Unafiki unaoletwa kwenye Mambo ya Mila na Desturi

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,900
UNAFIKI UNAOLETWA KWENYE MAMBO YA MILA NA DESTURI.

Anaandika, Robert Heriel.
Mtibeli.

Kwa kweli wengine unafiki ulitupita pembeni. Leo nitauelezea unafiki uliopo katika jamii yetu unaosemwa Kwa Wakubwa na wadogo. Sitamung'unya maneno. Hivyo kama unajiona una Roho nyepesi ingefaa upuuzie andiko hili hapahapa usiendelee kusoma. Andiko hili asome mtu mzima mwenye umri unaotambulika kama MTU mzima Kwa sheria za nchi na sheria za kimataifa,(mahususi miaka 18).

Oooh! Taikon hufuati Mila na desturi, mara hoo Watoto wa siku hizi mmeacha Mila na desturi na blah! Blah! Blah!
Alafu MTU huyohuyo anayeongea maneno hayo utashangaa unamkuta Kanisani au msikitini. Hivi mtaacha lini unafiki ninyi Watu. Hivi uliona wapi mtu anayefuata Mila na desturi za kiafrika akaenda Kanisani au msikitini. ATI sijui Mkristo au muislam. Lini muafrika mfuata Mila na desturi akawa Mkristo au muislam. Lini?
Kitendo cha kuwa mkristo au muislam moja Kwa moja kinaonyesha wewe sio MTU wa Mila na desturi za jamii yako.
Alafu unakaa unakaza shingo kuwaambia Watoto wako oooh! Ninyi hamfuati Mila na desturi, wewe unafuata?

Oooh! Kama unataka kunioa kanitolee Mahari, au unaishi na Binti yetu na haujatoa Mahari. Hufuati Mila na desturi. Kijana unasema sawasawa. Nitatoa Mahari na nitakuoa lakini sitaoa MKE mmoja nitaoa Wake wengi kwani Sisi ni waafrika na huo ni utamaduni wetu. Mwanamke hataki, familia yake haitaki. Hivi ninyi mmelogwa na Nani? Kwa nini mnaleta unafiki, Kwa nini mnapenda mambo nusunusu! Kama mmeamua kufuata Mila na desturi zenu fuateni kikamilifu. Si mnapenda Mila ninyi?

Sasa Mahari unataka utolewe, sawa! Lakini hutaki muolewe wake wengi. Umelogwa wewe. Kama unataka usasa basi fuata usasa. Kama unataka Mila fuata Mila. Eboo!

Unapenda mambo ya Mila na desturi alafu ukiambiwa Mumeo akifa urithiwe hautaki, wewe ni mwehu na mwendawazimu. Msitake kujifanya Watu wa Mila alafu Mila zenyewe hamziwezi. Acheni mambo ya unafiki.

Unataka mambo ya Mila na desturi alafu muda huohuo unakataa Ukabila. Hivi ninyi mmelogwa? Kufuata Mila na desturi ndio ukabila wenyewe huo. Huyu ni mnyamwezi Yule ni Mhehe. Kimila na kitamaduni hakuna mahusiano hapo.

Unajiita MTU wa Mila na desturi alafu hapohapo unakataa matambiko. Yaani kama jinga flani hivi. Hivi Muafrika na matambiko utamtenganishaje akiwa mfuata Mila. Matambiko ndio sehemu ya ibada za kimila. Lakini Kwa unafiki wetu MTU anakataa waziwa,I hataki matambiko alafu Baada ya muda utasikia akipayuka Watu mfuate Mila na desturi. Unabaki kumshangaa.

Nani anaamua Hii ni Mila potofu na hii sio Mila potofu? Nani huyo? Anatumia vigezo gani? Alafu unakuta MTU sio kabila Fulani au hatoki jamii Fulani alafu anasema Mila na desturi Fulani ni potofu. Anatumia vigezo gani kuhukumu mambo yasiyomhusu?

Tuache UNAFIKI, kama tumeamua kuishi kisasa na kila MTU ajiamulie mambo yake basi tuishi hivihivi. Ilimradi tufuate sheria za nchi. Kumbuka nchi ni mchanganyiko wa makabila mengi hivyo hakuna mambo ya Mila na desturi hapa.

Wewe ukisema mila Fulani ni potofu basi elewa Kwa mwingine inaweza kuwa sio potofu. Ukisema kuoa wake wengi sio kuzuri basi mwingine atakuambia kutoa Mahari ni Mila potofu. Yaani mtachanganyana kivyovyote. Kwa sababu mmeamua kuchangamana, na Mila na desturi haziruhusu kuchangamana.

Taikon nimemaliza, mambo ya kinafiki tuache. Tukubali moja kuacha kujifanya Watu wa Mila na desturi tuishi kisasa na tusipangiane, au tuamue kurudi Nyuma kufuata Mila na desturi zetu tupangiane, na hapo automatically ukabila utakuwa umerudishwa.

Nipumzike SASA.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Tuache unafiki ✍️
 
Upo sawa aisee. Hata haya majina ya kizungu tuyaache, tufate majina yetu kama Chacha, mwansansu, Marwa, Masunga, Rweyimamu n.k.
 
Taifa lisilo na utamaduni ni Taifa mfu.

Ila ili tuishi lazima tuchague kipo twende nacho kipi tukiache.

Kuna Mila nzuri tuzitunze tuishi nazo na kuna Mila mbaya lazima tuziache.

Tuige Yale yanayofaaa na kujenga jamii tuache kabisaa yakuiga ambayo ni mabaya mfano ushoga.

Lazima tuishi Kwa kuchanganya changanya Kwa vile hakuna Mila Fulani ambazo ni nzuri kwenye kila idara.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom