Una tabia gani za kizee?

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,815
4,565
Salaam Wadau?

Katika maisha yetu tunajikuta tunafanya matendo mbalimbali kila siku. Kuna namna fulani unaweza kujikuta wewe ni kijana lakini baadhi ya matendo yake ukijitafakari unaona kabisa hayaendani na umri wako.

Kwa upande wangu najikuta mtu mzima kwa kupenda nyimbo za Wazee wa zamani kama nilizaliwa nao. Nikisikiliza najiona nna busara nyingi sana.

Vipi wewe una tabia gani ambayo unahisi ni ya kizee?
 
"Watoto wangu njooni,
Njooni niwaambie,
Maisha ya sasa,
Yamebadilika,
Tofauti na zamani.

Wakati wa ujana wangu,
Mimi Baba yenu,
Shati dukani,
Shilingi sita unapata,
Lakini sasa hivi,
Shilingi sita,
Hata soda haupati.

Kwa hiyo wanangu,
Muishi kuendana,
Na wakati.
Kwa hiyo wanangu,
Muishi kuendana,
Na wakati.
 
Salaam Wadau?

Katika maisha yetu tunajikuta tunafanya matendo mbalimbali kila siku. Kuna namna fulani unaweza kujikuta wewe ni kijana lakini baadhi ya matendo yake ukijitafakari unaona kabisa hayaendani na umri wako.

Kwa upande wangu najikuta mtu mzima kwa kupenda nyimbo za Wazee wa zamani kama nilizaliwa nao. Nikisikiliza najiona nna busara nyingi sana.

Vipi wewe una tabia gani ambayo unahisi ni ya kizee?
Nikiona ugoro mwili unasisimka sana .. vipi hii inaweza kuwa tabia ya kizee kweli..!
 
Salaam Wadau?

Katika maisha yetu tunajikuta tunafanya matendo mbalimbali kila siku. Kuna namna fulani unaweza kujikuta wewe ni kijana lakini baadhi ya matendo yake ukijitafakari unaona kabisa hayaendani na umri wako...
Kusikiliza nyimbo sio tabia ya kizee.... Nyimbo ni chakula Cha ubongo kinachochochea hisia, kumbukumbu, mapenzi, urafiki, majonzi na nyakati.

Ubongo unavyotafsiri mapigo na sauti ya wimbo Hauna habari kuhusu umri wa ule wimbo. Ubongo unapenda kusikia na kuona vitu vizuri muda wote. Kuna nyimbo zimepikwa kweli....
 
Kutokubishana ovyo, hata kama ni mambo ya mipira napenda twende kwa data na hoja sio makelele kama mpo sokoni.

Napenda kukaa na watu wazima walionizidi umri na kipato! Kuna namna najifunza kutoka kwao !!!!!

Nikilala sipendi kuamshwa!

Nikimpigia mtu simu mara moja asipopokea sipigi tena, kama ni muhimu sana nitamtumia ujumbe mfupi!

Sifanyi kitu bila utaratibu/mipango! Mfano hata kama sina kazi from no where huwezi niambia twende sehemu flani nikaenda!!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom