Uzeeni tunaishiwa nguvu za kufanya kazi siyo nguvu za kula

Manyanza

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
9,527
14,403
Denis Mpagaze
________________________

1. Hivi umewahi kujiuliza ni kwa nini kila unavyozidi kukua kiumri ndivyo jamii inavyozidi kujitenga na wewe?

2. Yaani inakukwepa. Makazini waaita kustaafu. Unastaafu kufanya kazi lakini hustaafu kula.

3. Tatizo la uzee nao bhana. Kuna umri ukifika unakuwa kama picha ya ukutani nyumbani.

4. Ulipokaa ni hapo hapo. Hutoki. Tofauti yako na picha ya ukutani ni kula. Wewe unakula picha haili.😄😄

5. Unampata nani sasa wa kukaa na wewe uzeeni? Hata watoto wako mwenyewe wanakukwepa!

6. Sana watakutafutia mfanyakazi kukutunza na kumlipa kwa shida, maana hata wao maisha yamewakazia!

7. Hata mti ukiwa mdogo unamwagiliwa maji, ukikua wanaanza kuukata matawi na ukiwa mkubwa zaidi watasema unaleta bundi tuukate.

8. Unaona hiyo? Uzee siyo mzuri sana. Kila mtu anaukwepa.

9. Utasikia kabinti kanasema NIMPELEKE WAPI HUYO BABU? Kwani kibabu hakina haki ya kupendwa na mabinti?

10. Au Kakijana hata hela hakana, kanakula kwao unakuta kamekomaa HUYO BIBI KIZEE WA NINI SASA? Kwani Bibi Kizee hana haki ya kupendwa na vijana?

11. Sasa kijana oa mzee uone utakavyoshambuliwa na jamii utadhani wao ndo wamemuoa.

12. Utasikia, KAROGWA SIYO BURE. KAFUATA HELA! Kipenda roho hula nyama mbichi jamanii.

13. Hali huwa ni mbaya zaidi kama umri umekwenda na pesa huna. Watakuita mchawi ili tu kukutafutia gap la kukuua.

14. Hata watoto wako uliowazaa mwenyewe wanakuwa mbali na wewe.

15. Mwanao wa kumzaa anagonga miaka mpaka 15 hajajaja kwaona. Atakuja mkifa!

16. Kwa sasa anaogopa kuleta watoto kwenu mtawaroga. Vijukuu ni vyako lakini hivijui,havikujui, na wakali ulijinyima kumsomesha mzazi wao😄

17. Na ikitokea amekuja hana muda na nyie maana mmezeeka.

18. Atakuwa busy na washikaji zake mpaka unajiuliza alikuja kufanya nini? Si bora arudi alikotoka?

19. Halafu utasikia UTU UZIMA DAWA! Labda dawa isiyotibu kitu.

20. Sasa sikiliza dogo, tumia ujana wako unavyoona ila kumbuka kujiwekea vya kula uzeeni.

21. Siku za uzee wako haziko mbali! Miaka inakimbia kweli.

22. Umri unakimbia sana na na bado tunapoteza muda. Na siku hazigandi kila kukikucha afadhali ya jana.

23. Umri una mbio mnooo. Yaani kabla hujakua kua vizuri umezeeka!😄😄😄 Jamani.

24. Umemaliza chuo juzi tu lakini leo una mtoto anataka shule za kwenda na gari la njano.

25. Kufumba na kufumbua dogo anadai ada ya chuo kikuu maana amenyimwa mkopo.

26. Kumbuka uzee unakwenda na nguvu zako.

27. Jinsi umri unavyozidi kusonga ndivyo nguvu za miguu zinavyozidi kupungua. Hii ina maana gani? Tupunguze kutembeatembea! Kuna umri hutakiwi kwenda kila sehemu.

28. Jinsi umri unavyozidi kusonga ndivyo nguvu za macho kuona zinavyozidi kupungua. Hii ina maana gani? Tupunguze kuangalia angalia! Kuna vitu umri ukiishasonga sana hutakiwi kuviangalia.

29. Jinsi umri unavyozidi kusonga ndivyo nguvu za mikono zinavyozidi kupungua. Hii ina maana gani? Tupungeze kushikashika! Kuna vitu mzew hutakiwi kushika.

30. Jinsi umri unavyozidi kusonga ndivyo nguvu za meno zinavyozidi kupungua. Hii ina maana gani? Tupunguze kutafunatafuna! Kuna vitu mzee hutakiwi kula.

31. Jinsi umri unavyozidi kusonga ndivyo nguvu za maskio kusikia zinavyozidi kupungua. Hii ina maana gani? Tupunguze kusikiasikia! Kuna vitu umri ukienda hutakiwi kuvisikia maana utakufa.

