Mbu
JF-Expert Member
- Jan 11, 2007
- 12,753
- 7,845
- Thread starter
- #21
Duh hiyo bold imenikamata sana, well mi nadhani ni mtu kushindwa kuelewa au kujua anataka mwnza wa aina gani, anajiingiza kwa mtu na kuanza kumsoma wakati anakuwa tayari kwenye mahusiano, cha muhimu ni mtu ku focus, kujua nini ni nini, na kitu gani hakipendi......kuchagua mwenza sio jambo la kukurupuka, wengi wetu tunafanya maamuzi ya haraka na kuja kujuta badae, tunapokatishwa ndio tunaanza kujutia maamuzi yetu, mwisho nahitimisha "hakuna kuharibiwa maisha na mtu ni wewe mwenyewe ndio ulijiharibia" kwa kushindwa kuchagua nazi mpaka ukapat koroma
Nice Gaga,
hapo kwenye kosa la kujiingiza kwenye mahusiano kwanza, kisha unaanza kumsoma mtu ndio kosa mojawapo!
Lakin i hebu twende mbele tukirudi nyuma. Mfano; wazee wetu wa miaka ya 60s kurudi nyuma, wengi hawakuwa Boyfriend na Girlfriend kwenye ujana wao. Wengi wao walikutanishwa through mawifi, mashemeji, mashangazi nk...
Wengi wao walioana na kuja fahamiana ndani ya ndoa. Wengi wao wameleana mpaka vifo vinawatenganisha.
Tatizo lipo wapi miaka hii ya leo kiasi kwamba "tunaona kuna umuhimu wa kufahamiana kwanza" kabla ya kuoana?
Je, ni muda gani unahitajika kumfahamu mwenzako ndipo muoane? na kujiridhisha nini mnataka maishani?
Bado nataka kuamini nhili neno 'umeniharibia maisha' halina maana yeyote kwa anayelitamka ila kukupandikizia lawama.