Hospitali za Serikali zimekuwa zikitumia vijana waliomaliza intern (post intern attachment) huku wakiwalipa hela kidogo sana

Thecontingent999

New Member
Mar 20, 2024
2
0
Habari.

Kuna rafiki yangu mmoja amemaliza internship ya udaktari mwaka jana katika hospitali ya rufaa ya Morogoro na kabla ya wao kumaliza hospitali iliomba watu kumi waandike barua kwa ajili ya kujitolea na wakaiita (post intern attachment).

Kwa kawaida watu wanapochaguliwa kujitolea huwa wanapewa hela kama mshahara ambao unaendana na muongozo wa serikali na serikali huwa inawatambua kwasababu ndo watu inawatumia siku hizi katika sekta ya afya kuliko kuajiri watu.

Muongozo huwa unasema walipwe Tsh. 690,000 kila mwezi na huku wakipewa hela za extra duties na night calls kama waliyo wengine.

Lakini kwa vijana hawa ambao ni madaktari wanalipwa Tsh. 420,000 kwa mwezi bila hizo hela zingine na maisha yao yamekuwa magumu sana haki.

Wamejaribu kuomba kwa viongozi angalau kama wanapewa hela ndogo hivyo basi wapewa za extraduties na night calls lakini uongozi umekataa kabisa kufanya hivyo.

Wanaomba Ummy Mwalimu awasaidie maana wanapitia wakati mgumu sana huku wao ndo wanaotumika sana kwenye hospitali ile kuliko hata waajiriwa.
 
Leseni wanazo na pia wakujitolea huwa hawangalii leseni kwasababu kuna malipo ya mwenye leseni na pia asiyekuwa na leseni.
Sema kama wanaona malipo madogo si waache ? Huo mshahara walikuwa wanaujua since mwanzo hawajaanza kazi, wakaamua kufanya kazi hio hivo hivo, saizi wanalalamika,

Anyway, siungi mkono mishahara midogo ila hao madogo wana shida zao na walizingua toka mwanzo
 
Back
Top Bottom