32. Jinsi umri unavyozidi kusonga ndivyo nguvu ya kutamani vitu inavyozidi kupungua. Hii ina maana gani? Tutulie nyumbani na kula akiba tuliyojiwekea ujanani

33. Kuna hii chati ya umri naipenda sana;

34. Mwaka 1 hadi 5 Ni umri wa kula bure, umri wa kujifunza chochote kwa kuiga wakubwa. Umri huu hauongozwi na akili, unaongozwa kwa kuona.

35. Miaka 6 hadi 10 Ni umri wa kujenga tabia ya mtu. Ni umri muhimu sana maishani. Tabia unazojenga hapa utaishi nazo milele.

36. Miaka 11 hadi 17. Ni umri wa makuzi na matamanio. Ni umri wa kuanza tabia za chumbani.

37. Miaka 18 hadi 25 Ni umri wa ndoto kubwa za nia njema na matarajio makubwa. Hapa unakuwa na ndoto za kuwa bosi flani hivi, kumiliki vitu vya thamani, rubani, daktari nk).

38. Miaka 26 hadi 30 Ni umri wa wa ujuaji na kukosoa wengine; umri wa lawama nyingi na visingizio lukuki.

39. Miaka 31 hadi 35 Ni umri wa majuto na roho mbaya; umri wa kutengwa au kujitenga na mambo yako. Unajiona so spesho.

40. Miaka 36 hadi 40 Ni umri wa majukumu; hata matumizi ya pesa ni ya kikubwa. Ubabehave kiutu uzima. Mzee wa busara.

41. Miaka 41 hadi 45. Ni umri wa kujaribu nafasi nyingine ya mwisho kwa tahadhali kubwa kama ulifelo. Ni umri wa masahihisho kwa walioharibu, lakini ni umri wa kula maisha kwa waliojopanga. Wanasema life bigins at 40.

42. Miaka 46 hadi 50. Ni umri wa liwalo na liwe. Hakunaga majuto hapa. Una hela huna hela poa. Umesoma hujasoma potelea mbali.

43. Miaka 51 hadi 60 . Ni umri wa utulivu na kumtegemea Mungu. Umri wenye hofu na dunia. Umri wa kujilinda sana kiasi kwamba hata ukisikia mkeo au mmeo kachepuka unaona haikuhusu. Hutaki shida.

44. Miaka 61 hadi 70. Ni umri wa upatanisho wa imani na jamii. Umri wenye ushauri mwingi. Mahudhurio ya nyumba za ibada ni mazuri sana.

45. Miaka 71 hadi 100. Ni umri wa kuwaza kuondoka duniani. Maongezi yako hayamaliziki bila kutaja kifo.

46. Miaka 100 na zaidi. Ni umri wa pambo la nyumba. Yaani huna utofauti na picha ya ukutani au pambo la nyumbani.
 
Duh! Ina uma sana ukifika kwenye umri wa liwalo na liwe, hapo kama hujaoa sijui utamuoa nani kama si kukimbilia mabinti wadogo walau upate watoto wawili wa kuingia uzeeni. Maana wa zaizi yako ni wazee na wamekoma kuzaa kwani wamefikia ukomo hawapati hedhi tena kuwaoa ni kutaka ushirika usio na matunda(watoto). Labda uoe wa kukupa joto uzeeni ambaye ni mzee mwenzako
 
Uzeeni ni jambo la barka kubwa kwa kuwa wachche ndio huruzukiwa Uzee

kwa Tanzania Aged above 65 is less than 5% kwanini tusimshukuru Manani kwa bahati hiyo.

Jambo la msingi ni kuwa unajiandaa kisaikolojia kadri umri unavyosogea.

Ukiona Mwanafamilia mmojawapo wapo anaona kero kuwa karibu nawe, Mie huwa namsaidia kwa kukaa nae mbali hadi anajistukia

Jambo la msingi omba Mola asikutie msukosuko wa Maradhi ya mwili na ya Uchumi …ukiepuka maradhi hayo Mawili Wewe huna haja ya kuwa Mnyonge


Mie naweza kukaa ndani hata three days natoka kwenda Masjid, kufanya mazoezi na kushinda kwny mitandao nafurahi tu kwa update nikichoka nazungukia vijishughuli uchwara



kujaribu ku attach furaha ya nafsi yako kwa mtu mwingine ni kosa nililiepuka katika umri mdogo sana na Alhamdulillah nimefanikiwa kwa kipindi chote


umri umesogea unaenda kukimbizana na biashara ya Makuku ya kisasa ambayo ni stress kuanzia kuyakuza hadi kwny masoko kwanini usipate sonono?

unaenda sijui kulima matikiti unapambana hadi unavuna unafika buguruni unakuta mwenzie ana fuso mbili zimepaki zimejaa tikiti zilizokosa soko hadi Mzigo umeoza anabishana na wenye gari gharama za kupeleka dampo mitakataka hiyo.
 
Taabu yote ya nini kuzeeka mpaka kuwapa watu wengine shida? Pale itakapofikia viungo vya mwili vinashindwa kufanya kazi yake kwa ufanisi kutokana na uzee bora kumuomba Mungu akuite mbinguni tu
 
Back
Top Bottom