Jukwaa la malezi ya watoto, Tamaduni za Kitanzania, desturi na mila kale mbalimbali za Kiafrika

syndicate

JF-Expert Member
May 5, 2016
204
315
Habari wana JF,

Mods, Hon Members

Including Rais wa Jamhuri ya Muungano!

Leo naomba tupoze vichwa kidogo kutokana na maswahibu mbalimbali tunayoendelea nayo ikiwemo ili la Bandari.

Naomba Mods na Developers(maafisa ustawi wa jukwaa) wa Jamii forum, muone ulazima sasa wa kuongeza jukwaa pendwa litakalokuwa linahusu Malezi ya watoto, tamaduni mbalimbali za kitanzania, desturi na mila kale mbalimbali za kiafrika.

Yafuatayo ni mfano wa mambo mbalimbali ambayo yanaweza kuwemo katika jukwaa husika!

Watu kupata fursa mbalimbali ya kuandika vitu vyote vihusuvyo malezi mbalimbali ya watoto african based.

Vitu vinavyojenga akili za watoto katika makuzi, Lishe mbalimbali ya kiasili, maadili na miiko mbalimbali kutokana na mila tofauti tofauti.

Tamaduni mbalimbli za kitanzania:

Hapa watu wapewe fursa adhimu kusimulia tamaduni zao mfano jando na unyago tiba za asili (mfano kwenye kabila lako endapo yakitokea majanga mbalimbali kama njaa au ukame nini kilikuwa kinafanyika!? Au mtu akigongwa na nyoka ni dawa gani zilikuwa zikitumika, au mnyama mkali ikitokea akawa anasumbua kijiji nini kilikuwa kinafanyika na kadhalika.

Desturi:
Hapa kama kuna desturi yoyote kwenye jamii husika inaweza kuelezwa kiundani na watu wakajifunza.
Mfano wakunga wa zamani walikuw wanafanya nini kuzalisha mama zetu salama au uzazi wa mpango wa kale ulikuwa unafanyika kwa namna gani.

Mila kale mbalimbali:
Hapa watu wanaweza kueleza mila mbali mbali za kale zilizorithiwa vizazi na vizazi ambazo kwasasa inawezekana vipo au vimeshapotea lakini ni katika ku'enzi utamaduni wa mwafrika, mfano huko zamani wazee wetu walikuwa wana'abudu na kuamini nini...!? Kadha wa kadha.

Karibuni kuchangia zaidi na zaidi ili kuijenga jamii yetu kwasababu naamini tutawasaidia wengine katika yale tutakayoyaandika.

Naomba kuwasilisha.
 
Back
Top Bottom