaka kukupa mwambie nakusaidia tu kama binadamu mwenzangu na sio kwa ajili hicho kidude chako. halafu endelea kumsaidia hadi atimize malengo yake, nakwambia hivi, hata wakimwijia watu wa aina gani lazima atakushirikisha umshauri na hata kukuhangaikia kifikra. lkn ukichovya yeye akili yake kwamba amekulewesha kimahaba na ndo malipo yako kwa kumsaidia. toeni kuwasaidia kama sadaka. lkn inajenga mahusiano mema zaidi kuliko kuinvest kwa sababu ya kupata pozeo la kikojoleo.
 
Aisee :D

-"Wanawake wenye akili zao huwa hawadate wadogo zao au watu ambao wana hadhi ya chini yao."-

.......Swahiba, is this really coming from you au ni usingizi tu ulikupitia?

No wonder wanaume wengi wenye mawazo pumba hawakubali wake zao kujiendeleza kielimu na hata kuchukia wake zao wanapopata mafanikio ya kikazi au kibiashara (uanaume wao usijeshuka hadhi!)

Ndugu yangu Mbu

Wacha kabisa...kama mama Mbu ana-behave...basi mshukuru MUNGU...

DC alichoandika ni sahihi...hapo kwenye red, naomba nitofautiane na ww...with due respect.

Asilimia kubwa ya akina mama wakifanikiwa ni tatizo katika familia zao...
 
mbona heading haiendani na maudhui ya sred?acha kugeneralise na kuwalisha wenzio sumu,women are nt uniform objects.
mkuu maprosooo naona unawachokoza watu walio gender sentive kama mwanaharakati ciello shauri yako watagomea mechi
 
Mimi ni msichana wa miaka 20 naishi magomeni jijini dar nimejitokeza kwenu kushare tatizo langu. mimi sina wazazi wote walifariki kwa ajali ya gari mwaka 1998, Mimi waliniacha nasoma shule ya msingi. Sasa baada ya kumaliza nilifanikiwa kujiunga na sekondari nilisoma hadi form 4 nikamaliza pia nikapass mitihani yangu. nikatakiwa kidato cha tano,kabla sijaenda shule nilibahatika kupata mchumba muuza genge na akaahidi kunisomesha kwani mimi nilikosa ada. Nashukuru mungu kanisomesha hadi chuo kikuu na nimemaliza hadi sasa nimepata kazi yangu. siwezi kuishi na muuza genge hata siku moja kwanza hajui kuvaa akapendeza pili hana elimu.Sasa je nifanyeje kumwambia ukweli kwamba mimi siwezi kuishi na yeye bila kuumiza moyo wake.
"NIMEIKUTA MAHALI NIKASHIKWA NA BUTWAA NIKASHINDWA KUCOMMENT .........HIVI MTU KAMA HUYU UTAMSHAURI NINI!!"

Kwa Magomeni sishangai!!
 
Hahahaaaa! Hili ndo jiji banaaa, tenda wema uende zako, usingoje shukrani!!!! Muuza genge kakopwa huyooo! Dawa ni kutoinvest kwa mwanamke utegemee longterm returns!!!! Dawa ni kuendelea KUDOKOA investment yako daily hata siku ikikupiga chini ushafanya depreciation of asset ya kutosha tuuu. Ukiwekeza uje ule bdae!!!!! WENZIO WANAKUJA KULA NA HAWAMBAKISHII BABA!!!!
lara 1tehe!tehe!kama ulivyokopwa na sharo kwa wachina...kudadeki watu wabaya!wabaya!
 
Siku zote mwanamke anamkubari mwanamme kwa kuangaria status yake, kama hamuendani hawezi kubari kuwa nawe sasa kama huyu kaka hali yake bado ni ilele ya genge dada status yake imepanda toka o-level mpaka chuo, wanawake hawa wa kiafrika ni kazi sana kubaki kwenye hayo mahusiano.
 
Jamaa alichelewa nini kumdunga kamimba,wala asingejimanua manua hivyo!!
Hawa masista duu dawa yao ni mimba tu,mbwembwe zote tupa kule lol!
 
mbona heading haiendani na maudhui ya sred?acha kugeneralise na kuwalisha wenzio sumu,women are nt uniform objects.


Inawezekana uko sahihi Ciello lakini taarifa zilizoko hiko site zinasema wanaume wengi walioamua kuwasomesha wapenzzi wao ilhali hawana elimu hukimbiwa kwa hoja kama za kwenye uzi.

Kama umesoma somo la takwimu (statistics) kuna kitu kinaitwa mtawanyiko wa kawaida (normal distribution) ambacho kinadai kuwa hoja inaposema kuwa "wote" maana yake ni asilimia sitini na nane (68%).

Kuna ukweli fulani katika hii kitu.



Bazazi ni Bazazi!
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom